Naomba ushauri kuhusu usonji

Naomba ushauri kuhusu usonji

Bongo hakuna vipimo? Sasa Hawa watu wote wenye autism walijulikana vipi?
Autism ipo kwenye spectrum

Kuna ya kwenye higher end ndo hio unakua kama kichaa halafu kuna ya lower end ni kama unakosa social skills

Sasa MsLisa autism yake sio severe, nataka aseme kajuaje?

Mimi sometimes nahisi nipo autistic lakini sina njia ya uhakika ya kujua
 
Autism ipo kwenye spectrum

Kuna ya kwenye higher end ndo hio unakua kama kichaa halafu kuna ya lower end ni kama unakosa social skills

Sasa MsLisa autism yake sio severe, nataka aseme kajuaje?

Mimi sometimes nahisi nipo autistic lakini sina njia ya uhakika ya kujua
kuna kipindi nilikuwa nje ya tanzania nikafanyiwa informal assessment.
 
Mimi ni mwanamke, 30 yrs mwenye usonji. Jamii/familia yangu wanaona sina tatizo sababu shuleni nilikuwa nafaulu vizuri.

Ninapitia changamoto nyingi mnoo. Kuna wakati nahisi kukata tamaa. Anayeweza kunisaidia mawazo /counselling ntashukuru.
MsLisa counselling bila kujua chanzo cha huo usonji haisaidii kitu. Ukitaka kweli usaidikike lazima mshauri ajue source of your situation to enable him/her counselling you. Ni juu yako sasa kuwekwa chanzo vya usonji wako hapa au PM kama unaona hapa aifai.
 
Kwa anyejua sehemu za speech therapy, na occupation therapy Kwa watoto wenye autism jijini Dar es Salaam,naomba contacts zao please.Hata certified private speech therapist nahîtaji contact zake.Asante!
Zipo nyingi tu na nyingi ni za madaktari wenyewe wa Muhimbili au Regency. Ila malipo yake sio ya kitoto. Kwa mwaka zungumzia kuanzia M5 na kuendelea. Na hapo sio kwamba mtoto atapona ila atasaidika kujifunza kujihudumia katika mambo ya msingi mfano kwenda toilet, kutambua wazazi/Ndugu na kutambua na kuobey commands muhimu muhimu za nyumbani mfano kuamkia, kufua, kuosha vyombo, kuoga n.k
 
Okay, Maelezo mazuri, je una sehemu zozote ambazo unajua kuna qualified teachers au special schools for autistic kids in Dar es Salaam?
Sasa mimi nitajuaje shule zilipo wakati sifanyi kazi wizara ya elimu au afya.

Ila mtu mmoja kufundisha watoto wenye autism ni hadithi. Kwanini?

Elimu ya autistic children inatolewa through ‘evidence based intervention’, na hiyo knowledge ya ku-structure jinsi ya kumfundisha kila mtoto walimu wa shule wanaipata kutoka kwa wataalamu walio mfanyia assessment ie. depending on the identified symptoms na medics aliokutana nao.

Speech therapists atapendekeza namna bora kumfundisha kuelewa maneno, phsychologist atapendekeza namna ya ku-modify behaviour challenges alizonazo, mzazi nae atashirikishwa kwenye plan kwa sababu yeye ndio yupo nae muda mrefu hasa kwenye ku-modify behaviours.

Ni hivi it takes a lot of interprofessional involvement kufundisha autistic children and a long time mtoto kuanza kuelewa pattern; autism aina dawa (ni milele) mtu anajifunza kuishi nayo tu.

Sasa kwa elimu ya elfu 25 kwa saa hadi huyo mtoto akae sawa hiyo shule fees zake FEZA nafuu.

Cousin wangu ana mtoto mwenye moderate autistic, sasa hivi ni 20 something years anaishi mwenyewe. Lakini hadi kumfundisha hizo tabia ilikuwa kama miaka 5 ya special schools zao wanaenda kila siku kama wanafunzi wa kawaida kuanzia nursery, primary and secondary (O’level), kuanzia A level na University ndio wanaingia kwenye elimu ya wote.

Mdogo wangu nae ana mtoto autistic yake ni mild kikubwa kwake ni emotions anasoma shule za kawaida, ila ana attend ‘behaviour modification therapies’ (wote hao, wapo nje ya nchi unfortunately, kwa hivyo sio shule za bongo).

Lakini kusema mtoto ambae ana moderate form ya autism, mwenye speech difficulties and learning difficulties atafundishwa na mtu mmoja hiyo ni hadithi ya Ali Nacha.

Shida ni inaanzia wizara ya afya hakuna elimu jamii kuhusu autism.
 
