Naomba tuongee UHALISIA kuhusu biashara ya Real Estate kutumia mfano HAI

Ni ndogo sana mkuu, uwekezaji na return haviendani!, Labda ni uelewa wangu mdogo katika biashara.
Wala sio uelewa mdogo mkuu, naheshim mawazo yako, ndio mana tunajadili, mfano wewe kwa two bedroom house yenye choo na bafu ndani uliyojenga kwa 70M, ungelirent kwa kiasi gani ?
 
Tatizo sio kuirent kwa bei gani mkuu, ila ningeona aina hii ya biashara ni ngumu kwangu
Ooh ok nimekuelewa. Wewe ungeifanyia nini hio nyumba mkuu ili ikuletee pesa
 

Asante mkuu kwa ushauri.
 
Hii biashara ni nzuri mkuu, usije kuthubutu kuuza hiyo nyumba, utajuta, kikubwa tuendelee kuvumilia tu pengine bank zitatambua biashara hii na kutoa mikopo...
Next time, nenda kanunue kiwanja eneo karibu na chuo alafu jenga chumba choo...wanafunz sio wasumbufu...
Usiuze nyumba
 
Kama utafanikiwa kuuza kwa 70; tafuta viwanja 5 @3,000,000=15,000,000/=; Jenga viwanja 3@18,000,000= 54,0000,000; Jenga kwa awamu awamu; Lot: chumba na sebule na choo ndani; malengo kiwanja kiwe na lot 4, ila utaanza kwa lot moja moja kwanza

Awamu ya kwanza hio Nimekupata mkuu, vipi awamu ya pili , narent kwa shilingi ngapi kwa kila nyumba
 
Nashukuru mkuu kwa ushari wako
 
Hii biashara ni nzuri sana kama utakuwa na uvumilivu, na pia isiwe ni biashara ambayo unaitegemea sana yaani uwe na biashara nyingine pembeni, ngoja niangalie filamu ya mama alafu nitarudi hapa na maoni kwa kirefu zaidi
 
Itategemea mazingira na mkoa uliopo
Mazingira inaweza kuathiri bei ya kukodisha nyumba? Kuna mtu anaweza kujenga nyumba nzuri sana ya kukodisha kwa laki 4, lakin sababu ya mazingira mkodishaji akasema atampa laki 1 ?

Lengo la kuuliza swali la bei sasa ya hio lot moja ni ili tuwe na uhalisia kwamba tumetumia milioni 69 kununua viwanja na kujenga hizo nyumba, sasa tupate kodi kwa kila nyumba kwa mwezi, ili tulinganishe na kodi ya awali ya nyumba moja kwa mwezi
 
Hapa ndipo nilipoona udhaifu wa biashara hii mkuu, unatakiwa kuwa Kama umefanya kwa ajiri ya kutunza pesa na sio biashara kwa ajiri ya faida.
 
35m ni nyumba kubwa; we unajenga chumba,sebule na choo tu
Suggested buying price?
Naomba kujua kama umejenga kwa 18 million, unaweza kuiuza shilingi ngapi..
 
mimi nishaanza tayari lakin hii biashara ni nzuri ukijenga na kuuza lakin kwa kupangisha ni ujinga mkubwa otherwise uwe na mtaji mkubwa sanaaaaaaaaa
Mkuu hongera, naomba kujua njia unayyotumia je imekupa mafanikio?
 
Hapa ndipo nilipoona udhaifu wa biashara hii mkuu, unatakiwa kuwa Kama umefanya kwa ajiri ya kutunza pesa na sio biashara kwa ajiri ya faida.
Kwahio wewe ungekua unahifadhi pesa tu kupitia hio nyumba? Kwa malengo yapi?
Kumbuka ni the only investment unayo inayokuingizia pesa. Utafanyaje uongeze nyumba zingine kwa kutumia Tsh 450,000 kwa miezi mitatu?
 
Nenda katumie hiyo nyumba kukopa benk, then njoo Nungwi pub tuipangie matumizi hiyo pesa. Kufa kupo maisha ni hayahaya hakuna maisha.
Bank gani wanakopesha kwa hati...mi naitaka hii haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…