Naomba Msaada wa kujua Brand bora ya TV ya kununua kwa sasa

kama bajet ndogo tulia kwenye boss tu inakutosha... kumbuka kkoo bei nyingi za tv ni kulingana na duka,uongeaji wako na muuzaji uliyekutana naye...
nenda na hii akili inchi 32 usinunue juu ya 250k na hizo 40 kwa 43 usivuke 650k kwa hiz zisizo smart
 
Nunua Tv mpya mkuu acha kuangaika Tv zimeshuka Bei Sana
Watu wanunua Nchi 43 kwa 350k sasa sijui unaangaika Nini??
Naogopa sub-standard mkuu, maana hii ya kwangu nchi 49 LG nilinunua 1.5m kariakoo, ilikuwa mwaka 2016...
 
Mh
Kwahiyo unatupa bei za China?
Labda ziwe zimeshuka disemba hii.
Ila hapo Nov mzigo ulikuwa vile vile tu.


Tv zimeshuka Bei Sana sijui Kama mnajua Hilo tatizo watu hata hamsafiri siku mkifika huko China mtashanga Sana Bei ya hivyo vitu.
 
Tv zimeshuka Bei Sana sijui Kama mnajua Hilo tatizo watu hata hamsafiri siku mkifika huko China mtashanga Sana Bei ya hivyo vitu.
Nakuelewa sana waitu, siku ukienda holiday huko ulaya nishtue nikuagize TV ya kisasa kabisa.......mimi mtani wako sijawahi kabisa kupanda ndege.
 
Star-X watu wanaichukulia poa sana, sijui kwa sababu haina promo!? Ni non-made in china, ina bass, full HD ila watu kwa sasa wamekalili Hisense
Iko vizuri sana hiyo. Na sio hiyo tu, nakumbuka 2013 nilinunuaga Iris inch 32, tena used Toka kwa mtu. Ipo inafanya kazi mpaka leo.

Hiyo star X nilinunua 2019, mpaka leo inadunda
 
Hakuna nyingine zaidi ya ulizozitaja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…