Naomba ushauri kuhusu huyu bodaboda

Naomba ushauri kuhusu huyu bodaboda

Kuna kazi ya kumsimamia bodaboda nilipewa. Makubaliano ilikua alete 280k kila mwezi baada ya miezi 10 pikipiki itakua ya kwake, sasa uletaji wa hesabu umekua ukisua sua ana malimbikizo ya almost miezi mitatu, nataka kumwambia arudishe pikipiki tuvunje mkataba ila pesa ambayo bado hajaleta ni nyingi sana almost laki 8 kwaiyo siwezi kuipotezea hela yote.

Naweza kuchukua pikipiki na nikamdai kiasi kilichobaki? Na nikishaichukua pikipiki nitamshurutisha vipi alipe angalao hata nusu ya pesa anayodaiwa?

Naombeni ushauri wenu

Minaona umchezeshee kama za mandonga zile
 
Nipo iringa, nimeona bora nichukue pikipiki ipaki tu amekuja na mke wake ambae ndio alikua shaidi wake kipindi tunasaini nikamwambia anipe funguo tunavunja mkataba, kwa mara ya kwanza maisha yangu mtu mzima kabisa pamoja na mkewe wamenipigia magoti mpaka wanatoa machozi kuniomba niwavulie., nimeumia kinoma lakini sina jinsi nimekataa ombi lao nimechukua chombo
daah noma sana bosss
 
Kuna kazi ya kumsimamia bodaboda nilipewa. Makubaliano ilikua alete 280k kila mwezi baada ya miezi 10 pikipiki itakua ya kwake, sasa uletaji wa hesabu umekua ukisua sua ana malimbikizo ya almost miezi mitatu, nataka kumwambia arudishe pikipiki tuvunje mkataba ila pesa ambayo bado hajaleta ni nyingi sana almost laki 8 kwaiyo siwezi kuipotezea hela yote.

Naweza kuchukua pikipiki na nikamdai kiasi kilichobaki? Na nikishaichukua pikipiki nitamshurutisha vipi alipe angalao hata nusu ya pesa anayodaiwa?

Naombeni ushauri wenu
Mlipeana kirafiki au kwa mkataba?
Kama kirafiki una kazi ngumu kidogo ya kumbana, kama kwa mkataba obvious kuna kipengele cha kutokuleta hesabu ambapo mdhamini wake anawajibika, ikiwa ni pamoja na kulipa au kumbana mhusika alipe.

Angalizo:
Kipindi hiki hakikisha unaifuatilia sana unaweza letewa taarifa kuwa ameporwa pikipiki kumbe ameshacheza deal. Ikiwezekana ifunge fasta GPS, itakusaidia!!!
 
Mlipeana kirafiki au kwa mkataba?
Kama kirafiki una kazi ngumu kidogo ya kumbana, kama kwa mkataba obvious kuna kipengele cha kutokuleta hesabu ambapo mdhamini wake anawajibika, ikiwa ni pamoja na kulipa au kumbana mhusika alipe.

Angalizo:
Kipindi hiki hakikisha unaifuatilia sana unaweza letewa taarifa kuwa ameporwa pikipiki kumbe ameshacheza deal. Ikiwezekana ifunge fasta GPRS, itakusaidia!!!
Sio GPRS ni GPS.
 
Sio yangu mkuu nimepewa niisimamie tu maana mwenyewe yupo mbali, kuirudisha bila angalao hata nusu ya hesabu anayodaiwa sasa mwenye mali atanielewa kweli
Unashauriwa vizuri unakomaa na mawazo yako, haya acha deni liendelee kuwa kubwa siku pikipiki ikiharibika utachukua scrapper tuu maana hakuna hela ya kutengeneza na yeye atanunua ya kwake.
 
Mkataba upo ninao ndani waliandikishiana na mwenye pikipiki mimi nilisaini kama shahidi ila mwenye pikipiki alipata safari kikazi na atakaa muda mrefu uko akaniacha hapa kwake na pia akaniambia niwe nawafatilia bodaboda wake wapo wawili kuna mwingine angalao ana afazali mara moja moja analeta hesabu pungufu tunaandikishiana baada ya siku kadhaa anamaliza deni anaendelea ila huyu mwingine ninaemwongelea hapa ndo msumbufu kweli kweli, leo nimeamua kuchukua pikipiki na nimetaarifu nitaangalia nafikiria njia gani nitumie kumshurutisha aleta pesa anayodaiwa kwaiyo alete pesa kwa hiyari yake kabla hatujafikishana pabaya.. nataka niende polisi badae kuomba mwongozo hatua gani za kuchukua ili huyu jamaa alipe pesa anayodaiwa
 
Sio yangu mkuu nimepewa niisimamie tu maana mwenyewe yupo mbali, kuirudisha bila angalao hata nusu ya hesabu anayodaiwa sasa mwenye mali atanielewa kweli
Akilipa hela yote unayomdai ina maana kwamba mkataba wenu uko ON kwa hiyo hutakuwa na sifa ya kumnyang'anya hiyo pikipiki.

