Yupo mtu mmoja kwenye biblia anaitwa Yabesi, aligundua maana ya jina lake lilimaanisha huzuni, aliona inaweza ikamletea shida akawa amemwomba Mungu.
1 Mambo ya Nyakati 4
9 Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.
10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
Majina yanaweza kuumba kitu kama hutochukua hatua kama ya Yabesi, ila linaweza lisifanye kazi kama utakuwa na mahusiano mazuri na Mungu.
Tuwe makini na majina tunayoita watoto wetu, kwa sababu tumeona yanaweza kuumba kitu kibaya kutokana na jina hilo.