Naomba niwasaidie watangazaji wa vituo vyote vya redio namna ya kutamka majina ya Kijerumani

Naomba niwasaidie watangazaji wa vituo vyote vya redio namna ya kutamka majina ya Kijerumani

Naona hili ni tatizo kubwa sana kwa watangazaji wetu wa vituo vyote vya redio kuanzia redio ya taifa mpaka vituo vidogo vya redio linapokuja jina lenye asili ya kijerumani matamshi yanakuwa ndivyo sivyo kabisa. Ni kama wewe umsikie mtu akitamka jina Juma kama Jima au Joma. Au jina Ali kama Hali, James kama Jemesi, Mwajuma kama Mijuma n.k. Hii inaleta ukakasi masikioni. Nitaanza na majina machache na kama yeyote anahitaji usaidizi wa matamshi ya majina mengine au hata maneno ya kijerumani dondosha kwenye uzi huu kwa msaada.

1. Naanza na hili liwasaidie hata walimu na wanafunzi wa fizikia ( physics).

Albert Einstein : Nguli wa fizikia na hisabati - Tamka ALBART AINSHTAIN. Katika sarufi ya kijerumani herufi e na i zikifuatana (ei) hutamkwa kama "ai" na s na t zikifuatana (st) hutamkwa kama "sht"

2. Frank-Walter Steinmeir: Rais wa Ujerumani - Tamka FRANK VALTA SHTAINMAIA. Kwenye sarufi ya Kijerumani herufi W hutamkwa kama tunavyotamka herufi V. herufi "r" ikikaa mwisho wa neno itamke kama "a".

3. Annalena Baebock: Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani - Tamka ANALENA BEEBOK. Kwenye sarufi ya kijerumani herufi a na e zikifuatana (ae) hutamkwa sawa na ule mlio wa mbuzi (meeee!). Mara nyingi badala ya herufi mbili ae huandikwa tu ä.

4. Jens Stoltenberg: Katibu mkuu wa NATO - Tamka YEENS SHTOLTENBERG. Kwenye sarufi ya Kijerumani herufi J hutamkwa kama tunavyotamka herufi Y.

5. Ursula von der Leyen: Raisi wa Kamisheni ya Ulaya ( EU Commission). Huyu sijui kama kuna siku inapita bila kutajwa. Ni watangazaji wa DW tu nimewasikia wakilitamka jina lake kwa usahihi. Tamka URSULA FON DEA LEYEN. Kwenye sarufi ya Kijerumani herufi V hutamkwa kama herufi yetu F.

6. Olaf Scholz: Raisi wa Ujerumani- Tamka OLAF SHOLZ. Kwenye sarufi ya kijerumani "sch" hutamkwa kama "sh" . Mfano: Kijerumani- Schule, Kiswahili- Shule

Natumaini uzi huu uwasaidie hasa watangazaji wetu maana matangazo yanaenda nje ya mipaka ya nchi pia. Kwa msaada zaidi dondosha swali lako hapa.
Hapa naona nikujisumbua tu, hao wazungu wenyewe hawana muda wa kupoteza kujifunza kutamka majina yetu.

Sent from my SM-A145F using JamiiForums mobile app
 
YYURGEN KLOP
ü ina sauti kama ya "yi". Inatamkwa like u with round lips. Unaweza kuangalia videos youtube andika German umlauts pronounciation. Zipo video nyingi utaona namna ya kukunja mdomo wako ili kutamka ä,ö na ü.
 
ü ina sauti kama ya "yi". Inatamkwa like u with round lips. Unaweza kuangalia videos youtube andika German umlauts pronounciation. Zipo video nyingi utaona namna ya kukunja mdomo wako ili kutamka ä,ö na ü.
Mwanangu nakubali hii lugha unaijua. Me nimeisoma kidogo, kwahiyo nadokoa kimtindo


Eg:-

Ich bin Number ni 26

Ich komme aus Tansania

Mein hobby ist lesen

Mein beruf ist.....

Ich bin.... Jahre alt




Mengine yatakuja tutakapokuwa tunaongea. Hapa nipo napiga hesabu zangu tu nidumbukie huko kwa wa "DEUTSCH" wenzangu [emoji1787][emoji3]
 
Mwanangu nakubali hii lugha unaijua. Me nimeisoma kidogo, kwahiyo nadokoa kimtindo


Eg:-

Ich bin Number ni 26

Ich komme aus Tansania

Mein hobby ist lesen

Mein beruf ist.....

Ich bin.... Jahre alt




Mengine yatakuja tutakapokuwa tunaongea. Hapa nipo napiga hesabu zangu tu nidumbukie huko kwa wa "DEUTSCH" wenzangu [emoji1787][emoji3]
Tuko pamoja mkuu. Ukikwama popote niulize. Ila Youtube kuna videos nzuri za kujifunzia. Pitia pia website ya Deutsche Welle wana masomo. Google " Deutsch, warum nicht".
 
CCM inatamkwa schicem
KINANA inatamkwa chinerner
Chongolo inatamkwa tshonglo.
Jifunzeni kiswahili nyie nzi wa kijani msiwe kama wenzenu nyumbu kila kitu ni kupinga tuu....bahati mbaya wa mizambarauni hata hawajui zzk wao anataka Nini.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom