Naomba ushauri kutokana na changamoto ninazopitia ofisini ninapofanyia kazi

Unauza duka la vifaa gani...!
 
Hiyo ni kazi ya kijungujiko msome bosi wako umuepuke site zake
 
Mwaka flan nilienda kampun flan kufanya kaz..namna nilivyopata kaz walitangaza nafasi nikaomba nikaitwa kwenye usaili..wakat usaili ukiendelea nikiwa nimeshatumia kama dk 45 hiv mkurugenzi mkuu (mzungu) akanikubali na na nikaajiliwa..kumbe ile nafasi kuna mbongo mkuu wa idara alitaka ndugu yake ndo achukue ile nafasi..
Nilipoanza kaz nikaona sipat ushirikiano na watu wa idara yangu..chini chini kulawa na maneno "msimpe ushirikiano ili afail..".dogo mmoja wa IT tukiqa tunakunywa chai ndo akanimegea mkanda mzima...kwa kuwa na mimi nilikiwa mkuu wa idaranikatumia nafasi yangu kutaka taarifa mbali mbali...
Baadae nikabaini mambo meengi ya upigaji..nikamuita jamaa kistaarabu nikaamuliza akafoka na kugoma..halafu usiku kama saa saba akaingia whatsup kwenye grp la staff wote..akaoandika vitu vingi kama kunikosoa utendaji wangu..alivyopost nikasoma weee...kisha nikaingia kwenye email yangu nikavuta file lake la upigaji na hasara yoote aliyosababisha...nikapost pale...
Md na staff wengine wakalisoma..uchunguz ukaanza akasimamishwa kaz na kufunguliwa mashtaka na hatimae akafungwa..mwakana anamaliza kifungo...
 
Kabla ya kukushauli ningependa kufahamu hiyo kazi yako salary ngapi wanakupatia kwa mwezi
Na je hiyo salary inavuka 500,000

Je hiyo kazi ina overtime na malupu lupu unapata kupitia kazi unayofanya ambayo ndani ya mwezi inakupatia mia 4

Je kuna allowance zozote kama vile chakula , usafili , kodiii.......

Kama hivi vyote hamna piga chini hiyo kazi kama malupukupu yapo komaaa kuwa ngangari piga kaziii


Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Una uhakika kuwa wewe siyo tatizo? Kwanini unaamini wao ndiyo tatizo na siyo wewe?
 
Ushauri mmbovu huo
 
Hiyo Ofisi ni ya Serikali au Binafsi?
 
Uliagizwa ukadeki choo nn au nn
 
Nadhani hii ndiyo inaweza kuwa sababu.
 
mmm..pole sana, hiyo kazi ni ya serikali au ya kibinafsi?
 
Pole sana mkuu,hayo yapo sana maofisini,iliwahi kunikuta hiyo hali karibu miezi 9,nikaiweka hali ninayopitia mikononi mwa Mungu,ilikuwa ni kama picha flani hivi,wawili wakastaafu,wawili wengine wakahamishwa ofisi,la mwisho nikapandishwa cheo na kuhamia ofisi nyingine,waliobakia wakabaki wanatoa macho...
 
Mboka Manyema,
Wiki2 tu tayari wamekwisha kukujua ulivyo na wanakutendea hayo? Wiki2 tu tayari Ofisi imeanza kukutisha? kuna kitu katika utendeji wako wa kazi au tabia zako au namna ulivyoingia hapo ofisini kinapaswa kufanyiwa tatahmini lasivyo napata ugumu wa namna ya kuendelea kukushauri. umeingiaje hapo Ofisini, kuna mwenzio alifukuzwa ili uingie wewe?
 
Umeajiriwa na mkataba maalumu au umepewa kazi tu bila mkataba wowote?
Kama una mkataba fanya kazi zako bila uwoga ila kama hauna mkataba anza kujipendekezaa kwa mkuu wako wa idara, jjua nafasi yako kazini, mipaka yako, na majukumu yako.

Kama umeajiriwaa na mkataba anza kusoma mkataba wako vizuri na sheria ya kazi ujue vipi unapambana nawo kama watakufukuza bila kufata utaratibu. Alafu jiamini unapoongea na boss au mfanyakkazi mwezio kama kitu hujakipenda weka sura ya kumaanisha kile unachoongea siyo unaweka suraa ya kuonesha huruma ili uhurumiwe mwangalie machoni boss wako anapoongea itakusaidia mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…