Naomba neno moja tu la Kingereza ambalo halina tafsiri rasmi ya Kiswahili

Hiyo archimesdes principle imekaa vibaya akili ya mtoto inaweza ikafikiria mambo mengine kabisa tofauti na mada husika.
 
Hapana! Orodha nyeusi Si tafsiri sahihi ya neno blacklist. Tafsiri sahihi inapaswa kuwa ' orodha ya nchi korofi/ kaidi'.
Hapo neno nchi limekujaje/limetokea wapi?
Kumbuka hata kwenye simu yako kuna blacklist pia kwenye phonebook.
 
1. Adverb (really, indeed, truly, etc)
Kwani ameanza kuondoka?
Kwani wewe huoni?

2. Conjunction (since, for, because)
Anatafuta njia ya mkato kwani muda umemwishia.
Asante sana.Nimeelewa sana hiyo ya pili.Kwa urahisi sentensi hii "kwani hauji?" inaweza kutamkwaje kwa Kiingereza bila kupoteza maana iliyokusudiwa.Maana naona kama nikisema "..really/indeed/truly you are not coming?"inakuwa inaleta tafsiri ya "kweli hauji?" badala ya "kwani hauji"
 
Mkuu yapo, tena ni mengi tu, mathalani yafuatayo,
1. Achilles heel
2. Mutatis mutandis
3. Ceteris paribus
4. Dsyfunction
5. other technical jargon
6. n.k, n.k
 
Naomba nibadili mada kidogo. Vipi machawa nao wanaitwaje kwa kingereza
 
Ili tuelewe nini kinakusudiwa hapa, tuangalie mazingira fulani ambapo mtu anaweza kuuliza: ^Kwani hauji (huji)?^

Mmekubaliana kufika mahali fulani, labda kwenye mkutano. Kabla ya muda mwafaka, mtu huyo anakwambia:

^Mkitoka mkutanoni, nijulishe tafadhali.^

Ndipo unaweza kuuliza: ^Kwani huji?^

Hii ni namna ya mshangao fulani, sawa na ^Kwa hiyo huji?^ ama ^Ina maana huji?^ ama ^Ndiyo kusema huji?^

Inglishi yake inakuwa:
Does it mean you aren't coming?

Mifano mingine:
1. Does it matter? - kwani ina umuhimu (umaana) wowote?

Ukiangalia hapa Kiswahili cha ^kwani ina muhimu,^ hubeba dhana ya mshangao na msisitizo.

Tunaweza kusema kwamba neno ^kwani^ halionekani vizuri katika muundo wa Inglishi.

2. Must you kill? - kwani lazima uue? (Hivi lazima uue?)

3. Kwani ulikuja saa ngapi wewe? - wait a minute! At what time did you come?

Dhana ya wait a minute au tu wait (subiri kidogo) ni ya mshangao wa muulizaji ambaye pengine hakumtarajia muulizwaji awe amefika mapema hivyo.

Hii imejumuishwa kwenye neno kwani, ambayo akilini mwake ni udadisi wa mambo yanayomshangaza muulizaji.

Kwa ufupi, mantiki husika ndizo zinatupatia dhana ya really, indeed, wait a minute, nk

Ikumbukwe kwamba neno moja la lugha fulani linaweza kuwa na maana na mantiki pacha au zaidi katika lugha nyingine, kama ambavyo tumeona matumizi ya kwani hapa.

Dhana inayobebwa katika neno fulani inaweza isitimilike kwa neno lilelile la lugha ya pili kiasi cha kuhitaji muundo wa maneno mengine ili kutimilika ipasavyo.

Kama tungekuwa tunapambanua lugha hizi mbili kwa kuzingatia neno kwani na vitafsiri vyake katika Inglishi, tungesema kisahihi kwamba Kiingereza ni dhaifu au kimepwaya kuliko Kiswahili.

Kwa kuzingatia hilo, ulazimishaji wa kila neno liwe na neno lake kamili ilhali tukitarajia maana halisi ya tungo husika ibaki kama ilivyo, humithilisha jitihada dufu za kujaribu kuyavuka mafuriko kwa kiperea.
 
Kiswahili Ni lugha change Sana ambayo Haina misamiati mingi.
Kutafsiri kila nomino/ neno kutoka kwa kiingereza Hadi kiswahili Ni Jambo gumu Sana.
 
Sio kweli mhandisi wa ndege anaitwa Aircraft Engineer
Wote ni wahandisi wa ndege wana utofauti kidogo sana kwenye uwanda wao wa maeneo ya kazi.
Aeronautical Engineer anahusika na ndege zote zinazoruka kwenye anga la dunia wakati Aircraft Engineer/Aerospace Engineer anahusika na ndege zote zinazoruka kwenye anga la dunia pamoja na ndege zinazoruka nje ya anga la dunia.
 
Asante sana
 
Radio call

Kama kumbukumbu yangu ni nzuri, nafikiri kipindi cha nyuma kabisa kabla ya simu za mkononi, Radio call ilikuwa inatumika sana na vyombo vya dola. Kwa maana hiyo, nafikiri tafsiri yake ni

Radio call - simu hewa

Asante kwa mchango wako.
 
Kiswahili Ni lugha change Sana ambayo Haina misamiati mingi.
Kutafsiri kila nomino/ neno kutoka kwa kiingereza Hadi kiswahili Ni Jambo gumu Sana.

Observation nzuri sana. Ila swali kwako na wanajamii ya Kiswahili kwa ujumla ni,

Kama ni jambo gumu, ina maana haliwezekani kufanyika? Kama linawezekana, nani afanye wakati waongeaji wakubwa wa Kiswahili fasaha ni sisi?

Mchango mzuri. Tuendelee...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…