Binamu nakusalimu katika Jina la BWANA.
Uislam ni mzuri kuhusu issue ya wake wanne; kwa wanaume ambao hawajaamua kuridhika; na kwa wanawake ambao wanaenda kuolewa mke wa 2, 3 au 4. Ila kwa mke wa kwanza, suala la wanawake wanne kwake laweza kuwa shubiri;au kwa mke wa 2 na 3 pale anapoongezewa mke mdogo na yeye ndiyo utajua sasa kama wanafurahia kuongezewa wake wenzao.
The bitter truth; mtu asipoamua kuridhika hakuna idadi ya wanawake itakayomridhisha. Kwa sababu kuoa wake wanne haimaanishi ndiyo kwamba wakifika wanne tu na tamaa ya mwanaume inakufa. Ataendelea kutamani, na since hawezi kuoa mke wa 5,6..... basi atawafanya michepuko.
Na huo uke wenza uliohalalishwa; kwa kweli hekaheka zake tunaziona humu mtaani na duniani(especially insta). Hata wanawake tumeumbwa na ubinafsi, kilicho changu sitopenda kushare na mwingine period. Majority wanaolewa wake wenza kwa sababu tu ndiyo dini inataka hivyo na hawana option; lakini hawapendi. Ila most likely kadri unavyoongeza idadi ya wanawake, ndivyo unavyoongeza stress. Mara nyingi kila mwanamke atavutia upande wake na watoto wake ili wapendelewe zaidi wao. Na unaweza kuwatreat wake wote sawa; ila huwezi kuwapenda the same kuna sehemu tu upendo utazidi. Muda sio muda mabifu yanaanza, mara kukamatana uchawi n.k.. kwa zile hekaheka za wake wa mzee Yusuph au Queen Darleen na Sabra; kwa kweli naushukuru Ukristo. Na wanawake wanapeleka chuki zao hadi kwa watoto wa mke/wake wengine; watoto wengi wa kutoka kwenye familia za mitala hawapendani kwa sababu ya sumu wanazolishwa na mama zao.
Binadamu haturidhiki kwa sababu kiuhalisia kila siku kuna matamanio mapya; ni vile inafika hatua unasema na kuamua ngoja tu niridhike. Ni sawa tu na idadi ya partners; usipoamua kuridhika utaoa na kuacha kila siku. Usipojua/jifunza kuutiisha mwili wako; hakuna idadi ya wanawake itakayokutosheleza. Na kwa familia zetu hizo za uchumi wa kuvumiliana: wanawake wengi=umasikini
Na kwa shuhuda chache tu za watu walizozileta humu kuhusu ndugu zao waliokuwa na wake wengi; unaona kabisa jinsi fainali uzeeni inavyo-apply kwa wanaume. Mpende na kumuheshimu mke wa ujana wako.