Naomba ushauri juu ya mgogoro huu wa ardhi

Naomba ushauri juu ya mgogoro huu wa ardhi

Ah_laam

New Member
Joined
Mar 4, 2025
Posts
1
Reaction score
0
Habari za wakati huu,
Hapo eneo moja lililopo Dodoma mjini kuna Mama aliuziwa kiwanja miaka ya tisini huko kama sio mwanzoni mwa elfu mbili hivi.

Sasa akajenga kijumba kidogo cha kuanzia maisha kisha mambo mengine yatafuata mbele, na hapo mtaani eneo karibu lote wameuziwa viwanja/ mashamba na mzee huyo huyo na maeneo mengine mzee huyo aliwapa wanawe na wajukuu wamejenga hapo hapo yeye ameshafariki.

Sasa baada ya kuanza kufuatilia huko CDA akakuta kiwanja chake kina jina la mtu mwengine na huyo mtu hawakuwahi kumuona inaonekana ni wale watu wafanyakazi (wa sehemu husika waliokuwa wakijikatia maeneo), basi baada ya miaka zaidi ya 10 kupita akaja mtu akasema kuwa kiwanja hiko ni cha mzee wake ameshafariki na aliuziwa na serikali na hati wanayo. Kwa hiyo wamekuja na CDA wamepima na wanataka kujenga na hao CDA wamewaambia wahusika hata ukae sehemu miaka mia mwenye eneo akija huwezi kumzuia asijenge naombeni kujua hawa wazee wa eneo hili wafanye nini? Maana hata wao hawaelewi na wameambia mhusika anataka aje kujenga
Ni huruma sana🥲
 
Mkuu,Ni huruma sana kwa kweli.Kwanza hio hati ilitolewa kwa njia gani Wizara ya Ardhi wakiwamo humu wanaweza lichukua na kutafuta namna ya kulifanyia kazi.
 
Back
Top Bottom