Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Ahaaaa nacheka kama mazuri ila najiuliza wanawake wengine hii bahati wanayochezea hivi wanaitoaga wapi?.huyu dada kinachofata ni majuto. Ulosema yote yatatokea soon
 
NAENDELEA,

Kumbuka hapo tayari tumeshaamia kwenye nyumba yetu (YETU) na baada kama ya miezi sita niliingiza umeme ambao ulinigharimu kama 400000 wakati huo ( nguzo 2)

Mkuu naona kama ni rahisi kutabiri mwisho wake, all in all andika kila kitu ili moyo wako ushushe huo Mzigo ulioishi nao kwa muda mrefu hakika utapata ushauri, ila narudia tena wanaume ehhhh njia kuu ni suluhu ya magonjwa ya moyo, hivii vimchepuko vina tuendesha sana, nilishakataa kuyajenga na mchepuko, mchepuko ni wa kuwaona kama sumu maana ni parasite hawana chochote kwako
 
Yaani wanaume tumeumbwa mateso kuhangaika, kwanza hapo huenda hata hao watoto wa bi mdogo siyo wake, [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji848] namuwazia tu mwanaume mwenzangu
Unataka kumuongezea presha
 
Pole sana baba. Kwa ufupi wewe na mke mdogo soon mtaachana. Ila kachezea bahati sana atajuta atalia kwa uchungu.
 
Kipindi nipo nipo kikazi nje nilikuwa nikimtumia pesa ya matumizi kupitia rafiki yangu wa kazini, ambapo kila baada ya muda alikuwa akienda kuchukua pesa ya matumizi...
Unawezaje kufanya mambo makubwa hivyo mke wako mkubwa hajui, ila mkuu ulitolewa ufahamu kabisa
 
Kipindi nipo nipo kikazi nje nilikuwa nikimtumia pesa ya matumizi kupitia rafiki yangu wa kazini, ambapo kila baada ya muda alikuwa akienda kuchukua pesa ya matumizi...
Unawezaje kufanya mambo makubwa hivyo mke wako mkubwa hajui, ila mkuu ulitolewa ufahamu kabisa
 
Babamdogo pole na stress za dunia
Acha kijana wako nikushauri ..

- Kama bi mdogo ushamuona Ni waruwaru tafadhali hyo pesa ya nyumba asihusike nayo hata kidogo Kama ni kumumegea mpe kidogo ambayo inamfaa kulingana na akili yake uinovyo.

- Tambua Sasa huu ndo wakati wa bi mkubwa atajua ukweli wote kuhusu bi mdogo hapo patachimbika Kuanzia kwa bi mkubwa Hadi watoto wako wa bi mkubwa ..! Je Ni kwa nn nakwambia hyo hela uliyouza nyumba bi mdogo asihusike nayo?? Kumbuka apa umetangaza Vita na nyumba ya bi mkubwa Ni Bora uingie vitani ukiwa na hela kuliko kuingia vitan hela Ni kumlika kwa tochi..aisee utaona kila rangi ya dunia na kumbuka kwa Sasa kimbilio lako Ni kwa bi mkubwa huna namna Kama nyumba ushaipa mkono ..

- Tengeneza zengwe kwa bi mdogo punde installment ya mwisho ikiingia ili uachane nae kabisa

- Nikufungue macho hayo majarbu ya kipesa nk. unayopitia Ni kwa sababu ya huyo bi mdogo anakushusha chin badala akupandishe ..miradi mingapi umemfungulia na yote inabuma hujiulizi kitu apo?

- Mwisho Kama we ni wale wanaume mnadata na wivuu wa kiwango Cha SGR hamtaki kukubali Mambo basi Ushauri wetu Ni bure tunachangamsha genge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee
 
Mkuu story bado inaendelea !?
Hata robo bado ndugu yangu wewe una
wewe mawazo yako mtu akiitwa Bi mdogo basi lazima muwe mmepishana 30 au arobaini,

Hivi nimesema niko 50s na ndio kwanza imeingia na yeye yupo 42, hiyo tofauti ya miaka inaweza lingana na Mar Mengi au Ngwandu, mbona tena mimi naona nakuwa kijana sana zaidi,

Wakati nampata yeye yupo 20s , na ni 20 kweli, mimi nipo 28s na mke wangu wakati huo alikuwa 25,
Wakati mwengine am
Anza juu kwenye story ndio uchangie,

Halafu ni true storynimeomba msaada watu wanisaidie nilipo kengeuka maana mimi ni binadamu, makosa yapo, lakini a kujifunza kupo.
 
Mkuu pole sana,ushauri wangu mke mdogo mtoe katika mahesabu kabisa ila watoto wawe kipaumbele usiwaache kwani kulea mabinti siyo kazi rahisi. Baada ya hapo usiku na mchana sali Mungu akupe uwezo wa kuunganisha hao watoto wawili wa nje na familia yako kubwa. Narudia tena mke mdogo achana nae,ningekuwa wewe hata kulala nae ningeacha atakupa maradhi mzee wangu.
 
Pole sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…