Bechede
JF-Expert Member
- May 3, 2020
- 872
- 2,422
Ni kweli wengi sana wamehamia bongo au wapo kwa muda. Ukiingia youtube utawaona kibao, nilichogundua lakini wengi wao hawajajipanga na hawana jambo la maana wengi wanaishia kuwa youtuber tu kuonyesha hali ya maisha ya africa vs US ni kama trend fulani huko kwao wanajisifia sana kuja africa (wenyewe wanaita motherland).
Wengi wao ukifuatilia wanasema wamekimbia ukandamizwaji wa watu weusi huko kwa Biden (police brutality) na ubaguzi. Lakini kipindi hiki cha c19 wengi wamekimbilia sababu ndio nchi pekee ambayo haina lockdown au masharti ya kukaa ndani.
Kwa ujumla kuna wimbi la wamarekani weusi kuja afrika.
Youtube wamejaa, cheki huyu mmoja.
Baada ya kuona post yako Duksi , imebidi niangalie baadhi ya video mbalimbali youtube kuhusiana na mada tajwa hapo. Nami nikaamua kusumaraizi na kuongezea kidogo.
Hao wamarekani weusi wamejaa wengi sana tena wengine wamepanga mpaka uswahilini. Nimeangalia na nimefanikiwa kujua sababu kadha wa kadha zinazowafanya wamiminike bongo ikiwemo;
i). Ubaguzi ama police brutality huko Marekani kama ulivyosema.
Hapa kuna mzee anasimulia jinsi yeye na mtoto wake (kijana). Alikuwa anahadithia jinsi walivyokamatwa na polisi wa usalama barabarani na kuamriwa kwenda kituoni maana kuna msala walifanya kuwaudhi askari wetu wa usalama (hakutaja ni nini). Walichoshangaa ni pale waliporuhusiwa kuendesha gari wenyewe mpaka kituoni wakati huko kwao wangeoneshewa bastola na pingu juu huku ukiwa na hofu ya kuawa.
ii) Uponyaji wa kiimani (spiritual healing). hapa wengi ni wale wanaopenda mazingira ama nature.
iii) Bongo hamna mambo ya lock down
iv) Urahisi wa maisha. Mtu anapanga mansion kwa dola mpaka 800 wanaona ajabu sana wakati kwao kwa dola 2000 kupata tu nyumba ya kawaida ngumu sana labda upate kachumba tu wenyewe wanaita studio yaani ka ghetto ka kizushi.
v) Bongo kuna beach nzuri sana clear water haswa Zanzibar
vi) Kuna machaguo mengi ya sehemu za kukaa kwa kuzingatia hali ya hewa unayopenda mfano; wanaopenda baridi wanakaa Arusha na wanaopenda mjini wanakaa Dar kwa sababu ya malls ni nyingi na urahisi wa kupata kila unachohitaji
vii) Hii nchi ina amani sana na imetulia
viii) Vivutio vya kitalii ni vingi sana kuanzia Serengeti, mlima Kilimanjaro n.k
Licha ya kufurahi maisha yao hapa bongo na kusema sisi bongo ni wakarimu sana kwa kila mtu, baadhi wamekutana na tamaduni ambazo hawajazoea (culture shock) kwa mfano;
i) Suala la mavazi, waliozoea kuvaa vimini wanapata tabu sana
ii) Too much stare. Hahahaha... imenibidi nicheke kidogo. wabongo tunakodolea sana macho watu, ukipita mtu anakushangaa kama kaona sanamu, wanaona sio kawaida shangaa yetu ya kiajabu.
iii) Bongo ni ngumu sana kupata rafiki wa uhakika sababu wengi wanakuwa rafiki kwa sababu wanaona kama sehemu ya kitonga kupiga pesa za hapa na pale.
iv) wabongo tuko slow sana kwenye suala customer care, kila kitu ni pole pole tu
Pia matamanio yao makubwa kwa bongo ni wao kuweza kupata ardhi na kumiliki kama mzawa bila kupitia TIC (shirika la uwekezaji TZ). wao wanaamini wamerudi motherland sasa kitu kama hiki wanahisi hakijakaa sawa kinawabagua kimtindo. Wengine mpaka wameamua kuolewa na wabongo na sasa wameamua na kujenga nyumba za ndoto zao.
Hawa wamarekani weusi wanazidi kujaa si tu bongo bali Afrika haswa nchi ya Ghana, Gambia, Tanzania, Rwanda n.k na nchi ambayo ina mazingira mazuri sana kwao ni Ghana kwa sababu kule ilianzishwa kampeni mwaka 2019 inaitwa "A year of return" ilikuwa kwamba raisi Akufo Ado(serikali) inawapatia pasipoti ya Ghana, ardhi yako binafsi kwa ajili ya kujenga makazi yako n.k cha kushangaza bongo sio rahisi kama huko Ghana lakini wanajaa na wanaitana wengi sana.
Binafsi ningependa wajichanganye zaidi na wazawa na wawekeze katika maeneo mbalimbali kwani naamini kuishi kwao dunia ya kwanza watakuwa na exposure na ujuzi wa hali ya juu katika kuongezea uthamani kwa kuboresha uwekezaji wa kisasa nchini wasiishie kuwa youtubers tu, labda serikali ikiona mchango chanya toka kwao itaweza kuwapa kastatus fulani.