Autism ipo kwenye spectrum

Kuna ya kwenye higher end ndo hio unakua kama kichaa halafu kuna ya lower end ni kama unakosa social skills

Sasa MsLisa autism yake sio severe, nataka aseme kajuaje?

Mimi sometimes nahisi nipo autistic lakini sina njia ya uhakika ya kujua
unaenda tu hosp wanakupims brain nadhani mkuu
 
unaenda tu hosp wanakupims brain nadhani mkuu
Si kweli diagnosis ya autism ni displayed symptoms tu za sufferers; hakuna brain scan.

Common condition za autism ni ‘mild na moderate’, hizo ndio watu wanaweza ishi normal life with treatment.

Severe autism inakuja na ‘profound and multiple learning disability’ (PMLD), wengi awawezi ishi wenyewe maisha yao yote wanahitaji kuangaliwa.

PMLD kibongo bongo ndio tunasema ni ndondocha, be it political incorrect.
 
Si kweli diagnosis ya autism ni displayed symptoms tu za sufferers; hakuna brain scan.

Common condition mild na moderate.

Severe autism inakuja ‘profound and multiple learning disability’ (PMLD), wengi awawezi ishi wenyewe maisha yao yote wanahitaji kuangaliwa.
ohooo.kumbe...
 
Ulichosema ni sahihi kabisa. Niliuliza kama unajua baadhi ya sehemu wazotoa hizo program Kwa autistic kids Kwa dar.Kuna wengine wanajua na wamezitaja na sio kwamba wanafanya wizara ya afya.mimi nahîtaji for short term tu mtoto akiwa likizo Dar kwani mtoto ameshakua enrolled kwenye special school.Nafahamu hiyo process yote na ni long term mpaka mtoto akiwa 19 yo.
Ngoja nirudie niliyosoma ushauri uliopatikana humu; kumpeleka mtoto Kaizora na sijui mwalimu gani mwingine kuna mdau kasema amebobea (I am not dismissing their quality claims ya hizo taasisi au mtu, nonetheless it’s risky as results are not guaranteed).

Kama mchangiaji mwingine alivyoeleza experience yake ya miaka 5 mitano ya therapy kwa mwaka gharama karibu 5 million, hakuna dalili zozote za improvement kwa mtoto.

Ndio maana nikaeleza swala la intervention kwenye autism ni la multi-disciplinary (interproffesional) team work. Kwanini ni muhimu kufanya mambo kwa utaratibu huo hiyo inaondoa overlapping of treatment, variation of professional opinion kwenye methodology na kuna kuwa na clear road map and progress monitoring ya mtoto kwa pamoja kwa wataalamu.

Sasa kama shule inatumia mbinu A kwenye speech therapy, unampeleka kwengine wanatumia mbinu B. Uoni huyo mtoto atakuwa confused akamate lipi, remember autism treatment is only based on shaping the thinking through consistent style learning.

Pili mtoto mwenye autism sio kwamba aelewi kabisa ni kwamba ana process mambo tofauti. Na yeye pia anakuwa frustrated kwanini umuelewi anapo communicate na wewe au uelewi action/tabia zake (ndio maana wengi hasira/frustration zao zipo karibu sana).

Ikiendelea muda mrefu bila ya kuelewena kuna chances kubwa za mtoto ku-develop mental issues kama anxiety (hapo sasa ndio anaanza kujitenga, self esteem inapungua) na hali hiyo inaweza pelekea serious forms of mental health conditions kama depression huko mbele.

Hizo ndio sababu unahitaji consistent approaches kwenye methods of intervention sio kila siku mtaalamu mwingine aje na mbinu zake. Na ndio maana hata wataalamu tofauti wanaomfanyia mtoto diagnosis nchi zilizoendelea lazima waafiki kwa pamoja mkakati sahihi wa kumsaidia (.methodology) ambayo inapelekwa shule husika waalimu kutumia na mzazi kupewa elimu on how best to interact with the child from the same agreed treatment plan.

Ni hivi hayo mambo ni ya kisera zaidi na government investment ya hizo shule. Kwa sasa sidhani hata kama hizo shule wataalamu wake wamethibitishwa na wizara ya afya au methods zao ni tested. Vinginevyo shule ingekueleza mzazi jinsi ya kuishi na mwanao na namna ya kuzungumza nae kama sehemu yake ya continuous learning anapokuwa likizo.

Jamani msituone wajinga kule kwenye majukwaa ya fujo tunapolilia Dorothy Gwajima arudishwe afya, kuna kazi kubwa bado ni rahisi kumpelekea malalamiko ya aina hii akaona hayo mapungufu na pengine kuyafanyia kazi. Kuliko kumlalamikia waziri ambae ni cluess kabisa.

