Naomba Msaada wa kujua Brand bora ya TV ya kununua kwa sasa

Hii kampuni ya Hisense ni moto, ninayo inchi 43 hakika sijawahi jutia kuwa nayo
 
Nina LG yangu nchi 49 imekufa kioo, ni wapi nitapata mkuu....na bei ikoje.
😂😂😂 yale yale nimetokaa kuongea hapa ! Ww ungekuwa na hela hiyo tv wala usingekuja hapa kuulizia ni wapi utaenda kutengeneza maana sehem ni nyingi ila garamaa ndo itakutoa ushuzii... hao wanaokuambia kariako usifikiri ukija huku ni mteremko... watu wanafanya kazi kwa kujuana ... fundi anaweza kuenda akamaliza kila kitu kwa laki mbili na nusu ila ww nenda uskie bei zake ! Wakikiona tuu bei utakayotajiwa utaona bora ujipinde ununue nyingine .... cha msingi mtafte fundi unae mwamini mpee kazi ili incase of anything unaweza ukapambana nae
 
Mafundi wazuri wako wapi, maana hilo ndo la msingi kwangu......gharama haiwezi kunishinda.
 
Ya nini kuchukua tv ya gharama, yenye uwezo wa 4K na specifications zingine Kali Kali,alaf unaenda kuangalizia sinema zetu?

Chukua tv ya kawaida tu, then kula maisha. Itadumu kutegemeana na umakini wako tu.
[emoji23]
 
Nina LG yangu nchi 49 imekufa kioo, ni wapi nitapata mkuu....na bei ikoje.
Mkuu hayo madude yakisumbua kioo achana nayo tupa nunua nyingne tofauti na hapo utakula hasara na tv haiponi.
Samsung yangu iliharibika kioo nikaenda kwa dealer akasema kioo ni laki 4 ,nikatoa pesa kioo kikaagizwa lakini bado tv haikuwaka nikaamua kuachana nayo nikavuta Sony ndio nipo nayo
 
Asante
 
Mafundi wa kibongo chenga sana, ni bora angejaribu na kioo cha TV nzima kabla ya kuagiza......ukiona hivyo hawawezi kufanya diagnosis ya tatizo la kioo, wanabahatisha bahatisha tu.
 
Chukua Samsung Smart 65 Inches ni safi kabisa kwa muda wa miaka ipo palepale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…