Naomba ushauri biashara ya kusajili laini na kuuza vocha

Vocha ya 500 bei ya jumla ni 480 so faida ni 20,vocha ya buku unauziwa kwa 960 faida ni 40.golini kwangu naziuza kama stail tu ya kuvuta wateja na kusaidia kuuza vitu vingine.
Na wanunuzi wengi hununua kupitia cm.
 
Vocha ya 500 bei ya jumla ni 480 so faida ni 20,vocha ya buku unauziwa kwa 960 faida ni 40.golini kwangu naziuza kama stail tu ya kuvuta wateja na kusaidia kuuza vitu vingine.
Uko maeneo gani uku kwetu za 500 jumla ni 475, faida 25, buku ni 950, faida 50, 5000 ni 4750 faida 250, na ya 10000 faida 500. Ila uliwa ktk mzunguko wa watu wengi vituoni au kariakoo ivi uwe na uhakika wa kuuza za kama laki moja kwa siku faida utaiona mkuu
 
Kibamba mkuu, vocha ata uwe location ya namna gan ni pasua kichwa.
 
Kumbe kuna bei tofauti tofauti [emoji848][emoji848], nashukuru kwa kufunguka kwenu kunanipa mwanga... Mi nipo chuo kikuu kimoja hapa Dar.. Baada ya chakula, wanachuo tunakula vocha kama hatuna akili nzuri [emoji1787][emoji1787]
 
Mtaji mdogo unataka kuuza vocha?

Kama unataka kuongeza kama bidhaa mpya kwenye biashara iliokwisha aanzishwa sawa lakin Kama ndio unataka kutokea hapo hutoki!
mi mwanafunzi wa chuo, hivyo naona biashara ya vocha haitavurugana sana na kitabu.. Naelewa faida sio kubwa kunitoa kimaisha ila nataka nisikae tu kama 'wa kusoma' [emoji1787][emoji1787]
 
Sawa, utaratibu wa kuuza za kurusha upoje?
Kama unaline za uwakala hiyo huduma ipo kwa tigo piga *148*08# ni TIGORUSHA Na hii unauza mda wa maongezi na vifurushi

Pia kwenye airtel ukiingia kwenye menu ya Airtel money utaikuta

Kwa tigo Kama huna line za uwakala nenda tigo shop watakuunganisha ni bule kabisa
 
Nashukuru kwa ufafanuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…