Unatakiwa kumnyang'anya hiyo pikipiki ikiwa bado unamdai kama kielelezo cha yeye kuvunja makubaliano yenu.

Usisubiri sana. Chukua chombo mapema.
 
Unashauriwa vizuri unakomaa na mawazo yako, haya acha deni liendelee kuwa kubwa siku pikipiki ikiharibika utachukua scrapper tuu maana hakuna hela ya kutengeneza na yeye atanunua ya kwake.
Mkuu nishafanya kama nilivyoshauriwa uko juu sometimes jambo linaweza kuonekana rahisi kama halijakukuta wewe, kama hujawahi ku-deal na hawa bodaboda ni rahisi sana kutoa lawama
 
Akilipa hela yote unayomdai ina maana kwamba mkataba wenu uko ON kwa hiyo hutakuwa na sifa ya kumnyang'anya hiyo pikipiki.

Unatakiwa kumnyang'anya hiyo pikipiki ikiwa bado unamdai kama kielelezo cha yeye kuvunja makubaliano yenu.

Usisubiri sana. Chukua chombo mapema.
Nimeichukua pikipiki akilipa tunaendela tuliposhia
 
Atakuelewa ama na za miezi mingine ulikua hujampatia?
Pesa yote ya hesabu niliyopewa ipo hata siku moja siwezi kugusa pesa ambayo sio yangu, hapa iringa kwenyewe mimi ni mgeni kidogo bado hata sina makazi rasmi kwa kipindi chote ambacho jamaa hayupo kaniacha hapa kwake sasa kwa wema kama huo tu nitaanzaje hata kugusa tu pesa ambayo sio yangu.. nimeamua kuchukua pikipiki akija namwelezea kila kitu kwa sababu dereva mwenyewe kaanza usumbufu tangu yeye akiwepo basi atanielewa
 
Msamehe,kwenye biashara si kupata faida tu,kuna kulata na hasara.

Vunja mkataba chukua pikipiki
 
Sababu zipi zilizompelekea akashindwa kuleta marejesho
Huyu jamaa ni fundi ujenzi sasa kipindi mkataba ushaanza alipata kazi ya ujenzi kujenga zahanati ni mbali kidogo na hapa iringa mjini akanitaarifu ataenda na pikipiki alafu wakilipwa malipo yao atakaporudi atamaliza kiasi chote ambacho kitakua anadaiwa nikathibitisha kweli kapewa iyo kazi niliona mikataba pamoja na kuuliza watu wake wa karibu sasa baada ya miezi miwili ndo akarudi nikamfata kwake akaniambia bado hawajalipwa nikaenda kumfatilia ila sasa unaenda mwezi wa tatu sababu yake kubwa ni kwamba bado hawajalipwa pesa ya ujenzi, nikamwambia pesa inatakiwa itoke kwenye pikipiki mambo ya malipo ya ujenzi mimi hayanihusu nikaenda mpaka kuongea na mke wake sasa zimebaki takribani siku nne malimbikizo ya deni yafike kiasi cha miezi mitatu (kuna miezi hapo kati alikua analeta ila pungufu kwaiyo hesabu ya deni inaongezeka).. nimeona nivunje tu
 
Ungempa principles zako kwanza kuwa silei deni hata liwe dogo...

Kwahiyo alipe kwanza ndio mkataba uendelee... La sivyo mkataba uishe immediately.
Sio deni lote la kwangu kuna deni jingine nimerithi kwa mwenye mali aliniachia nimfatilie bodaboda akiwa bado kiasi fulani cha pesa hajaleta kwa makubaliano akilipwa hela yake ya ujenzi anamalizia yote hayo mwenye mali anajua
 
Huyu jamaa ni fundi ujenzi sasa kipindi mkataba ushaanza alipata kazi ya ujenzi kujenga zahanati ni mbali kidogo na hapa iringa mjini akanitaarifu ataenda na pikipiki alafu wakilipwa malipo yao atakaporudi atamaliza kiasi chote ambacho kitakua anadaiwa nikathibitisha kweli kapewa iyo kazi niliona mikataba pamoja na kuuliza watu wake wa karibu sasa baada ya miezi miwili ndo akarudi nikamfata kwake akaniambia bado hawajalipwa nikaenda kumfatilia ila sasa unaenda mwezi wa tatu sababu yake kubwa ni kwamba bado hawajalipwa pesa ya ujenzi, nikamwambia pesa inatakiwa itoke kwenye pikipiki mambo ya malipo ya ujenzi mimi hayanihusu nikaenda mpaka kuongea na mke wake sasa zimebaki takribani siku nne malimbikizo ya deni yafike kiasi cha miezi mitatu (kuna miezi hapo kati alikua analeta ila pungufu kwaiyo hesabu ya deni inaongezeka).. nimeona nivunje tu
Huo ujenzi haukuwa unakuhusu toka mwanzo...

Pikipiki haikuwa ya kwenda nayo kazini... Ilikuwa ya biashara...

Ungemwambia toka mwanzo achague ujenzi au mkataba wa pikipiki?
 
Back
Top Bottom