Boss! Kua connected kwenye biashara ndio kila kitu, naeza sema hii ndio prime factor. Wenzetu wazungu wanapenda kusema "Your network is your net worth."
Na sisi ambao hatukubahatika kuwa na surnames za kiheshimiwa kutengeneza network ni ngumu sana. Yani leo hii wewe na riz1 wote mkipewa mil 10 mfanye biashara, ndani ya mwaka m1 jamaa keshakuacha mbali sana. Maana hata akisema anasupply pipi za ivory kwenye taasis za serikali anaeza hata kuuza pakti elf 20, wewe huku kitaa pakti unauza ef 3.
Ukianza biashara hautaelewa kila kitu in an eye blink. Ni pole pole, kadri unavyozidi kua kwenye game ndio unavyoelewa how it's done na ndivyo unavyozidi kukutana na watu wengi, hawa watu ndio connections zenyewe. Niseme kwa ufupi, kukutana na watu sahihi ndio njia rahisi zaidi ya kutengeneza network yako.
Hata kwenye masoko pia ni hivyo hivyo.