Naomba ushauri kuhusu mwanangu

DALALI MKUU

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2022
Posts
2,011
Reaction score
4,705
Bila shaka Wote Mpo salama.

Naomba ushauri wenu, Mwanangu kwa sasa ana miaka mitatu na nusu ila nimeamua nisimpeleke shule hizi za kawaida kusoma Darasa la kwanza Hadi la Saba na kuendelea.

Nimeona ikiwezekana nimpeleke akasomee ufundi moja kwa moja Kwa vitu ambavyo ataweza kuvifanya hata akiwa na umri mdogo.

Mfano naweza kumpeleka chuo cha Urembo, au Music, ama Video and productions au mapishi ama Utangazaji.

Nyie wakuu Mna lipi la kumshauri Je inawezekana? Nini faida na hasara zake.

NB: anajua kusoma na kuandika.
 
Mpe basic knowledge ya number hapo nyumbani (ajiri mwalimu maalum, English language like lengo kuu)akifikisha 5yrs to 6yrs mpeleke akasomee programming and coding, fanya hivyo na utakuja kunipa high five.
 
Point nzuri sana
 
Hivi kumbe mjinga anapata supporters? Ni maajabu
 
Elimu ya msingi ni muhimu sana, atajifunza kuandika, kusoma, kuhesabu, kufanya hesabu muhimu, n.k.

mpeleke shule ila kwenye likizo unamuongezea ujuzi
 
Mpe basic knowledge ya number hapo nyumbani (ajiri mwalimu maalum, English language like lengo kuu)akifikisha 5yrs to 6yrs mpeleke akasomee programming and coding, fanya hivyo na utakuja kunipa high five.
Watakubali kumpokea kwenye vyuo vyetu au nimtafutie mwalimu pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…