Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Haya yote yanatokea mke mkubwa alikuwa wapi yani hajaongelewa sana humu

Kipo kitu kimejificha hapa miaka 18 sio rahic sisi wanawake ucgundue tabia ya mume nakusiwe na ugomv wowote Yani wiki tu tayar umejua kua ana mchepuko me nafkiria hapa nyumba kubwa alijua kuhusu nyumba ndogo na mke mkubwa akagombana na mume na hapo mume akahamishia makazi nyumba ndogo
 
Yaani nimwachie nyumba kweli? Nikiwa hai naona anafaidi nyumba yangu na wanaume wengine!?

Kweli? Hapana hapo sasa mnataka ndio mniue,
Kabisa au mimi niue mtu, sipo tayari kumwachia nyumba yangu, labda kama mimi ndio ningeonyesha simtaki, ningemwachianyumba ili apunguze machungu, lakini yeye anifanyie vituko vyote hivyo halafu nimwachie nyumba, hapana,
 
We mzee mbona una vichambo hivo, huyo mke mdogo unambakisha kweli[emoji16][emoji16][emoji16]

[emoji23][emoji23], inabidi tu mzee wetu ajifariji na kuilazimisha furaha, afanyeje yashamwagika.
 
Kwa sababu story ilikuwa mwanzo sana, na story ilikuwa inahusu bi mdogo, sikutaka sana kumzungumzia yeye, nimeona hata wengine wanasema muda mwingi nilikuwa natumia kwa bi mdogo, hapana nilikuwa nabalanci sana muda wangu ili kila upande ulizike, na kuwa kazi zangu zilikuwa ni za masaa tofauti tofauti, mala usiku mala mchana, mala weekend unaenda unapumzika katikati ya wiki (shift), mala safari, mala overtim e, hayo yote yalisaidia sana kuonekana pande zote na wakawa wamezoea hiyo mienendo yangu,

Kuhusu bi mkubwa kugundua alikuja gundua baadaye sana, kwanza baada ya bi mdomo kuniwekea chupi ya mtoto kwenye bag langu, wakati nimetoka safari,
Hapo pamoja na kujitetea ndio alipoamza kuweka Q mark,

Baadaye sana sasa ikawa wazi kabisa ,
Ila alinaambia yeye hataki mtoto kwake, kama ni nyuma niwajenge e huko huko
 
Na ndoa ni ya mume na mke mmoja.
Hizo nyingine ni uzinzi na ushetani tu unaotafutiwa njia ya kuuhalalisha.

Eti maumbile!!!
Kuanza kuuhalalisha udhaifu kwa kisingizio cha maumbile ni upumbavu Sana.
 
Unaona sasa? Hukuweka mambo yote wazi. Anyways.. usiku mwema mzee wangu
 
Mtu asiyeweza kuamua kuridhika na mmoja; hata apewe mia hatoweza kuridhika pia. Hatuoi/kuolewa na malaika; ila pamoja na mapungufu yao bado tumeamua kuwachagua na kuridhika na hao hao
Na ndoa ni ya mume na mke mmoja.
Hizo nyingine ni uzinzi na ushetani tu unaotafutiwa njia ya kuuhalalisha.

Eti maumbile!!!
Kuanza kuuhalalisha udhaifu kwa kisingizio cha maumbile ni upumbavu Sana.
 
Aisee..we Baba una moyo Khaaa!!..naona aibu kukuonea huruma
 
Mtu asiyeweza kuamua kuridhika na mmoja; hata apewe mia hatoweza kuridhika pia. Hatuoi/kuolewa na malaika; ila pamoja na mapungufu yao bado tumeamua kuwachagua na kuridhika na hao hao
[emoji122][emoji817]
Sina Cha kuongeza[emoji119]

Biblia huwa naipenda sana.
Imeandika kila kitu kuhusu namna ya kuudhibiti mwili.
 
Kwahiyo kumbe bimkubwa alijua Kama ana mwenzie !?? 🙄 Aisee
 
Ahsante sana, Mwenyezi Mungu akubariki sana, ni ushauri mzuri, kwanza niliogopa sana, kumfukuza nikijua kuwa, atasema labda nimemtumia vya kutosha sasa nimemchoka narudi kwa mke,
Lakini baada ya kugundua anaendelea na mwanaume ambaye, nilishamtuhumu miaka 10 iliyopita pamoja na visa vyote hivi na kiburi, kumbe naye ana bwana yake pembeni, hapana uzalendo umenishinda, potelea mbali , kama ataniraumu basi ni mwendelezo wa akili zake ndogo kutokujua makosa, kwa kipindi chote hicho,

Lingine nililogundua kumbe hata hizo biashara ya mchele huko Morogoro walikuwa wapo pamoja,

Ila mbaya zaidi pamoja na malalamiko yangu kwa wazazi wake, lakini hawaonyeshi hata kushtuka,

Mfano halisi ni sasa hivi, mtoto wao yupo kwao lakini hata kunipigia simu, kuniulizia kulikoni hakuna! Mpaka bajiuliza hii ni familia ya aina gani,

Mpaka nawaeleza waziwazi kabisa mbona mtoto wenu anatembea na aliyewahi kuwa mkwenu ( huyo bwana alishawahi kuoa binamu ya mke mdogo) wakagombana baada ya kufumaniana,

Na jamaa akataka kumuua mgoni wake kisu,
Akatoroka kijiji kwa muda fulani.
Lakini mpaka nafikia hatua ya kuwaambia wazi wazi, kuwa mlikuwa mnanidanganya kumbe mnajua mtoto wenu ana wanaume wawili halafu mkiendelea kuniomba vimisaada, na kuwakatia simu ambapo leo ni wiki ya tatu hawanipigia tena!
 
Father achana na huyo mwanamke..achana na hiyo familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…