Hahaaa pole ndugu yangu, napaogopa polisi, usiombe kwenda kule,maana huyu mwanamke aliniitia polisi, ndio kwanza nimefika nyumbani saa nane, tu kila nisubili chakula sikioni kuja, nikienda jikoni naona ni maji tu tanachemka
Nadhani kudu iris mala nipo sebureni, naona vijana wa nguvu wanaingia sebureni na mke yupo yupo nyuma anawasmbia, huyo hapo, mala wananiambia ninyanyuke wao ni polisi, nawaambia tatizo nini, wanasema twende utajua huko huko,
Nilikuwa nimevaa bukta nikawaomba niingie chumbani nivae suruali, wanifuata mpaka chumbani,
Kusema kweli nikidhani jamaa ni majambazi , maana niwale wanasimamaga nyumba ya defender, tukaongozana mpaka kituoni, naomba niwanieleze kosa langu, wakagoma, mala vua mkanda, vua viatu, weka simu hapa
Haya ingia rumande huko,
Ilikuwa ni saa kumi na moja tayali, sikuona huu ni usiku au mchana, nilikesha usiku kucha mpaka asubuhi naona watu wanaketa chai, hapo hakuna ndugu yangu hata mmoja anafahamu kama nimewekwa rumande,
Sielwi ilikua ni saa ngapi nikampa Afande fulani sh 5000.
Akanipa simu yake nikampigia yule mwanamke aje anitoe maana kesho yake naingia ofisi is mapema sana,
Alinijibu neno moja tu, KAA HUKO HUKO,
Akakata simu,
Kesho yake kaja kunitoa saa tano!!!!