Naomba Msaada wa kujua Brand bora ya TV ya kununua kwa sasa

We Kama upo DSM nenda kariakoo maduka ya wachina utapata Tv Bei sawa na bure Mimi Nina miez tisa nimechukua 320k nch 40 LG
Mkuu ulipata 40 inches kwa only 320k??
 
kama bajet ndogo tulia kwenye boss tu inakutosha... kumbuka kkoo bei nyingi za tv ni kulingana na duka,uongeaji wako na muuzaji uliyekutana naye...
nenda na hii akili inchi 32 usinunue juu ya 250k na hizo 40 kwa 43 usivuke 650k kwa hiz zisizo smart
Asante
 
Hapohapo kwenye kioo
Hisense Tv inchi 42 kioo kimepasuka
Mwenye anaweza nielekeza kwa kukipata kipya ninunue ...na bei gani kioo na matengenezo???
 
Hizo brands kubwa Sina hakika kama zina TV za DC&AC kwenye mzunguko kibongobongo hivyo nilinunua brand "uchwara" ya kichina kwa ajili ya matumizi ya sola na ni miaka 8 sasa hakuna changamoto yoyote si picha si sauti.
 
Tv zote kubadili kioo ni zaidi ya asilimia 50 ya thamani halisi ya tv, kikawaida tv kubadili kioo si uamuzi wa busara, ndio maana unaona nadra kukuta spare za vioo.
 
Budget, ukubwa wa TV unayotaka na matumizi yako ni information muhimu kwenye huu uzi wako.
 
Wakuu TV langu haliwaki Samsung msaada tafadhali kwa mafundi wazuri wa TV.
 
Tv zote kubadili kioo ni zaidi ya asilimia 50 ya thamani halisi ya tv, kikawaida tv kubadili kioo si uamuzi wa busara, ndio maana unaona nadra kukuta spare za vioo.
Ivi mkuu TV ikizingua kuwaka tatizo inakuwa ni nini? Yani ukiwasha inajizima enyewe. Nimekosa uhondo wa epl tangu krismass Samsung tv yangu inazingua
 
So Achukue ya bei gani?
1. Hisense
2. Solarmax (Hii nilienda na mtu kununua kkoo kitambo kidogo, wakatupa na warranty ya mwaka mzima, mpaka sasa bado inadunda, tulichukua yenye double screen).

Kikubwa nimeona kama hauna mambo mengi na upo sehemu ya utulivu, hizi za TCL, Boss n.k zinadumu vizuri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…