Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Issue ni kwamba hata mkiolewa wanne, sio guarantee kwamba ndiyo mpo wanne tu, mume kamaliza tamaa zake. Issue hapa ni mwanaume kuchagua kuridhika na mke wake. Afu muolewe wake wanne, kwa nguvu zipi za kiume na uchumi upi kama sio kukaribisha umaskini? Multiple relationships=multiple confusions
 
Wangekuelewa wasingekulaumu

Jicontrol
 
Mzee... vipi yule binti wa form 4? Bado unaendelea kula tunda kimasikhara ama imekuaje?

Ni upweke wa MCHEPUKO umekupelekea uhamie kwa dent ama kuna kingine?

Kama gharama unaina zinakuzidia inakuaje unaenda kimpangia makazi? Bado hujajifunza tuu na drammar yote hii?
Na stress.zote hizi kweli mzee wangu?
Unajua maradhi yapo? Huogipi? Na endapo ukarudi kwa mke.. plz pima afya yako.
Kwanini usiache huu uzinzi kwa huo umri? At ur age kwa mama yangu ni bibi ana mjukuu
Sijajua kama unao ama lah. Nadhan ni muda muafaka wa wewe kutulia na familia yako. Hao watoto achana nao. Usije kufia kifuani .

Hii tabia ya kuwa na kila aina ya mwanamke malipo yake makubwa sana. Pata picha kila mchepuko ukuloge, na mke nae ukute anakuloga.. si utakua kichaa? Nakushauri tulia...
 
Mi naomba niulize hivi bi mkubwa huwa unamuachaje unapokuwa unashinda huko nyumba ndogo mbona kama unaishi kwa bi mdogo sana
Mbona kama mkeo anajua tayari kwa jinsi wanawake tulivyo kweli asiwe amehisi chochote

Mimi nimeuliza, yaani kwa wanawake walivyo wiki mbili nyingi.
 
It seems unamatatizo makubwa kuliko huyu mleta mada. Otherwise usingemuattack namna hii. Pole na utafute wataalam wakusaidie kabla haijawa mbaya zaidi.
Tena kamuattack tofauti na mleta mada alivyoandika
 
[emoji3][emoji16][emoji16][emoji16][emoji3]imebdi nicheeeke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Utaingizwa kwenye kundi letu acha nilale mie
 
Hakuna jinsi hiyo nyumba huyo mwanamke ana sehemu yake. Na inaonekana hana sehemu ya kuishi hapa mjini. Kama alivyoshauri mtu hapo juu, kata viwanja uza, ila Mimi nitaongeza kidogo, kaa chini uzungumze nae. Mfanye tathmini ya thamani ya nyumba Kisha mgawane nusu kwa nusu. Mlipe nusu yake kisheria au kwa mkataba utakaomfunga kutokusumbua wewe ubaki na nyumba. Kumbuka kwamba hiyo nyumba pia warithi wake ni wanao ambao tayari wameegamia kwa mama yao . Usijali wajengee future yao na usiwategemee kwamba watakusaidia! Wameshalishwa sumu na mama yao ambaye anafanya mocking ya makusudi ili uonekane unamnyanyasa au kumtesa mama yao.

Cha msingi ni kuachana naye, ameshaharibu maisha na mtazamo wa watoto juu yako lakini atafanya Kila jitihada aharibu taswira yako. kwa ndugu,jirani na rafiki zako.

Yupo kwenye mapenzi mapya na huyo jamaa na hisia zinamuendesha na sio akili. Hatojali kwa sababu hana cha kupoteza. Piga chini kistaarabu acha ahangaike na Dunia.
 
Umemfukunyua wapi tena, sasa kwa stress hizi asipopata wa kumpetpet pengine asingelikuwapo, tuwe wa kweli hakuna mtu asiyependa kupetiwa basi tu ikitokea ukakosa unavumilia bila chuki lakini🤭 Ila kama binti ni underage sasa hapo hatari
 
Mi naona baba yangu ujisalimishe kwa mke mkubwa tu maana unakoelekea siko kuzuri mamdogo hana mpango na wewe ila mali zako, pole lakini kwanini unamng'ang'ania hivyo licha ya matukio aliyokufanyia?

Mshirikishe hata Yule rafiki wako anaweza kukuelewa akushauri nini ufanye

Hii inataka iwe Stockholm syndrome
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…