Ulichosema ni sahihi kabisa. Niliuliza kama unajua baadhi ya sehemu wazotoa hizo program Kwa autistic kids Kwa dar.Kuna wengine wanajua na wamezitaja na sio kwamba wanafanya wizara ya afya.mimi nahîtaji for short term tu mtoto akiwa likizo Dar kwani mtoto ameshakua enrolled kwenye special school.Nafahamu hiyo process yote na ni long term mpaka mtoto akiwa 19 yo.
Ngoja nirudie niliyosoma ushauri uliopatikana humu; kumpeleka mtoto Kaizora na sijui mwalimu gani mwingine kuna mdau kasema amebobea (I am not dismissing their quality claims ya hizo taasisi au mtu, nonetheless it’s risky as results are not guaranteed).
Kama mchangiaji mwingine alivyoeleza experience yake ya miaka 5 mitano ya therapy kwa mwaka gharama karibu 5 million, hakuna dalili zozote za improvement kwa mtoto.
Ndio maana nikaeleza swala la intervention kwenye autism ni la multi-disciplinary (interproffesional) team work. Kwanini ni muhimu kufanya mambo kwa utaratibu huo hiyo inaondoa overlapping of treatment, variation of professional opinion kwenye methodology na kuna kuwa na clear road map and progress monitoring ya mtoto kwa pamoja kwa wataalamu.
Sasa kama shule inatumia mbinu A kwenye speech therapy, unampeleka kwengine wanatumia mbinu B. Uoni huyo mtoto atakuwa confused akamate lipi, remember autism treatment is only based on shaping the thinking through consistent style learning.
Pili mtoto mwenye autism sio kwamba aelewi kabisa ni kwamba ana process mambo tofauti. Na yeye pia anakuwa frustrated kwanini umuelewi anapo communicate na wewe au uelewi action/tabia zake (ndio maana wengi hasira/frustration zao zipo karibu sana).
Ikiendelea muda mrefu bila ya kuelewena kuna chances kubwa za mtoto ku-develop mental issues kama anxiety (hapo sasa ndio anaanza kujitenga, self esteem inapungua) na hali hiyo inaweza pelekea serious forms of mental health conditions kama depression huko mbele.
Hizo ndio sababu unahitaji consistent approaches kwenye methods of intervention sio kila siku mtaalamu mwingine aje na mbinu zake. Na ndio maana hata wataalamu tofauti wanaomfanyia mtoto diagnosis nchi zilizoendelea lazima waafiki kwa pamoja mkakati sahihi wa kumsaidia (.methodology) ambayo inapelekwa shule husika waalimu kutumia na mzazi kupewa elimu on how best to interact with the child from the same agreed treatment plan.
Ni hivi hayo mambo ni ya kisera zaidi na government investment ya hizo shule. Kwa sasa sidhani hata kama hizo shule wataalamu wake wamethibitishwa na wizara ya afya au methods zao ni tested. Vinginevyo shule ingekueleza mzazi jinsi ya kuishi na mwanao na namna ya kuzungumza nae kama sehemu yake ya continuous learning anapokuwa likizo.
Jamani msituone wajinga kule kwenye majukwaa ya fujo tunapolilia Dorothy Gwajima arudishwe afya, kuna kazi kubwa bado ni rahisi kumpelekea malalamiko ya aina hii akaona hayo mapungufu na pengine kuyafanyia kazi. Kuliko kumlalamikia waziri ambae ni cluess kabisa.
If anything wizara ya afya na elimu ndio ilitakiwa kuwa source ya info ya huduma zilizopo kila eneo, zinazotolewa na certified professional. Haya sio mambo ya kuokota taarifa kwenye social media.