Hivi ninavyoandika hapa, tuligombana sana mpaka kumtupia nguo zake na vitu nje, hiyo ilikuwa tar 4 mwezi huu,
Kisa nilishachoka kuondoka bila kuaga, sasa anasema amekodi mashamva huko moro, aliniaga anaenda nikamkatalia, akaenda kwa nguvu, alivyorudi nikamfukuza, na ugonvi mwingi mpaka watoto wakachangia kunitamkia maneno machafu,
Majirani wakaja wakawaombea, nikawaruhusu waingie ndani, tar 9 Jan yaani siku 4 tu toka nimkataze kwenda moro, kaenda tena bila ruhusa yangu,
Hajarudi mpaka leo,
Ila juzi nilipata taarifa ameonekana anatelemshwa Na gari ya jamaa ambaye nilishamtuhumu kuwa ana mahusiano naye kimapenzi, na hata mwezi wa 11 mwaka jana nilifuma message yake akimwalifu tayari yupo Dar
Nikaamua kumpigia simu huyo bwana nakamkoromea kuwa anaharibu famlia yangu akakataa
Baadaye ni kamuuliza bi mdogo huyo bwana anafanya shughuli gani akasema hafahamu,
Baada ya kuulizia nikasikia baba yake kastaafu kazi ya ualimu kamfungulia duka la nguo,
Hapo nyuma huo mwezi wa kumi na moja mke wangu alinionesha vi tisheti vitatu vipya na kitenge kuwa kanunua kumbe jamaa alipokuja Dar alimhonga