Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Mwitore si ajabu hata wazazi wako kuwajengea nyumba ya milion 50. Ulifanywa chanzo cha mapato na mjasilimali wa kijijini akawa wa mjini.
Kabisa, story ilivyoanza nilijua mwisho wake,
Hasemi ukweli, yeye ndiyo alimshawishi mchepuko, kuhama kule kwa shemeji, na kwenda kupanga, naamini hili.

Na hasemi ukweli, mchepuko lazima, alikuwa anampa vipigo vya mbwa koko, guilty conscience, ndiyo ilikuwa inamfanya akubali na ampe chochote! Akiamini ndiyo kummiliki till death do us apart!

Alikuwa ukweli aliuona muda mrefu, ila binadamu tunaishi in denial, maadam alikuwa na watoto na akienda anagaiwa mbunye, it wasn't a problem.
Alijua kumpa mihela ndiyo suluhisho!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Haamini, kashindwa kummeneji!

Kakolea hawezi kumuacha, hapa mchepuko anasubiria kikokotoo, hana wasiwasi anajua watagawana pasu kwa pasu, 😂

Jamaa watoto pande zote, wanajua baba yao alichowafanyia mama zao, so wana stick na mama zao, ataishi maisha ya upweke SANA asipojirudi kwa bi mkubwa na kutulia huko!

Everyday is Saturday................................😎
 

Ushauri Kama huu unalipiwa pesa.
 
Unasema, akirudi nimpokee tena? Big hapana.
Naomba nisaidie kumwomba Mungu asirudi.

Kumuuliza ulikuwa wapi nilichokaga, ameshaondokaga mala nyingi tu,
Na kurudi mpaka nikaanza kumwangalia tu,

Nilishaanza kuhisi huyu ana matatizo ya akili, sio mzima huyu

Siku moja mwezi wa nne mwaka jana,
Nikikuta msg ya mwanaume, aakakana kumfahamu, nikamwambia kesho nakuja uniambie vizuri,
Nilivyoenda kesho nikakuta kachukua baadhi ya nguo zake kaondoka

Ilikuwa kipindi kile shule zimefungwa sababu ya corona, nikwaambia watoto nikijua shule zinafunguliwa lini, mmojawapo kabla hajarudi shule, amalizie hii mizigo kumpelekea huko kwao

Nadhani watoto walimwambia kuwa baba kasema tukuletee mizigo yako kabla ya kurudi shule,

Mala tangazo la kufunguliwa shule likatoka,
Akarudi haraka sana, nilipoenda nikamkuta,

Nikashinda hapo mpaka jioni bila kumuuliza kitu,
Wakati naondoka, nilimwambia nina mazungumzo na wewe, sio vizuri niondoke bila kujua ulikuwa wapi, na Ume rudi bila kujibu lile swali langu,

Akanijibu kwa mkato tu, kuwa nilikuwa kwa Baba mdogo , moro.

Sikutaka hata kuendelea kumuuliza tena,
Nikageuka nikaanza kuondoka,
Wakati naondoka akaniambia TENA ILE HATI IRUDISHE HAPA,

Niligeuka na kumwangalia na kutikisa kichwa na kuondoka bila kumjibu kitu,

Nilipata mawazo kuwa huwa sasa hivi si mtu,
Ni kichaa tayari hana akili za kibinadamu tena,

Hata mtoto mdogo akikosea hawezi kukufanyiatena kosa muda huo huo,

Kuhusu kuangalia simu yake, ni baada ya kuona mwenendo usio wa kawaida, Ndio nikaanza kufanya uchunguzi,

Mbona bi mkubwa siangalii simu yake, unataka kuniambia yeye yupo perfect sana, kwamba hana makando kando yanaendelea huko, hapana naye ni binadamu, lakini hakuna alichowahi kunitendea kila cha kunifanya nintilie shaka
 
Miranda I, hilo halina shaka, najiamini,
Ndugu yangu nimetumia kila mbinu, asiende huko, ikiwa ni pamoja na kumfukuza ndani mwangu,amewahi kulala nje mala mbili,

Nimeshamwitia mjumbe, mpaka majirani,
Nimeshapiga,
Nimeshatoa taarifa kwa wazazi wake,

Hebu fikiria hili,
Kwa zaidi ya miaka mitano tumekuwa tukipingana kuhusu biashara ya kusafiri
Na akisafiri ndio hivyo anakaa wiki anarudi tnagombana sana,

Lakini leo unathubutu kwenda kukodi shamba ulime, na ni hukohuko Moro ambako sitaki uende?
Unafikiri hii ni akili kweli ya binadamu
Hapana huyu ni kichaa tayali
 
Huko anaaga safarini kikazi, just imagine mwanaume anakula nje mpaka mtoto anamaliza chuo huna habari.

