PostGE2025 Naomba niongee na vijana wa Tanzania, Gen-z

PostGE2025 Naomba niongee na vijana wa Tanzania, Gen-z

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Tulionya humu sana mda hauko upande wa watawala kwanini hakufanya maridhiano kabla 29 October tulionya humu mimi nimwombea kura humu. Nikatuma Maombi yangu lakini kimya
 
Tulionya humu sana mda hauko upande wa watawala kwanini hakufanya maridhiano kabla 29 October tulionya humu mimi nimwombea kura humu. Nikatuma Maombi yangu lakini kimya
 
Nichukue fursa na nafasi hii kuongea na vijana wa nchi hii..

Najua mioyo yenu inauma mmeumia kupoteza wapendwa wenu na wapendwa wetu pia lakini kuna jambo moja muhimu sana vijana wenzangu, amani na mshikamano ni kitu muhimu sana kwenye taifa lolote..

Yaliyotokea tarehe 29 yamewaumiza na kuwasononesha sana nichukue nafasi hii kumuombea msamaha kwenu Rais samia suluhu hassan kama yeye mwenyewe alivyoongea ameomba maridhiano na kuliponya taifa nawaomba tumuunge mkono na kumsapoti kwenye hili jambo muhimu sana.

Najua wengi mmeshakata tamaa na kuamua liwalo na liwe lakini naomba niwakumbushe jambo moja kwa upole na unyenyekevu Amani amani amani tumpe nafasi Rais samia ya kuweza kuirudisha tena Tanzania ile tuliyoizowea na kuisifia

Rais samia nae ni mzazi kama walivyo wazazi wengine na ni binadamu kama walivyo binadamu wengine ana teleza na kukosea hakuna mkamilifu apa duniani zaidi ya mungu pekee binadamu bora na mwenye hekima ni yule anayetambua kuwa amekosea na kukubali kurudi nyuma na kuangalia wapi amekosea amemuja na maridhiano ya kitaifa tumuunge mkono na tumsapoti ili taifa letu liweze kurudi kama lilivyokuwa mwanzo ..

Asanteni..
Mwambie atoke apige magoti chini aombe msamaha mwenyewe sio wewe unakuja kumuombea msamaha yeye mwenyewe anajua nini cha kufanya kabla ya kuongelea maviziano alibidi aombe kwanza msamaha kwa aliyoyafanya ndio aendelee na mengine yanayofuata baada ya kuomba msamaha na kuomba msamaha kuna mawili kukubaliwa au kukataliwa kwa hio awe tayari kupokea lolote kati ya hayo ila ili msamaha ukubariwe inabidi awasikilize wananchi wanataka nini aache kiburi na jeuri... asikilize wananchi wake wanachokitaka kujitia ukiziwi na yeye sio kiziwi wa kuzaliwa atazibuliwa mpaka atasikia
 
Lazima atafute maridhiano maana ndo yanaenda kufanya au kuhalisha Urais wake kwake lazima apambane juu chini apate maridhiano wasi wasi Mtandao wasije tena wakamuingiza mjini kama kwenye uchaguzi October 29 na kusababisha mauaji Tafadhali Usije kuingia maridhiano hewa akili inaitajika sana Maridhiano hewa ya propaganda na watu ambao hawana kibali cha watu ni kupoteza mda
 
Unawaza utumbo tu. Unajua wanademand vitu gani?! unajua ni mambo gani yamewafanya wawe hivo walivyo?! Kama unajua yaweke bayana pia, kama ujui tuliza vidole hivo.
Kama mtu ana njaa na anakuja kwako pekee ndio Kuna chakula ataanza Kwa kukuomba the first time........the tenth time atatafuta pakuingilia.
 
Back
Top Bottom