Naomba ushauri kutokana na changamoto ninazopitia ofisini ninapofanyia kazi

Tuachage kudanganya kwenye CV zetu. Ndio yale mambo ya kuandika kwenye CV kuwa unajua French unaajiriwa anakuja mfaransa unaanza kuongea mistari ya Awilo Longomba.

[emoji3][emoji3]

Ndugu Ngurukia sawa bwana
Kwenye CV unaandika ujuzi wa kutumia Microsoft excel kwa ufasaha,haya tucholee pie chart ya takwimu hizi.
 
Chunguza hao jamaa wa hapo ofsini kwako sio kabila Moja kweli? Kama ndivyo tengemea hiyo trending.....!
Ushauri:
1.jiamini na timiza wajibu wako.
2.kua mbunifu kwenye kazi zako .
3.fanya kazi kwa bidii.
4.usijionyeshe wewe ni mnyonge sana na mtu wa kupelekwa pelekwa.
5. Badilisha muonekano wako, sio Kila siku unaenda kazini umechoka choka, nguo hubadilishi, unarudia nguo mara 3(kama ndivyo ulivyo lkn)
6.kitakachokufanya uheshimike sehemu unayodhalailika ni mchango wako unao utoa. (Jichunguze sana hapa)

KAZA KIJANA HAKUNA TONGE LINALOPATIKANA KIURAHISI.
 
Private au Serikalini?

Utakua umejimix ukajifanya much-know.

Ukiwa mgeni jifanye fala, hadi usome mchezo ndio unaota mapembe.
 
Akitoka itakuwa kama kwenye movie vile anakuja kukuteka😂😂😂😂
 
Ubaya ubaya tu mkuu hukukosea kbsa
 
2024 makaburi ya Kinondoni yanapata member mpya.
 
Hii imekaa kiunyama mwingi sana. Inaitwa kumkoma nyani.😂😂😂 Ukamzima kabisa mpaka behind the bars?!
 
Kesho ingia kazini na Panga kiunoni,uweke na sura ya kazi,

Usikubali binadamu mwenzako akudharau au akudhalilishe hata kama umefanya kosa,kila binadamu anastahili kuheshimiwa,na anapokosea anastahili kurekebishwa kwa njia ya kiubinadamu.
 
1. Muulize supervisor unakosea wapi urekebishe mwende nae sawa.

2. Jitume na ujiongeze kwa kuonesha moyo wa kutaka kujifunza na kuuliza usichojua, ikishindikana mueleze kiongozi wako changamoto unayopitia ajaribu kuongea na workmates wako ili waweze kushirikiana naww. Saa ingine umekaa hujitumi unategemea wao ndio wajipendekeze kwako kukuelekeza au unajiona special ndio maana wanakupuuzia, hapa tatizo linaweza kuwa kwako nahisi.

3. Anakufokea sababu kuna maneno anapewa kuhusu utetandaji wako mbovu wa kazi ivyo hawezi kukuchekea, unatakiwa uangalie unapokosea urekebishe.

4. Jifunze kazi upige kazi, acha kujitenga na kujiona unajua huu ni muda wa kujishusha kwa wazoefu na kujipendekeza ujue kazi, ukijishusha hakuna atakaekusema vibaya na akitokea wapo watakaokutetea.

NB: Usijionee huruma kwa kuangalia unavyosemwa, jiangalie Pia wewe unafeli wapi unaweza ukawa unalaumu watu kumbe wewe ndio tatizo. Otherwise kila kazi itakushinda.
 
Utendaji kazi wako ni mbovu ukiona hivyo.

Jitahidi kazi zako ziwe zimenyooka alafu uone kama kuna kima atasogea
 
Kwa mujibu wa maelezo yako watalaamu wa mambo wamebaini una shida ya Communication Skills na personal development improve kwenye hayo maeneo utaenjoy kazi yako. kwaheri
 
kwa kaliba ya huyo jamaa akitoka jela hiyo vita haitaisha labda uhame nchi.. huna usalama hata kidogo utaishi kama digidigi. revenge is real
 
Nijuavyo sehemu ya kazi ukiwa mgeni ukaleta mbwembwe Hutoboi. Jifanye mjinga jifunze kazi ishi nao kama hawakusumbui vile ila wasalimie wajulie hali jenga urafiki umeenda kufanya kazi hujaenda kupendwa wala kudekezwa hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…