Naomba tuungane kuanzisha Vitabu vya Dini ya Waafrika

Naomba tuungane kuanzisha Vitabu vya Dini ya Waafrika

Kabla ya ujio wa hizi dini waafrika walikuwa gizani wakimtafuta Mungu kupitia kuabudu vitu wasivyovijua in deep yaani nature kupitia matambiko kwa kuabudu milima, misitu, nk.
Sababu ya kuwa gizani wakimtafuta Mungu, shetani akatumia fursa hio akawamiliki kiimani akajifunua kwao kupitia mizimu , wao waliamini wanamuabudu Mungu. Kwa sababu shetani ndie mkuu wa ulimwengu, mwanadamu baada ya kutenda dhambi akatupwa duniani ambapo tayari shetani alikuwa ashatupwa duniani toka mbinguni,hali mwanadamu alitupwa toka bustani ya Eden.
Mwanadamu na shetani wote wapo duniani kwa mda mfupi sababu Dunia si makazi y kudumu kwa shetani na mwanadamu.Makazi ya kudumu ni paradiso na jehanamu.
Dunia si milele, ni temporary place, thus tunakufa mda ukifika.
We jamaa huoni kuwa umeandika ujinga? Huyo Mungu wenu mbona sasa aliwaacha waafrika nyakati zote? Unatetea upumbavu wa imani kuona kuwa huyo mungu mbaguzi alibaki na wazungu tuu akawaacha waafrika siku zote kabla? Mungu wa wazungu ni mungu wa mchongo sana
 
Uzuri wenzetu wana maelezo yanayojitosheleza yanayoweza tumika kujustify wakati wa kushawishi watu

Hiyo Miungu yetu sasa… hata jina hatujui

Hapo jumlisha role models

Wakristo wana Yesu, kwa Yesu wao huwaambii kitu

Waislam tuna Muhammad (pbuh)
Hutwambii kitu

Role model hawa kwetu ndiyo viigizo mtu akiishi ana strive kuwa kama Yesu au Muhammad hawa ni watakatifu

Hiyo dini ya Afrika nani mtakatifu?
Firauni? Ambaye toka tunakua tunafundishwa kuwa alikuwa na laana?

Nani atatenda miujiza ili tumwamini kweli katumwa na Miungu yetu😂
Maine mwanamalundi
 
Habarini,

Baada ya kupitia mijadala mingi humu JF na mitandao mbalimbali nimeona sasa kunaumuhimu wa kuungana sisi wenyewe Waafrika na kuanzisha dini/kanisa la Imani ya Waafrika/Washindi wa Afrika/Africa Catholic nk.

Hii ni kutokana na uwazi kuwa sasa Waafrika tumeanza kujitambua hivyo inatubidi kuweka maandiko yetu ya kiimani na kuabudu yatakayofundisha mambo mazuri na kuyaendeleza na pia mambo mabaya na kuyaacha kwa kufuata mfumo uleule wa kuzikataa dini na imani tulizoletewa na wakokoni wote kwani siyo rahisi kuzikataa pasipo kuanzisha ya kwetu.

Naomba mapendekezo yenu wote wenye nia njema na Afrika kwa kuanza na jina lipi litumike kuiwakilisha dini/imani yetu ingawa naona kabisa madhebu yetu yanaweza kuegemea koo au makabila yenye mila na desturi zilizosawa na vitabu vyetu pia vinaweza kuwa hivyohivyo i.e. kitabu cha Wasukuma, kitabu cha Wachanga, n.k

Naomba kuwasilisha.
Dini zote kubwa zilizokubaliwa Dunia nzima ni kutoka middle East and Asia, yaani Ibrahim Ibrahimic RELIGIOUS BELIEFS, CHRISTIANITY, ISLAMIC AND JEWISM/JUDAISM
Kwahiyo Siyo wazungu walioanzisha Kama mnavyodhani, Lakini huu ni wakati ambao WATU WANAMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI, siyo Dini inayo m DEFINE mtu kuwa mwenye dhambi au la,
Tubu DHAMBI uokoke ungalipo hai [emoji91][emoji91]
 
East africa tu kuungana tumeshindwa ndo tutaweza ungana na kuwa na imani na dini moja?
Iweje tuwe na Imani moja wazaramo na wanyakyusa,kwa mzaramo unaweza kuoa na kuishi na mkeo, kwa Baba mkwe, Lakini kwa wanyakyusa ni mwiko,
 
Nature ya wanaadamu ni usaliti

Kwani Mussa hakusalitiwa?
Yesu je?
Muhammad nae?

Hao wote walisalitiwa na wakaibuka washindi sishangai kinjekitile kusalitiwa

Ikiwa yeye alitumwa na Mungu kweli alipaswa kutoboa hata kama alisalitiwa

Halafu fikra za kuona kila kitu unaonewa ni mbaya kabisa

Kila kitu unalaumu watu wewe huoni tulikosea wapi? Umefanya jitihada kwako binafsi kurekebisha?

Is your life in order? Unaabudi hiyo Miungu unayohubiri hapa?

Kama huiabudu unawezaje kukosoa wengine

Anza kuishi idea yako wewe kwanza na sisi tushawishi kwa mfano hai sio story

Yesu hakupiga story aliishi ukristo kweli

Muhammad alianza peke yake na wengine tukamfuata

Kwahiyo na wewe anza ww kwanza na kama hujasoma🤣 jua umekwisha!!!
Kwani Yesu aliposalitiwa alishinda? Si aliuawa msalabani au mimi ndo sijui? Hata Mwanamalundi alisalitiwa ila kifo chake pia kiliacha alama kubwa juu ya hatma yake
 
Basi kwa ufupi Uislamu ni Uarabu na Ukristu ni uzungu. Sasa wewe Mwafrika unadandia tu imani za watu.
 
Kwani Yesu aliposalitiwa alishinda? Si aliuawa msalabani au mimi ndo sijui? Hata Mwanamalundi alisalitiwa ila kifo chake pia kiliacha alama kubwa juu ya hatma yake
Hiyo story ina mapokeo tofauti mfano Waislam hawaamini kuwa alikufa msalabani

Na Wakristo wenyewe wanaamini kuwa alinyanyuliwa kwenda mbinguni either way alitoboa

Nambie kuhusu hatma ya kinjekitile
 
Hiyo story ina mapokeo tofauti mfano Waislam hawaamini kuwa alikufa msalabani

Na Wakristo wenyewe wanaamini kuwa alinyanyuliwa kwenda mbinguni either way alitoboa

Nambie kuhusu hatma ya kinjekitile
Akina Stefano waliuawa na ikaisha. Sijasema Mwanamalundi ndiye Yesu wetu ila nimesema fate yake ilikuwa bora pia kama ya Yesu. Alihubiri upendo na wema pia ndo maana alipendwa. Yeye alifanya mengi maisha yake yote
 
Msikikilize msomi, Profesa Rudolph Ware, aliyefanya tafiti kuhusu dini Afrika:

 
of what use? Nilidhani tuungane tutengeneze magari, ndege , baiskeli , tugundue dawa za magonjwa yanayotukabiri, etc etc za african brand/flavour, bado tu mko kwenye dini!
Ndio tungeanzia dini tuje huko
 
Back
Top Bottom