Naomba nisaidiwe tiba ya harufu kali ya kikwapa

Kunywa maji mengi tumia deodorant Nivea dry utaondoa tabu Kwa watu safi kabisa
 
Hiyo ni fursa ya kutengeneza dawa ya mbu
 
Hakikisha Nywele hazioti Kwapani, Gumia Magic kunyolea.

Harufu ya kikwqpa hutengenezwa na mgandiano wa uchafu kwnye nywele za kwapa.

Hakikisha huruhusu nywele kuota, muda wote uwe kipara,Mengine Fata utayoshauriwa ila usiache Fanya ushauri wangu.
 
Nenda hospital waambie wakuchome sindano ya BOTOX kwenye kwapa zote mbili, hilo tatizo litaisha.

Kuna uwezekano mkubwa kwa madaktari wachache sana wanaoifahamu hii tiba.
 
Ona mwamba.

Tambua kuwa unachokula ndicho kinachotengeneza harufu utakayotoa.

Ukipendelea kula vitu plain, basi utatoa harufu plain.

Ukila vitu vikali, harufu inatoka kali.

We chukulia tu kijambo cha anayekula pilau nyama na linganisha na wa mbogamboga na matunda🤔

Kadri unapokula vyakula vilivyochangamka zaidi basi na harufu inayotoka inakuwa imechangamka.
 
Vyote natumia
ratiba yangu ya kuoga ni mara mbili kwa siku
Nenda kamuone Dermatologist (daktari wa magonjwa ya ngozi) akuchome Botox injection kwenye kwapa.
Deodorants, limau, ndimu, chumvi etc etc haziwezi kuondoa hilo tatizo.

Choma kwanza hiyo Botox ndio utumie hizo deodorants.

Ni PM ili nikuelekeze vizuri. ………
Tuwasiliane.
 
Kama unaweza hamia mkoa wenye hali ya hewa ya baridi na low humidity kama mikoa ya kanda ya kati.

Sehemu zenye joto na humidity kubwa kama Tanga, Dar, Pwani na kusini kunaongeza tatizo.
 
Nenda hospital waambie wakuchome sindano ya BOTOX kwenye kwapa zote mbili, hilo tatizo litaisha.

Kuna uwezekano mkubwa kwa madaktari wachache sana wanaoifahamu hii tiba.
Botox inazuia jasho kutoka, harufu inasababishwa na bacteria, bado atakua hajatibu chanzo.

Pia botox inaishia after every three months kama sijasahau.
 
Botox inazuia jasho kutoka, harufu inasababishwa na bacteria, bado atakua hajatibu chanzo.

Pia botox inaishia after every three months kama sijasahau.
Combination ya excessive sweating (hyperhidrosis) + bacteria ndo shida.
Inabidi hiyo excessive sweating kwapani ipunguzwe kwanza ndiyo ifuatiwe na maswala usafi kwanza kusiwe na hao bacteria.
 
Kuna mti unaitwa mtopetope poli chukua majani yake yatwangetwange kisha nyoa kwenye makwapa vzr anza kuosha makwapa asbh na jion ndan ya mwezi tatzo hilo litaisha. Any way jaribu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…