Naomba ushauri kuhusu huyu bodaboda

Naomba ushauri kuhusu huyu bodaboda

Ungempa principles zako kwanza kuwa silei deni hata liwe dogo...

Kwahiyo alipe kwanza ndio mkataba uendelee... La sivyo mkataba uishe immediately.
Ni kweli mkuu lakini maisha yetu jobless huku mtaani ni tofauti kidogo na wenye vipato vya uhakika.. kwa mimi hapa sina shughuli rasmi wala makazi maalumu, nategemea zaidi wasamalia wema tu sasa imetokea mtu kuniachia nikae kwake kwa miezi yote ambayo hatokwepo na kusimamia miradi yake ikiwemo izo pikipiki sio rahisi kukumbuka hayo mambo ya kuwekeana masharti
 
Huyu jamaa ni fundi ujenzi sasa kipindi mkataba ushaanza alipata kazi ya ujenzi kujenga zahanati ni mbali kidogo na hapa iringa mjini akanitaarifu ataenda na pikipiki alafu wakilipwa malipo yao atakaporudi atamaliza kiasi chote ambacho kitakua anadaiwa nikathibitisha kweli kapewa iyo kazi niliona mikataba pamoja na kuuliza watu wake wa karibu sasa baada ya miezi miwili ndo akarudi nikamfata kwake akaniambia bado hawajalipwa nikaenda kumfatilia ila sasa unaenda mwezi wa tatu sababu yake kubwa ni kwamba bado hawajalipwa pesa ya ujenzi, nikamwambia pesa inatakiwa itoke kwenye pikipiki mambo ya malipo ya ujenzi mimi hayanihusu nikaenda mpaka kuongea na mke wake sasa zimebaki takribani siku nne malimbikizo ya deni yafike kiasi cha miezi mitatu (kuna miezi hapo kati alikua analeta ila pungufu kwaiyo hesabu ya deni inaongezeka).. nimeona nivunje tu
Ameingiwa na tamaa; tafuta mtu mwingine, pia usiweke siku nyingi za marejesho, weka angalau kila baada ya siku 2 akuletee; mtu kukaa na hela nyingi muda mrefu zinamshawishi.

Inawezekana, anafanya hivyo ili uchukue chombo chako na yeye anunue kingine kwa mapato aliyoyapata
 
Biashara ya boda lazima wakuchangamshe uwe na akili kama zao
 
Kati ya biashara ya kichaa ni hii ya bodaboda.

Hizi biashara Bora uwe unafanya mwenyewe.

Kumpa mtu bodaboda ni upuuzi.tegemea hasara.

Kuna mmoja nae niliwahi mshauri aachane na hii biashara Bora hata afungue genge akakaza fuvu akachezea za uso hadi anajuta.
 
Ameingiwa na tamaa; tafuta mtu mwingine, pia usiweke siku nyingi za marejesho, weka angalau kila baada ya siku 2 akuletee; mtu kukaa na hela nyingi muda mrefu zinamshawishi.

Inawezekana, anafanya hivyo ili uchukue chombo chako na yeye anunue kingine kwa mapato aliyoyapata
Sawa mkuu, tayari nishavunja mkataba nimechukua pikipiki nimeipaki tu ndani, pikipiki sio yangu niliachiwa tu kusimamia na suala la kukaa muda mrefu hata mimi wakati naachiwa uangalizi nilimwambia mwenye pikipiki hii haipo sawa mkataba inabidi uwe wa muda mfupi kama bodaboda akiwa mbabaishaji ijulikane mapema ila nikagundua ndo utaratibu wa huku mkoani na huyu mwenye pikipiki kanipa hifadhi kwake pamoja na kusimamia miradi yake zikiwemo izo pikipiki( zipo mbili ila huyu mwingine ni mstaarabu kidogo kwaiyo tunaenda sawa) kwa kipindi chote ambacho hatakwepo maana amesafiri kikazi hatokwepo kwa takribani miezi mitano au sita, sasa ingawa nilijua huu mkataba utaleta shida lakini ilikua ngumu kukataa maana mtaani hali sio shwari kupewa hifadhi ya bure kwa karibu nusu mwaka ni fadhira kubwa sana sio rahisi kumpa mtu izo principles za mkataba
 
Huo ujenzi haukuwa unakuhusu toka mwanzo...