Wanawake wengine jamani, mbona kulalia masikio hivyo.
Yaani hapo mke wa ndoa anadanganywa hadi basi.
Wanawake mama zetu mnapitia mengi sana [emoji24]


Hapo bado vurumai la watoto wa ndoa na hao wa nje.
 
Mzee wangu ashakum si matusi, naomba niseme tuu mwenye kichaa ni wewe sio huyo mchepuko.

Sababu ziko wazi kabisa. Hebu kaa chini tafakari kwa kina na utajua mwenye shida huko upstairs ni wewe na si huyo mchepuko wako.

Mzee wangu wewe ni mwanaume, hebu fanya maamuzi ya kiume.
Unforgetable
 
Huko anaaga safarini kikazi, just imagine mwanaume anakula nje mpaka mtoto anamaliza chuo huna habari.

Wanawake wengine jamani, mbona kulalia masikio hivyo.
Hapana rumande nimela siku moja, na ni siku ambayo wife, anajua huwa sirudi
Ila bahati nzuri, siku hiyo vile vile wife alikuwa amesafiri kwao siku tatu zilizopita, kwa hiyo hakuwepo Dar,

Kuhusu wife kujua kama ni watoto nje
Alishajua, hili mbona tayari nimelisemea humu

Ila kiufupi aliumia sana.
Na kukataa kabisa kuwatambua watoto, na

Alisha niambie kama ni hao watoto basi niwajengee huko huko, lakini home NO
 
Una kila kitu Kwa mke mkubwa, mkuu nyumba usiuze achia watoto baki na hati tu kwamba asiweze kuiuza. Ita wanao wakabidhi kila kitu hapo Kwa sasa ni wakubwa wanajitambua, wewe rudi Kwa mkeo wa halali maana kwa jinsi ninavyokusoma mkeo anajua kabisa una nyumba ndogo na ameshakuuliza maana hiyo mikasa katika nyumba mpya imekufanya uegemee zaidi Kwa bi mdogo. Kama hajakuuliza tambua ke tuna akili Sana ni kwamba anajua ipo siku utakuja mtamkia mwenyewe ndio maana katulia. Tena kwa taarifa yako hata watoto wako wa nyumba kubwa wanajua hilo. Mkuu Kwa mbali naona unachokisubiri hapo ni kifo tu Kwa ugonjwa au kuuawa, rudi Kwa mkeo mle pension yenu huku mkilea wajukuu insha'Allah hapo mtakapojaaliwa kuwapata. Achana naye tafadhali usitafute mengine jinsi ulivyomchoka yeye kakichoka zaidi, ke Wana tabia ya kukinai na kusahau ukimwacha tu haipiti muda atakukumbuka usirudi baki na mkeo tu, block namba zake iwe ndio mwisho.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]wenzako tumeambiwa tunafurahia matatizo ya wanaume tuna stress[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mi mwanaume akiwa na mambo ya michepuko wacha avurugwe mpaka basi ye si mwanaume kaamua basi sawa
Basi Mimi nimeyafurahia kweli yaani
Na natamani wamvuruge hadi wamtapeli kila kitu .
Nasubiri waje hao wa kupiga ramli kwamba nina stress nijadili nao kinagaubaga.

Hii hata ingemkuta baba yangu mzazi Basi wavuruge haswaa hadi wamtapeli kila kitu...na hao watoto wanaoitwa wa nje sisi hatuwajui..hasa Mimi!naowajua ni ndugu zangu tu wa tumbo Moja..na asije akajichanganya akaleta huo ujinga..aisee atasimulia.
Sisi huwa hatumfichi mtu mbona.

Nasema hivi wanaume wahuni na wanaojidai miili yao inawaka sana Moto wapelekwe Moto hivyohivyo ,
Kama yameamua kuwa mazezeta sisi tufanyaje???
Mimi sijawahi kuwa na huruma na mtu kwa mambo ya kipumbavu Kama haya.

Zaidi sana nampa pole na kumuonea huruma huyo mama mke wa ndoa kwa furushi Hilo la mzigo alilolipata..Mungu wa Mbinguni amtie nguvu.
 
Labda yeye anafikiri mke hajui au ana subiri aulizwe ili atiririke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…