Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Shemeji hongera sana, upande wa kupambana na kumiliki mali ulifanikiwa sana; lakini bahati mbaya sana, pamoja na mali zote ulizozipata hazikufanikiwa kukuletea amani ya moyo. Sanasana hizo mali nyingine kama hiyo nyumba ya bi mdogo inataka kukutoa roho sasa hivi.

Wahenga walisema za kuambiwa changanya na zako; sio kila ushauri ni wa kuubeba tu kisa mzazi kasema; sio kila alichopitia yeye au anachoona yeye ni sawa kwake kitakuwa sawa na kwako. Hata kama mlikuwa mnaishi na mkeo kwa amani kidogo, ni bora mara elfu amani hiyo kidogo kuliko majanga uliyoenda kuyatafuta huko nje. Sasa hivi umebaki mwenyewe na mali zako zinazokustress.
 
Nyie Wote hapa mnapiga kelele tu,huyu mzee wetu amelogwa sio amelogwa ila kapikwa na kaiva.
Dawa yake kumkamata kinguvu afungwe kamba na kumpeleka kwa mwamposa au mganga.
Hii sio akili ya kawaida,marufuku kuoa mwanamke masikini,acha masikini waoane wenyewe kwa wenyewe'ukioa masikini utalishwa kila Haina ya uchafu
 
Una roho ya kishetani msubhati
 
Ndio maana kaleta hii news hapa. Hata kama yeye yamemkuta, lakini iwe funzo kwa wengine.
 
Wao wanasimama na mwanaume mwenzao na sisi tunasimama na mwanamke mwenzetu yule wa ndoa kila mtu apambane na hali yake

Hivi kwanza umeshaelewa au unajicommentisha tu
Hivi ni lazima ucomment?Mtoa mada aliomba ushauri na sio mashindano ya who is right and who is wrong,kama haukua na cha kumshauri ingekua bora kukaa kimya kuliko kumuattack,hujui hata anapitia emotional stress gani.Usijifiche nyuma ya screen na keyboard yako ukaona ni sawa tuu kuandika kila kinachokuja kichwani,jaribu kufikiria kama unachoandika kitaleta athari gani kwa muhusika!!
 
Kaka yangu, bora uondoe neno hilo 'mke wangu' kichwani...linakutesa mno. Nasisitiza na Mimi KUWA MWANAUME,

Uza hio nyumba igawe mara nne. Sehemu/mgao wako na watoto jenga sehemu nyingine. Atakuua huyo
 
[emoji23][emoji23][emoji23]yote haya umo tu
 
Huyu mwanamke simtaki tena, lakini naona kama anawapambe,

Nipeni ushauri wapendwa,
Maana ninachokiona siku moja huyu mwanamke anaweza rudimentary hapa kwa gia ya watoto
Hao watoto wangekuwa niwadogo sawa lakin kama ni wa kubwa wala mkuu usiumize kichwa acha awachukue watoto wake yakimshinda watoto watarudi kwako wenyewe.
 
Luv, nyumba si ya watoto. Kisheria nyumba ni ya Mme na Mke. Na kwa kuwa hao wawili wameishi miaka yote hiyo zaidi ya 20 kama wanandoa na wamebahatika kupata watoto, na urithi pekee wa watoto ni elimu kitu ambacho mleta mada amejitahidi sana kuwapatia kwa uwezp wake wote.

Sasa, mimi ninachomshauri hapo hapa ridhiki tena kwani ni kiasi gani cha fedha ambacho amekipoteza kwa ajili ya huyo mwanamke. Nyumba iuzwe na wagawane.

Cha msingi, amweleze na kumshirikisha mke wake wa ndoa kila kitu, ingawa naelewa kuwa mkewe anaelewa kila kitu kuhusu huyo baba na mwanamke wake huyo.

Amepoteza vitu vingi, kwani kupoteza hiyo nyumba kuna tatizo gani. Yeye kishasema kuwa huyo mwanamke hamtaki tena, sasa shida nini tena.
 
Mkuu hao ni single mothers ndio wans shadadia muhusika kupata shida hizo.wanajifunza kwenda kubomoa nyumba za watu,hicho ndio walichojifinza humu kwenye huu Uzi.Achana nao wanakuchosha bure.Wapo 7 hadi sasa nimempm joka jeusi aje adeal nao maana hawajaolewa na bikra Metii doi.
 
Na kama story ni ya kweli asifikiri bi mkubwa kwa vile alireact akanyamaza yameisha moyoni mwake, asubiri azeeke vizuri hakuna rangi ataacha kuona, sumu yoote aloiweka moyoni kwa bi mkubwa ishatemwa kwa watoto, anasema ana 250m akistaafu
Yaan jamaa anaona wote wako wodini milembe lakini anamcheka mwenzie
 
Umemshauri utafikiri moyo wake unaujua....kwa maelezo yake we unaona ana jeuri ya kumfanyia ivo bi mdogo
 
Mwitore.......una roho ngumu sana,pia nimvumilivu sana,
kwa micomment tuliyokuwa tunatupia humu lakini umekomaa mpaka ukamaliza story.

kwa ugumu huu,naamin hufi leo au hv karibuni.

Ushauri:Uza nyumba,ukiendelea kuwa nayo itakuuwa,
Baada ya kuuza,hifadhi 40 mil,ambayo itakusaidia kuwatengenezea biashara hao watoto wako watakapokuwa wamekosa ajira.
 
Hebu mkuu tuambie wewe umeamua nini sasa?
Mbona nimeashaamua kumwacha,
Na sasa hivi ana mwezi mzima hayupo hapa nyumbani, aliindoka kwa bila kunitaarifu,
Ila nasilkia yupo kijijini kwao

Na mimi naomba sana kwa mungu asirudi,

Sasa swali lako la mimi naamua nini,?

1- Watoto wote wapo shule, nina wasiwasi anategea warudi, likizo ya pasaka naye arudi
, ingawa kweli akirudi nitamshangaa sana,
Hapo itaanza mambo ya ugomvi tena, na tulipofikia sasa ugonvi ukianza watu wanatoka nje ( majirani)

2–nyumba sasa hivi nimeifunga hakuna mtu, ingawa bado naenda na ninalala huko wakati mwingine, sasa akirudi anikute nitamfukuza, au nitafunga nyumba Na kuondoka,
Sasa sielewiataenda kwa mjumbe au polisi, ingawa mjumbe tayari naye keshamchukia kwa tabia zake

3– sitaki mambo ya polisi tena kwenda kushtakiana,
Sasa sielewi kama polisi wanaweza kunilazimisha nimfumgulie nyumba au huo uwezo hawana, kama hawana natashukuru sana

4– labda atashawishiwa aende mahakamani,
Hilo hata mimi naona ni sawa tu,
Kama ana haki zake atapata huko

5– kama kuna wanasheria hapa ingekuwa vizuri
Kutupa darasa wanafikiri ni nini itakuwa outcome ya kesi hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…