Naomba ushauri kuhusu ofa ya mshahara

Naomba ushauri kuhusu ofa ya mshahara

Mi nimemuelewa jamaaa, kinachomvuta kwa mhindi ni mkataba.
Ni bora kutokuwa na mkataba kuliko kuwa na mkataba usio na masilahi unao kuumiza.
Ukienda kufanya kazi masaki kwanza jua gharama za maisha zinapanda tofauti na Kibaha.
Baki kwenye kazi yako, endelea kutunza uaminifu na Mungu atakufanikisha.
NB Tunza uaminifu
 
Muhind mwenyewe mwizi tu we bibi kizee vp?
Kwani alikulazimisha ukafanye kazi kwake, njaa zako na ujinga wako unakufanya usizione fursa mpaka aje Muhindi azione akutume na wewe.

Unalalamika nini? Hakuna sheria za kazi Tanzania?
 
Kwani alikulazimisha ukafanye kazi kwake, njaa zako na ujinga wako unakufanya usizione fursa mpaka aje Muhindi azione akutume na wewe.

Unalalamika nini? Hakuna sheria za kazi Tanzania?
We bibi nitake radhi mimi sifanyi kazi kwa muhindi. Mbn unawatetea hoa makanjibai au ndio vile tena.
 
MKuu achana na huyo muhindi kabisa, kama unafanya kazi ambayo unaweza kupata japo 40,000 kwa siku ni bora ukabakia hapo hata kama hakuna mkataba wowote.

mkataba hautakusaidia kitu labda kama ingekuwa ni ajira permanent kama ya serikali, ila hizo za mwakamwaka hakuna issue, bakia zako kibaha na masaki pasikuchanganye
 
Kosa lao wezi, wanyonyaji na wakandamizaji kwa wa Tz wenzetu tumeshashuhudia sana.
Hizo ni fikra zako tu, walikuibia nini?

hao waliokandamizwa hazijuwi mahakama?

Sema wahindi wamewazidi ujanja. Akianza hata kidika cha kuuza kachori, mara anakuwa bilionea. Hawalewi, hawachezi ngoma, utawapata wapi wewe?

Ukimuona mhindi masikini kama wewe ujuwe mlevi kama wewehuyo. Birds of the feather.
 
Hizo ni fikra zako tu, walikuibia nini?

hao waliokandamizwa hazijuwi mahakama?

Sema wahindi wamewazidi ujanja. Akianza hata kidika cha kuuza kachori, mara anakuwa bilionea. Hawalewi, hawachezi ngoma, utawapata wapi wewe?

Ukimuona mhindi masikini kama wewe ujuwe mlevi kama wewehuyo. Birds of the feather.
We bibi mdwanzi sana unawatetea kisa wewe yaya wao.
 
Nafuatilia comment kwa umakini Sana nikiwa hapa na wahindi muda huu😅😂🤣
Nikiwa na chochote Cha kuongezea ntakuja kuufunga huu mjadala

Wadau mnaweza kuendelea kutiririka hapa vijana wapate madini.

Nasubiria comment ya Kalaga Baho Nongwa
Wahindi hata wakimuwekea 900k mezani asijichanganye itamtokea puani hiyo
 
halafu kwa huku nilipo naiingiza tu wala siangaiki sana na kazi ni chache japo ni kweli sina mkataba
Fanya hukuhuku achana nao hao wakitaka double the payment km huku unakunja 700k waambie wakulipe mara 2 wakichomoa achana nao endelea na huku huku wasikuchukulie cheap kiasi hicho km wanaweza si wafanye wenyewe
 
Wakuu hope mmeamka salama.

Nina jambo kidogo nahitaji ushauri ndugu zangu, Mimi ni kijana wa kiume ni mkaz wa Dar es salaam ila kwa sasa nipo mkoa wa pwani kibaha nimejiriwa na mtu binafsi tunalipana kwa % yeye anachuka 40% mimi nachukua 60% na pia kaniamini kwa kiasi kikubwa sana na kabla sijapata room huku kibaha kwa siku za mwanzo nilikuwa naishi kwake mpaka nilivyopata pesa ya kutosha ndio nikapanga room mpaka sasa tunafanya kazi pamoja na upendo.

Pale malipo kwa mwezi huwa inarange laki 7, laki 6 au laki 5 inategemea na mzunguko wa wateja kifupi kukunja 40k kwa siku ni jambo la kawaida.

Sasa tukiachana na hilo pia kuna kampuni X ya wahindi ipo masaki kuna mtu aliwapa info zangu wakanichek lengo ni kufanya kazi nao basi nikaenda ofisini kwao tukazungumza wakanifanyia interview mbili nikafaulu vzr wakasema wameridhishwa namimi so wanaomba tufanye kazi nikawambia sawa ila mjue mimi nimeajiriwa mahali so ni vema mnipe offer yenu nione kama ina maslahi wakasema aina tatzo nirudi tu home HR atanichek kwa Email yangu nikasema poa.

Kesho yake asubuhi HR akanichek anaomba nimtumie details zangu aniandikie mkataba nikawauliza why ntume taarifa zangu mniandikie mkataba wakati bado sijaskia offer yenu nikawaambi kwa navyofaham mimi hizi huwa ni process za mwisho kabisa baada ya kukubalia wakasema sawa tutakupa offer yetu.

Baadae HR akanichek akaniambia offer yao ni 400k kwa mwezi nikachomoa sasa baadae simu zikawa nyingi wahindi wanapiga simu hao wakiniomba nikubali kufanya nao kazi sababu hata kama mshahara sio mkubwa sana ila wananipa mkataba wa mwaka mmoja nikachomoa nikawambia wekeni 500k mezani wakasema ngoja wakadiscus jibu likaja kuwa sababu ndio kwanza ninaanza na utendaji wangu wa kazi awaujui so ni vema nianze tu na hiyo 400k nikakataa.

Ikapita kama siku tatu jana meneja wao wa mauzo ni mdada akanipigia tena anaomba niende kufanya nao kazi na niseme pesa nayotaka kulipwa ukiachana na hiyo 400k. Nikamwabia nitakutafuta nkitulia sasa wakuu ebu naombeni mnishauri nipange mshahara kiasi gani sababu hata hiyo 500k naiona ndogo kulingana na kazi nitakazokuwa nafanya halafu kwa huku nilipo naiingiza tu wala siangaiki sana na kazi ni chache japo ni kweli sina mkataba.

Naombeni ushauri wa mapana hapo kazi ipi ni bora zaidi hata hata kama mishahara inaweza kuwa sawa.

Na vp kwa watu mnaofanya kazi kwenye taasisi mbalimbali au serikali mtu anaelipwa 500k ukitoa makato ya serikali na Nssf sijui unaweza kubaki na bei gani? Poleni kwa maelezo marefu nipo hapa nasubiri maoni yenu.
Kuchamba kwingi mpaka utajipaka kimbaz, wahindi unawajua kweli?? Nipe hilo shavu mimi hapo ulipo,uende huko kwa wahindi wako.
 
Achana na wahind mamaang Mkubwa tangu ujana wake aliajiriwa Kwa Hao wahind na makubaliano mazuri ya mshahara na posho atapoamua kumpumzika ikiwa imebaki kma mwak aache kazi alikuwa mtu mzima umri ushaenda wakaanza mtafutia visa mwisho wakamnyima stahiki zake akapewa pesa kidogo sana
Tulia hapo ulipokuwa usije kujuta
 
Back
Top Bottom