Naomba msaada wa mtu kunidhamini nipate kazi GardaWorld Security

Nimejikuta napata maswali mengi yasio na majibu kama:-

Hivi kweli umekosa mtu wa kukudhamini katika watu wanao kuzunguka?

Nikweli umekosa mtu wa kukudhamini kati ya ndugu ulionao?

Hata unapo sali umekosa mdhamini kweli?

Nikweli umekosa jirani hata rafiki wa kukudhamini hadi uje hapa mtandaoni?

Mkuu, dhamani ni jambo kubwa na sio dogo kama unavyolidhania, na ili kumdhamini mtu ni vyema ukamfahamu kwa undani aiseeee.

Yes, unahitaji msaada lakini ebu jaribu kutathmini hili unalohitaji kusaidiwa tena na watu ambao hamfahamiani.

Kama nimekukwaza samahani mkuu...πŸ™ ila nimejikuta nawaza tu.
Anyway, I wish you all the best.
 
Mungu akutangulie uweze kufanikisha jambo lako ingawa suala la kupata mtu wa kukudhamini kwenye kazi ya ulinzi sio jambo jepesi.

Sikukatishi tamaa ila ni ngumu sana kupata mtu wa kukudhamini ikiwa hakufahamu kiundani kuhusu tabia yako na mambo mengine.

Kumbuka unaenda kulinda mali za mamilioni na bahati mbaya ikitokea wizi wa hizo mali katika eneo lako la kazi basi jua tu kwamba mdhamini wako atakua responsible na kutokana na hali hiyo ni ngumu kumpata mtu akudhamini kwasababu tu utampata chochote kitu kama kifuta jasho.

Nakushauri nenda kwa watu wako wa karibu wanaokufahamu tabia zako zungumza nao na nina imani watakusaidia lakini kwa hapa mtandaoni kupata hitaji lako ni ngumu sana labda itokee tu.
 
Kampuni haiwezi kuzijua kiundani tabia za wafanyakazi wote au waomba kazi wote, kwa maana hiyo wanaweka kigezo cha wadhamini wakiamini ni watu wanaowajua vizuri wanaoomba kazi kwa kiasi cha kuwa tayari kuwajibika kwa niaba yao kulingana na matakwa ya sheria yanavyoruhusu.

Kwa kifupi sana, njia nzuri ya kupata mdhamini ni kudili na watu wanaokujua vizuri miongoni mwa watu wako wa karibu.

Hili unalionaje Mkuu? Au kama umeshafanya hivyo kipi kimekukwamisha?
 
Kama wewe ni mtu mwema kwa jamii inayokuzunguka huwezi kosa mdhamini, kuanzia msikitini, kanisani, mjumbe nk. Tofauti na hapo hapa jukwaani si rahisi kupata mtu wa kukudhamini, udhamini kwenye kazi hizi za ulinzi haushii kwenye makaratasi, unaenda mbali zaidi kwamba aliyekudhamini anabaki na dhamana endapo ukikoroga huko kazini. Ukizingatia ukiwa lindoni na ukatokea wizi wewe ndo mtuhumiwa namba moja. Na kwa kuongezea tu ukipata kazi utambue kuwa kila unapokuwa lindoni kuna makosa matatu tayari kinachosubiriwa ni chaji kuandikwa tu, nayo ni Uzembe kwa kushindwa kuzia wizi, ( 2) Wizi wa kuaminiwa (3) Kushawishi na kushiriki wizi.

Pia kama utashindwa kupata kazi hapo Gurda kwa hayo masharti nafuu hivo G4s hata usisogee make wale hawataki mdhamini ndugu, na kama ni ndugu awe mfanyakazi serikalini na aandike barua na igongwe mhuri wa ofisi husika, Mdahamini wa pili lazima awe ni Mjumbe wa nyumba kumi au mwenyekiti wa serikali ya mtaa.

Somo jifunze kuishi na jamii inayokuzunguka, shiriki kwenye jumuiya mbali mbali mtaani kwako. Naongelea jumuiya siongelei makundi.
 
Ninao wajua vzr hawana sifa wapo km mim tu mtafutaji hawana lesen za biashara wala kuajiriwa sehem kwamba wana kitambulisho cha Kazi..hiyo ndio shida

Sawa Mkuu, endelea kumulika naamini atapatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…