Jibu lake lilikuwa ni kwamba unajua wewe una mke mkubwa na una familia kubwa huko unaweza kutumia kwa mambo mengine, baada ya kufikilia sana, nikaona ana hoja. Na kwa kuwa lengo ni kujengea nyumba watoto na watoto ni wake, isitoshe hata hivyosikuwa Na lengo baya, basi nilimkubalia kumpa ile pesa,
Ila baadaye nilikuja kugundua kwa mala ya kwanza kule kuwa na kiburi na kisirani kipindi kile tunasubilia pesa ni usmuzi ambao nilimwambia kuwa, basi katika hiyo pesa naomba nitoe kama 15 m ili nikapunguze madeni yangu mbali mbali angalau na mimi nipumue nijione kama kweli nafanya kazi na mshahara nauona,
Maana zaidi ya miaka mitano kusema kweli nilikuwa nikipata mshahara halafu nalipa madeni na nakopa tena hapo hapo,
Ikitokea nimefanyaovertime au nimepata kasafari kidogo ndio hapo nalipia watoto karo zao na nyingine angalau kutumia wazazi,
Lakini kiujweli hali ilikuwa mbaya sana kipesa kipindi hicho, maana nilikuwa Manila madeni, mpaka kazi yenyewe nikaichukia,ilifikia kipindi nikataka kuacha na kazi yenyewe lakini nashukuru kipindi hicho kilipita,
Sasa baada ya kumwambia nitachukua ile 15 m ili nipunguze madeni yangu ALIGOMA
Na mimi nikamwambia basi angalau 10m vilevile akagoma, basi nikamwambia sasa pesa yote tukilipwa naweka kwenye Acc yangu, hapo ndipo akakubali na nikachukua sasa 15m yote nyingine itayobaki aweke yeye,
Nikamweleza mnunuzi kiasi fulani anipe mimi na kinachobaki aweke Kwenye Acc ya mke wangu,
Kwanza alishtuka lakini baada ya kumweleshaakakubali ila akinaambia niwe makini, na nisije nikampa matatizo,
Basi fungu la kwanza ilikiluwa ni 30 m ,
15 akaniwekea mimi iliyobaki ikawekwa kwa Mama
Tunaendelea
NINI KILITOKEA?