Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Hapana huyu mwanamke alishaanza kuonyesha ni mshenzi tu
Mimi kwakweli hio roho ya huruma huwa sina haswa mtu akitanguliza ujinga siwezi kumsamehe mtu anae nikanyaga makusudi akitarajia akiniomba msamaha nimuelewe ndio situation kama ya huyu baba
Pale pale alipoanza kununua magodoro ndio ingekuwa mwisho wake
Kuna wanawake wanatamani mwanaume Kama huyu yeye analeta ujinga
Acha tuone mwisho wa stori unaishaje. Huenda jamaa alifanya maamuzi unayodhani ni sahihi. Binafsi so far alichokifanya jamaa, his conduct ni sahihi. Ubinadamu kwanza. That woman is a mother of his children so she deserves some respect and be treated as such.
 
Ujinga ujinga tu
Mwanaume anae hangaika na michepuko akitulia akajenga na mkewe anakuwa mbali zaidi nguvu anayo igawa huku na huku
Huyu mzee angewekeza kwa familia yake angekuwa zaidi ya hapa alipo now naamini
Kwanza mchepuko kapewa mtaji zaidi ya mara mbili kafeli aisee aaargh
Hela ngapi kapoteza na mchepuko wake na kweli angetulia na mkewe wangekuwa mbali sana acha avune alichopanda
 
Acha tuone mwisho wa stori unaishaje. Huenda jamaa alifanya maamuzi unayodhani ni sahihi. Binafsi so far alichokifanya jamaa, his conduct ni sahihi. Ubinadamu kwanza. That woman is a mother of his children so she deserves some respect and be treated as such.

Ubinadamu huo upo upande mmoja
My friend ukiishi na principle za ubinadamu utaishia kuumizwa watu wataichukulia hio kama udhaifu wako
Shida huwezi kuwa binadamu katikati ya wanyama,hujui moyo wa mtu umebeba nini
Huwa na apply ubinadamu baada ya kutendewa ila ukianza kwa unyama huwa natembea na bit hizo hizo,hii dunia haina usawa watu wazuri huishi maisha magumu kama hivyo
 
Hapa kwenye kumpa tena hela toka fungu la pili aisee nimeshindwa kukuonea huruma pamoja na makashkash yaliyotokana na fungu la kwanza.

Ungekua karibu yangu ningekunasa vibao kama vitatu hivi ili akili ikukae sawa. Shubaaamit
Kama unakumbuka,
Ndivyo ilivyandikwa kwa Advocate
 
Nimejua sasa hivi, hana mapenzi na mimi, thats why nipo hapa,
Ila bado hujajua nahitaji msaada gani
Binafsi naamini huyu bi mdogo alikuwa na mapenzi na wewe. Mwanamke mpaka kufikia hatua ya kuzaa na wewe kuna sehemu ndani ya moyo wake unakupenda. Kumbuka pia una mke mkuu, upendo wake kwako ulikuwa unakutana na kizingiti cha wewe kuwa na mke, so inabidi pia uvae viatu vyake. Pia duniani hakuna upendo unaokuja bila ya "kisababishi". Kila mtu anampenda mtu flani kwa sababu ya kitu flani. Huo ndio uhalisia. Unaweza kupendwa kwa sababu ya uhandsome wako. Unaweza kupendwa kwa sababu ya urembo wako, usingekuwa mrembo usingependwa. Unaweza kupendwa kwa fedha zako. Hakuna kupendwa bila kisababishi. Kisababishi kikitoweka either utaachwa au utavumiliwa.
 
Ushauri sahihi ila mshauriwa ataelewa baada muda sana🙏
Sema mzee kengele imegongwa ya kwenda nyumba yeye ndio anaingia getini wakati na madarasa yamesha fungwa na walimu wameondoka
Ataelewa nini muda huu ata ukimwambia tume soma moja 2 /3
Muda ndio kila kitu ukisha kosea muda okoka piga mapambio yata kusogeza
 
Ubinadamu huo upo upande mmoja
My friend ukiishi na principle za ubinadamu utaishia kuumizwa watu wataichukulia hio kama udhaifu wako
Shida huwezi kuwa binadamu katikati ya wanyama,hujui moyo wa mtu umebeba nini
Huwa na apply ubinadamu baada ya kutendewa ila ukianza kwa unyama huwa natembea na bit hizo hizo,hii dunia haina usawa watu wazuri huishi maisha magumu kama hivyo
Point yako nimeikubali "huwezi kuwa binadamu katikati ya wanyama"
 
Binafsi naamini huyu bi mdogo alikuwa na mapenzi na wewe. Mwanamke mpaka kufikia hatua ya kuzaa na wewe kuna sehemu ndani ya moyo wake unakupenda. Kumbuka pia una mke mkuu, upendo wake kwako ulikuwa unakutana na kizingiti cha wewe kuwa na mke, so inabidi pia uvae viatu vyake. Pia duniani hakuna upendo unaokuja bila ya "kisababishi". Kila mtu anampenda mtu flani kwa sababu ya kitu flani. Huo ndio uhalisia. Unaweza kupendwa kwa sababu ya uhandsome wako. Unaweza kupendwa kwa sababu ya urembo wako, usingekuwa mrembo usingependwa. Unaweza kupendwa kwa fedha zako. Hakuna kupendwa bila kisababishi. Kisababishi kikitoweka either utaachwa au utavumiliwa.
Ni kweli Konda,
Kama utakumbuka, huyu msichana nilimpata mdogo sana 19au 20 years, sidhani maamuzi aliyofanya wakati huoalikuwa na nia ya kuniangamiza, alinipenda na mimi nilimpenda,
Labda tatizo language kubwa ni kwamba, nikishakuwa na hisia za kumpenda mtu, huwa nampenda kweli, lakini naye akionesha kunipenda, huyu simumunyi mdomo naye alinipenda, ila kusema wakati huo alikuwa na malengo mabaya na mie sio kabisa?
Hiyo dhambi simpi, ni dunia tu imekuja kumharibu, na hii si una ni Dar tena
 
Mwisho wa hii story wakati nakushauri Nitgawa wtu makundi kdhaa.kuna kundi moja nitamkabidhi joka jeusi adeal nalo,hayo mengine nitadeal nayo Mimi mwenyewe.kuna watu wanatamani hizo opportunities na chance ulizompa shemej.Wengi wana maisha ya shida sana wanaokukejeli,na shida hizo hawajazitafuta.lakini kwa vile ni wajinga na wapumbavu wanataka wakukatishe tamaa.Wengi hao ni wanawake,hawajui baba zao huko nje wanamabalaa gani.sana assume they have perfect lives makwao ila siku ile can of warms ikifunguliwa hell will break lose. Wengine ni vijana ambao wapo 20's.Badala ya kufuatilia what you are going through wajifunze kitu kisiwakute wanaona wana akili.
 
Back
Top Bottom