Pikipiki haikuwa ya kwenda nayo kazini... Ilikuwa ya biashara...

Ungemwambia toka mwanzo achague ujenzi au mkataba wa pikipiki?
Ni kweli mkuu hatujui yajayo maisha ni kama kufanya predictions tu sometimes ndo ivyo predictions zinakataa
 
Kati ya biashara ya kichaa ni hii ya bodaboda.

Hizi biashara Bora uwe unafanya mwenyewe.

Kumpa mtu bodaboda ni upuuzi.tegemea hasara.

Kuna mmoja nae niliwahi mshauri aachane na hii biashara Bora hata afungue genge akakaza fuvu akachezea za uso hadi anajuta.
Ni kweli mkuu ila huku mkoani ni too much nilishawahi kuachiwa pikipiki niisimamie nikiwa dar yule boda tulikua tunaenda vzr tu mpaka nikawa nikisikia malalamiko ya watu kuhusu bodaboda nikawa nashangaa tatizo nini, yule bodaboda alikua mchaga, kwa kweli linapokuja suala la biashara wachaga wapewe sifa yao ya kipekee
 
Kwanini muandikishiane kwa Mwezi?Hapo Ndio tatizo likeanzia.,Walau ingekuwa wa week
 
Yaani wewe huna tofauti na Mandonga, ishakula kwako, bora uchukue kwa sasa. Wengine mifumo cku hizi ni kwa wiki akisogeza wiki ya pili unanyanganya. Cha kukusaidia kamata picpick weka ndani, kamata chochote chake chenye dhaman hiyo kamatia akileta hiyo 800K unampa kwa masharti mengine mapya
 
Kwanini muandikishiane kwa Mwezi?Hapo Ndio tatizo likeanzia.,Walau ingekuwa wa week
Sio ya kwangu nimeachiwa nisimamie mkataba ukiwa tayari ushasainiwa na pia huku mikoani utaratibu wa hesabu kwa mwezi ndo unaotumika hata mimi pia mara ya kwanza nausoma mkataba nilishangaa
 
Boda boda kama huendeshi mwenyewe basi jiandae kwa lolote
 
Sasa kama una mkataba si mpeleke kwenye vyombo vya sheria... Halafu mtu hakupi rejesho zaidi ya ×2 unamuangalia tu hadi inafika laki8. Chukua pikipik weka ndani sio muda atakuambia ameibiwa pikpik. Muandikie barua ya kuvunja mkataba kwasabab moja mbili tatu... Siku nyingine mkataba weka wa kila wiki, kwa mwezi hawawez wengi wanatamaa wanakula pesa
 
kwani kabla ya kumpa mkataba ulishindwa nn kumloga awe ndondocha wako kila mwezi alete pesa unajua nyie mnafanya mambo yawe magumu hawa wafanya kazi wetu bila kuwaloga hawaendi ungempa mganga laki mbili akamfunga akili saa hzi si ungekua huna stress kila mwezi mtu analeta hesabu bila hata kujua kaletaje
 
Kwa akili zako fyatu za kumsubiri bodaboda akulipe malimbikizo miezi mitatu yote trust me, hufai hata kusimamia ugawaji wa soda kwenye msiba uko kijijini
 
HILI KOSA LILIANZIA SIKU YA KWANZA... KURUHUSU DENI LA MWEZI MMOJA... HUTAKIWI KURUHUSU DENI HATA LA SIKU MOJA... HAPO HAPO UNAVUNJA MKATABA... LAKINI UKILIMBIKIZA... BAADAE UNAUMIA WEWE...
Kawaida asipoleta pesa ndani ya siku 10 ndio mkataba unavunjwa bhana au 15 na hapo hamdaiani

sasa huyu jamaa anaomba ushauri wakat angerejea kusoma mkataba unasemaje
 
Back
Top Bottom