Naomba tumsaidie Joyce Kiria wa wanawake live. Anabomoa msingi wa taifa Bora

Kikubwa kinaanzaga na kidogo ndugu yangu, utajikuta umepata hasira ukamuua ukaishia jela na watoto wakateseka milele. So achaaa kabisaa kaeni mzungumzee
Kama ulishawahi kupitia machapisho ya domestic violence, sababu mojawapo kubwa ni gender inequality. Ni tatizo structural la kidunia. Ndio maana nilisema awali kwamba utatuzi wa hili tatizo unakwenda mbali zaidi ya yeye kuishia kuwashauri waathirika kuondoka nje ya ndoa kwamba labda ndio muarobaini.
 
Wakiachwa kuvumilia yenyewe hawawez wanaumia sanaa, roho ya mwanaume haijawahi kuaccept kuachwa kabisaaa ndo unakuta anakuvizia na kuua esp akiona umepata mwingine anayekupenda
Labda umuache akiwa hana pesa ndio utamkomoa 😆😆😆 ila vinginevyo ni sawa na kumpiga chura teke. Utaanzaje kulialia na koti limejaa pesa, ukiondoka asubuhi jioni mjengoni kuna mali safi imeingia 😅
 
Nahisi you have the wrong choice, if you have one goal why uongee Mara mbili??
Ndo maana nasema wanawake can be stupid at times. Unaweza kuwa very gentle ukawa na mtu mwenye pepo sijui. Unaongea kitu hicho hicho a million times ila still mtu atarudia the same mistake. I actually don't beat but i spank!

Ukiskia mtu kupigwa ni kama huyo aliepigwa manyuzi hadi usoni. Spanking ni kwa kuonya tu and i guess some women were designed for that!
 
Lakini hapo joyce anatoa maoni yake ka wewe unavotoa kwanini uone ni kosa mwanamke kutoa mtazamo wake kisa huupendi na yeye ni mtu mzima kwanini umpamgie Cha kufanya huo si ndio u dictator wenyewe.
Hyo ya simu na kuanzisha mahusiano mengine nje ya mahusiano sikuhizi ni fashion wanaume kwa wanawake wote wanashindana michepuko kwahyo ngoma droo tu, maana Imani imejengeka bila michepuko no marriage
 
Sawa ila mtazamo wake hautolei chumbani kwake, anauweka kwenye medias ambazo pia kuna options za kupinga ama kukubaliana nae kulingana na utashi wetu.

Hakatazwi kuongea na ndo maana ameongea yaujazayo moyo wake ila nasie upande wetu uheshimiwe vile vile sababu yeye sio malaika au nabii. Lazima tutoe maoni yetu kulingana na muktadha wa mada husika.
 
Tatizo kubwa la huyo dada and the likes ni kutozingatia misingi sahihi ya taaluma ya habari. Habari yoyote ile inayohusisha malalamiko juu ya mtu fulani ni lazima itafute upande wa pili (mlalamikiwa) ili ku-balance utimilifu wake kabla habari hiyo haijatangazwa wa hadhara.
Kwa kifupi kipindi chake kinapaswa kufungiwa kwa kukiuka maadili na taratibu za taaluma ya habari.
 
Unataka ndoa zivunjike kusudi ukachukue nafasi?
40% ya wanaume wanaonyanyasika ndani ya ndoa unaizungumziaje?
Sio kazi ya wanaume kuwapenda wake zao ila Wanandoa wapendane .
 
siungi mkono manyanyaso kwa wanawake

ila ushauri wangu kwa wanawake walio kwenye ndoa msichukue ushauri wa ndoa kwa wanawake walio achika hawa wanasumu mbaya, visasi na wivu kwa familia zinazo ishi kwa amani hivyo hata mkikwaruzana kidogo tu atakushauri uvunje ndoa yako
 
Mimi sio kichaa mkuu tafadhali sana. Mwenye kujua hili ni la kuachika au kuvumilia ni mwanandoa mwenyewe yeye Joyce anatoa maoni yake linalokufaa unachukua lisilokufaa unamuachia
 
Hivi mtu amepigwa hadi ametolewa meno au jicho tunahitaji kumsikiliza eti ilikuwaje hadi akamtoa mwenzie jicho??? Vipi visivyozingatia taaluma ya habari vinafungiwa kila siku kwani huoni? Hadi kimeachwa maana yake kipo sawa
 
Kilewo alijibebea gunia la misumari!
 
Unataka ndoa zivunjike kusudi ukachukue nafasi?
40% ya wanaume wanaonyanyasika ndani ya ndoa unaizungumziaje?
Sio kazi ya wanaume kuwapenda wake zao ila Wanandoa wapendane .
Nikachukue nafasi kwa mume wa mtu? Siwezi kuolewa na mume wa mtu mimi. Hao asilimia 40 wapaze sauti pia kama wanataka
 
Nimekusoma mkuu. Lakini kumbuka hata madawa ya kulevya yana uhitaji mkubwa japo yanaharibu.... na ndiyo maana yanazidi kushamiri. Niwe muwazi: asilimia kubwa ya migogoro ya ndoa hasa kwa nchi za dunia zetu za tatu inasababishwa na wanaume kuwa wakorofi. Mimi nadhani mwanzisha mada anataka kusema lengo la huyo mama liwe ni kujaribu kuondoa unyanyasaji kwa kwa njia zote kabla ya kufikia hatua ya kuachana. Uzoefu wangu unaonyesha kwamba wanawake waliokuwa kwenye ndoa zenye manyanyaso na wakaachana na waume zao wanakuwa na ile tendecy ya kushawishi kila mwanamke anayelalamikia unyanyasaji kwenye ndoa kuwa suluhisho liko kwenye kuachana tu. Hii inaweza kutokea kwa sababu pengine ndoa aliyokuwemo mumewe alikuwa katili sana hivyo inasabisha aathirike kisaikolojia na kudhani njia sahihi ni kutengana tu. Unajua hata mahamani inashauriwa ndoa ivunjike tu pale ambapo inaonekana hakuna suluhisho jingine.
 
Kwani sie tunaovumilia midomo yenu michafu ni vichaa ama? Ndoa ni uvumilivu...ndoa si lelemama! Kwa mtu ambaye anajua kwake subira ni mtihani basi asitake matatizo kabisa akae mita 200 nje ya taasisi ya ndoa.
Baba mimi nitavumilia njaa, dhiki, ugonjwa na mengine ila sio kipondo aisee mambo ya kutiana ulemavu kwa makususi nimekataa kabisa bora tu nikae mbali kama ulivyosema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…