Boss vipi hali ya maisha yako?
Unakula milo mitatu?
Hautingwi sana na masula ya kutafuta kipato?
Una mke au mwanamke ambae unakuwa nae yeye tu na unamuamini?Unaweza kuwa unapata hofu za magonjwa n.k no haki ya kawaida.
Unatumia kitu chenye addiction kama sigara,pombe n.k(punguza sana,au acha ukiweza)
Suluhisho jepesi
1.Acha kujishuku, nimeona umejibu kuwa unarudia mara 2 japo wazungu wanawahi kutoka...mpaka hapo hali sio mbaya.
2.Kula vizuri na kwa wakati, kula mboga mboga na matunda kila siku, ndizi mbivu mbili hivi.
3.Jipumzishe na usiwaze sana kuhusu hilo,kuwaza kwako kunakupa hofu...
4.Endelea na mazoezi, ukienda kuoga chukua maji ya moto kidogo(sio sana) lowesha kitambaa bandika katika mzee kwa dakika kadhaa, kisha oga maji ya baridi kwa siku kama tatu hivi.
5.MUHIMU:Unapoingia kulala lala ukijaribu kuacha kuwaza sana, lala ukiwa na faraja ya kumaliza siku salama na kuamini ukiamka kesho utakuwa na nafasi nzuro zaidi ya kupigania unayoamini.
Haya sio masuluhisho ya kidaktari, ni mbinu tu za kawaida na zinafanya kazi