If anything wizara ya afya na elimu ndio ilitakiwa kuwa source ya info ya huduma zilizopo kila eneo, zinazotolewa na certified professional. Haya sio mambo ya kuokota taarifa kwenye social media.
 
Okay, Maelezo mazuri, je una sehemu zozote ambazo unajua kuna qualified teachers au special schools for autistic kids in Dar es Salaam?
Kwa Dar zipo shule kuna moja ipo somewhere Mbezi Beach (hii ni private) hapa nilienda but unfortunately hawafundishi kwa Kiswahili (therapists walinishauri kwa sababu mtoto hajui kuongea anatakiwa hata masomo apewe kupitia lugha mama yake Kiswahili).

So nimempeleka government Kibamba Shule ya Msingi wana kitengo chao maalumu,unaanzia kwanza pale Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko kwa wataalamu kumthibitisha pia kushauri namna mtoto anavyopaswa kufundishwa.

Ukihitaji # ya mkuu wa hicho kitengo Kibamba utasema nikupe uone namna ya kumsaidia mtoto.
 
  • Thanks
Reactions: Mit
Ni tatizo humpata mtoto akiwa ktk process za kuzaliwa,wangu niliambiwa mama yake alicheleweshwa sana akanywa yale maji machafu ya uzazi matokeo:homa za mara kwa mara,kuchelewa kuongea hata mpaka sasa hajaweza kuongea vizuri,slow learning ni mgumu mno kuelewa anajua kusoma na kuandika vizuri ila kwa kukariri (haelewi maana ya alichokiandika)

Kisababishi kingine ni mtoto chini ya miaka mitatu kupigwa na degedege kali mara kwa mara,vyote hivi vilimpata mwanangu ila namshukuru sana Mungu nilifanikiwa kumuwahisha hospital pale MNH kitengo cha wataalamu wa ubongo wakampa matibabu yaliyozuia ubongo kuzidi kuathirika (shukrani za kipekee kwa Dr Edward Kija Mungu akubariki sana huko ulipo) mwaka wa tisa huu najaribu kuizoea hali yake maana inaniumiza sana akili kila nikiwaza hatma ya dunia yake siku nikiwa sipo.

Mleta mada pole sana,at least unajitambua shukuru kwa hilo mengine utayazoea tu waza juu ya yule asiyejitambua kabisa uone namna ulivyobarikiwa.
Isee pole sana mkuu. mbaya zaidi tuko nchi ya kiwehu kama tanzania unakosa kabisa kuona future ya mtoto. walau nchi za wenzetu unakua na uhakika ataishi vema hata siku ukiwa haupo duniani. ni huzun kwa kweli kuishi huku shimoni afirika
 
mkuu umewezaje kuandika kwa ufasaha hivi?
nina binti yangu ana USONJI.
ana miaka 6 kuongea hawezi wala kuandika.
[emoji24][emoji24][emoji24] Kuna ndugu yangu mwanaye ana miaka miwili sasa,anapewa matumaini tu Hooo mwanao akifikisha miaka mitatu au minne ataongea,wako ana miaka sita na haongei,Madaktari wanasemaje Mkuu?
 
[emoji24][emoji24][emoji24] Kuna ndugu yangu mwanaye ana miaka miwili sasa,anapewa matumaini tu Hooo mwanao akifikisha miaka mitatu au minne ataongea,wako ana miaka sita na haongei,Madaktari wanasemaje Mkuu?
Uyo mtoto mwenye miaka miwili anapenda kucheza mchezo gani!? Anapenda kuzunguka? Ukiwa unamuongeleshwa anakuangalia usoni? Ukimuita jina lake anageuka au anakuja kwa wakati? Anapenda kuchezea taili za toi au kuona taili ikizunguka? Ukimkataza kucheza kufanya kitu anarudia tena kitu ulichomkataza? Anatembea bira kukanyaga na visigino!? Akihitaji kitu anakushika mkono umchukulie au ulishe ataki kula kwa mikono yake? Na haogopi kucheza sehem ya hayatı!? Anachagua vyakula? Anasumbuliwa na Choo kigumu conspation ? Ukimuweka Acheze na wenzake anafwatishwa mchezo wanaocheza na wenzake au anacheza mchezo wake peke yake!? Anachezesha mikono yake au vidole vyake? Some times anacheka pekeyake! Au apumziki muda wote anatembea tembea, kupata usingiz yy shida!? Muda mwingine anaweza kısılmama akakimbia ghafla!? Kutumua pot kujisaidia kwake ni tabu? Apendi maziwa ya ngo’ombe? Anapaya areg ya vipele vidogo vidogo! So kuna vitu vingi unaanza kuvigundua kwa mtoto wenye autism/ usonji akifika miaka mi 3 utagundua anadalili nyingi za autism!
 
Back
Top Bottom