Ni tatizo humpata mtoto akiwa ktk process za kuzaliwa,wangu niliambiwa mama yake alicheleweshwa sana akanywa yale maji machafu ya uzazi matokeo:homa za mara kwa mara,kuchelewa kuongea hata mpaka sasa hajaweza kuongea vizuri,slow learning ni mgumu mno kuelewa anajua kusoma na kuandika vizuri ila kwa kukariri (haelewi maana ya alichokiandika)
Kisababishi kingine ni mtoto chini ya miaka mitatu kupigwa na degedege kali mara kwa mara,vyote hivi vilimpata mwanangu ila namshukuru sana Mungu nilifanikiwa kumuwahisha hospital pale MNH kitengo cha wataalamu wa ubongo wakampa matibabu yaliyozuia ubongo kuzidi kuathirika (shukrani za kipekee kwa Dr Edward Kija Mungu akubariki sana huko ulipo) mwaka wa tisa huu najaribu kuizoea hali yake maana inaniumiza sana akili kila nikiwaza hatma ya dunia yake siku nikiwa sipo.
Mleta mada pole sana,at least unajitambua shukuru kwa hilo mengine utayazoea tu waza juu ya yule asiyejitambua kabisa uone namna ulivyobarikiwa.