Naomba ushauri: Hati ya kiwanja ni ya mke wangu pekee au naweza kubadilisha majina?

Ndio mnaweza kabisa.

Kwanza hicho mlichonacho au alichonacho sio HATI bali ni mkataba/makubaliano tu. Nimesema sio hati kupitia hapo uliposema mashahidi, naamini itakuwa ni hivyo.

Sasa chakufanya hapo ni mtaandika makubaliano ya umiliki wa pamoja, sababu umesema mmechanga pamoja hiyo hela.

Sasa hapo tafuta wakili anayejua anachotakiwa kufanya ila wewe chakumwambia ni kuwa mnahitaji awaandikie makubaliano ya kumiliki pamoja, urampa stori yenu kisha yeye atajua namna ya kuyaweka vizuri yaeleweke kisheria.

Kisha hayo makubaliano yatasomwa pamoja na huo mkataba wa mkeo kununua hicho kiwanja.

Muhimu hakikisha mnaweka sahihi.zenu pamoja na dole gumba, ili kuepusha habari za sio mimi nili saini.

Kama upo Arusha tuwasiliane nikusaidie kuyaweka sawa Mkuu.
 
Kiwanja kina hati (title deed)? Au mkataba tu wa mauziano?

P.s kwa vyovyote mkeo ana nia ovu. Yes mnaweza kubadili isomeke majina yenu wote wawili bila tatizo. Isikua yeye (wife) akubali maana hicho kiwanja ni Mali yake 💯
Naona mgogoro unaanzia hapa "isipokua yeye (wife) akubali maana hicho kiwanja ni Mali yake 💯"...
 
Nipo Dar
 
Fuata huu ushauri. Wakili nipo hapa kama kiwanja kipo dar es salaam/ pwani. At reasonable fee.
 
Hiyo ni hati au karatasi ya Serikali za Mtaa?
 
Wewe ni mwanasheria mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…