Naomba ushauri kuhusu ofa ya mshahara

Naomba ushauri kuhusu ofa ya mshahara

Naona kazi unayofanya kwa sasa is more of partnership than boss na mwajiriwa. Pia kazi ya sasa una opportunity ya kukua na kuwa na business yako mwenyewe kuliko kwa mhindi. Hivyo baki huko huko kwa mhindi usiende hata wakupe offer ya 700k mkuu.
 
Wakuu hope mmeamka salama.

Nina jambo kidogo nahitaji ushauri ndugu zangu, Mimi ni kijana wa kiume ni mkaz wa Dar es salaam ila kwa sasa nipo mkoa wa pwani kibaha nimejiriwa na mtu binafsi tunalipana kwa % yeye anachuka 40% mimi nachukua 60% na pia kaniamini kwa kiasi kikubwa sana na kabla sijapata room huku kibaha kwa siku za mwanzo nilikuwa naishi kwake mpaka nilivyopata pesa ya kutosha ndio nikapanga room mpaka sasa tunafanya kazi pamoja na upendo.

Pale malipo kwa mwezi huwa inarange laki 7, laki 6 au laki 5 inategemea na mzunguko wa wateja kifupi kukunja 40k kwa siku ni jambo la kawaida.

Sasa tukiachana na hilo pia kuna kampuni X ya wahindi ipo masaki kuna mtu aliwapa info zangu wakanichek lengo ni kufanya kazi nao basi nikaenda ofisini kwao tukazungumza wakanifanyia interview mbili nikafaulu vzr wakasema wameridhishwa namimi so wanaomba tufanye kazi nikawambia sawa ila mjue mimi nimeajiriwa mahali so ni vema mnipe offer yenu nione kama ina maslahi wakasema aina tatzo nirudi tu home HR atanichek kwa Email yangu nikasema poa.

Kesho yake asubuhi HR akanichek anaomba nimtumie details zangu aniandikie mkataba nikawauliza why ntume taarifa zangu mniandikie mkataba wakati bado sijaskia offer yenu nikawaambi kwa navyofaham mimi hizi huwa ni process za mwisho kabisa baada ya kukubalia wakasema sawa tutakupa offer yetu.

Baadae HR akanichek akaniambia offer yao ni 400k kwa mwezi nikachomoa sasa baadae simu zikawa nyingi wahindi wanapiga simu hao wakiniomba nikubali kufanya nao kazi sababu hata kama mshahara sio mkubwa sana ila wananipa mkataba wa mwaka mmoja nikachomoa nikawambia wekeni 500k mezani wakasema ngoja wakadiscus jibu likaja kuwa sababu ndio kwanza ninaanza na utendaji wangu wa kazi awaujui so ni vema nianze tu na hiyo 400k nikakataa.

Ikapita kama siku tatu jana meneja wao wa mauzo ni mdada akanipigia tena anaomba niende kufanya nao kazi na niseme pesa nayotaka kulipwa ukiachana na hiyo 400k. Nikamwabia nitakutafuta nkitulia sasa wakuu ebu naombeni mnishauri nipange mshahara kiasi gani sababu hata hiyo 500k naiona ndogo kulingana na kazi nitakazokuwa nafanya halafu kwa huku nilipo naiingiza tu wala siangaiki sana na kazi ni chache japo ni kweli sina mkataba.

Naombeni ushauri wa mapana hapo kazi ipi ni bora zaidi hata hata kama mishahara inaweza kuwa sawa.

Na vp kwa watu mnaofanya kazi kwenye taasisi mbalimbali au serikali mtu anaelipwa 500k ukitoa makato ya serikali na Nssf sijui unaweza kubaki na bei gani? Poleni kwa maelezo marefu nipo hapa nasubiri maoni yenu.
Hata hiyo 500k ni kidogo sanaa.
Maisha ya huko mjini is still hard than Kibaha.



Wahindi ni watu wa kukaa nao mbali mkuu nakushauri maana naona bado wewe ni mdogo ,
Utaishi kwa tabu sanaa bora wabongo wenzetu.
 
Sibagui sio sibaguwi.....ulisomea ujinga??

Hubagui kabila wala rangi ila dini unabagua tena unabagua kwelikweli.

Wahindi ni wanyanyasaji wa wafanyakazi wao, hawafai.
Mimi ni Muislam.

hayo ya ubaguzi unayajuwa wewe. Uislam haujanifundisha ubaguzi hata chembe.

Ukiitwa kondoo na ndiyo mnavyojiita wenyewe ni ubaguzi au ndiyo sifa yenu hiyo?

Kondoo waheda.

Najivunia Uislam wangu.
 
Uko wapi ungesogea hapa nikutandike kofi la utambuzi kwanza kabla ya kukushauri. Umeajiriwa Kibaha na unataka uache kazi yenye uhuru uende kufanya kazi Masaki kwa Muhindi kisa laki tano.

Umbali wa Masaki na Kibaha gharama yake kwa mwezi utaiweza? Kuunganisha magari.

Utaweza afford gharama za kufanya kazi Masaki zenye tofauti kubwa sana na Kibaha?

Pressure ya kazi kwa Wahindi utaiweza, utawahi kazini, utaweza kuondoka umechelewa zile overtime, utaiweza foleni ya kutoka Masaki mida ya kazi wanyonge wote mnagombea daladala kuondoka?

Kuna mtu kakuroga unachukulia kazi yako kienyeji na mazoea. Ukiiacha hiyo bila kazi nyingine yenye mazingira mazuri zaidi unaweza poromoka kimaisha ukapiga zako miaka hata 15 hujawahi pata nafasi kama hiyo.
 
Back
Top Bottom