Naomba ufafanuzi wa gari aina ya Volkswagen Polo

Naomba ufafanuzi wa gari aina ya Volkswagen Polo

Polo MK4 ina engine za petrol 8 zenye ukubwa kuanzia 1200cc mpk 1800cc zinazotoa HP kati ya 55 mpk 150.

Polo MK4 ina engine za diesel 4 zenye ukubwa kuanzia 1400cc mpk 1900cc zinazotoa HP kati ya 70 mpk 130.

Mark x 1st gen. wana Engine za Petrol 3 zinazo range kuanzia 2500cc mpk 3000cc zinazotoa Hp kati ya 212 mpk 315.

Crown S180 wana Engine za Petrol 3 zenye ukubwa wa kuanzia 2500cc mpk 3500 zinazotoa hp 212 mpk 314 hp,wkt crown S170 zina engine za petrol 5 kuanzia cc 2500 mpk 3000cc zinazotoa HP Kati ya 197 mpk 280.

Sasa hapo Polo itakatizia wapi jomba?

Nasubiri facts zako boss.
Hata mabondia waliokuwa wanapiganishwa na Tysons walikuwa wanamzidi vitu vingi ikiwamo kimo, muonekano muscle pack etc ila alikuwa anawabatua fasta.....

Tusiongelee story tafuta mtu mwenye hiyo gari. Tena kama vipo upate ile Golf VW GTI..... Utajuta kubet.....
 
Cruise auto spare ni wauzaji wa spear party za magari
Jeep,
BMW,
Audi,
Land rover,
Porsche,
Volkswagen,
Chrysler,
Range/Land rover

Duka linapatikana MAKAO MAPYA,EDEN ROAD jirani na cafe laziz restaurant,Arusha

Kwa mawasiliano piga +255743805465,+255786050747
Email:cruisespares@gmail.com
Fb&IG:cruiseautospareparts

Pia usisite kuwasiliana nasi pia tunatoa ushauri.
 
Wewe unaelekea hii gari haujawai itumia au hata kuishuhudia barabarani. Gari za Volkswagen zinasifa ya kupumua na kuchapa mwendo plus handling nzuri.

Hii ni mojawapo. Mimi huwa navutiwa na ile Golf GTI. Nilishaiendesha. Kuelekea Arusha nikitokea Dar.... Aiseee hizi gari ni ndogo ila zimetengenezwa kuvimbiana misuli na gari kubwa.

Zinachapa mwendo balaa. Kama ile ya Golf nadhani modeli yake ya sasa itakuwa inacheza kwenye 320 top speed if not mistaken. Ila bei sasa baba. Bei ndio shida. Bei yake umeshanunua harrier na chenji ya mafuta ya mwezi mzima full tank itabakia.
Yani kama una crown au mark x usifuatane na Golf utapata hasira zile gari nikitu kingine
 
Wewe naona unahadithiwa na kukariri tu vitu.

Yeye ameongelea polo wewe unaongelea Golf GTI.,hakuna sehemu nimeongelea GTI hapa.GTI inakimbia kwny category ya gari za dizaini hio,nilishaweka hapa JF video ya GTI ikiiacha Crown iliyokua kwny 180km/h na nikamuuliza mdau mmoja humu mwenye GTI RRONDO namna hio GTI ilivyoiacha hio Crown akasema GTI inatembea lkn ilivyoiacha hio Crown sio kawaida,itakua hio GTI imefanyiwa remapping/tuned,hopefully unajua maana ya hicho nilichokisema hapo.

Khs bei,bei zake ni za kawaida tu acha kutisha watu.Nilishataka kuinunua GTI 2006 model(2.0 TFSI GTI manual) ambayo ndio common kwa hapa bongo,be forward walikua wanaiuza $3000,haya nenda kaangalie kodi ya GTI kule TRA uone kama ni pesa nyingi kiasi hicho.

GTI edition 30 2006 model ndio ilikua juu ya hapo kwny $5200.Niliacha nikanunua mazda rx -8 moded.

Ukisema Golf R bei zake hazishikiki hapo ni sawa kabisa.So hizo habari za kuambiwa eti bei ya kununua GTI unanunua harrier na chenchi inabaki ni story za kuhadithiwa tu.

Khs hii hoja yako ya 'Kama ile ya Golf nadhani modeli yake ya sasa itakuwa inacheza kwenye 320 top speed if not mistaken'

Hata model za miaka ya zamani huko za 'Golf GTI mk5' speedometer inasoma 300km/h,lkn haiwezi kuifikia hio top speed kamwe.

GTI top speed yake haiwezi kuzidi hata 250km/h,kuzidi hapo ni mpk ifanyiwe tuning na makorokoro kibao tena iwe heavy moded lkn ikiwa stock ni never ever. Inshort hakuna uwezekano wa gari yenye 200hp ikafikia top speed ya 320km/h.

Hii nilifanya testing mwenyewe kwa kutumia gti stock kwny rally Oldonyosambu,Arusha na nikajionea mwenyewe,hizo 320km/h ni marketing strategy na pia kwa watengenezaji wa magari ni gharama sana kwao kuweka kila model ya gari na speedometer ya tofauti wkt speedometer hio hio inaweza kuwekwa na kwny model nyingine.

Golf inakimbia lkn usi-exaggerate.

Sula la bei inadepend na Production ya mwaka gani.

Mfano, Golf GTi ya mwaka 2010 bei imechangamka.

Golf GTi ya mwaka 2015 na kuendelea, bei zake ni motooo, hazishikiki.

-Kaveli-
 
Ni kazuri sana na kako stabble sana road, tatizo ukikataka kukauza ndio shida inapoanzia hapo

Na kwa appearance, binafsi naonaga Polo ina muonekano mzuri kuliko golf... hasa sura ya mbele na mkato wa nyuma.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom