Naomba ushauri: Namwambia aache pombe hataki. Nampenda sana siwezi kumuacha, nifanyeje?

Umeongea point madam...
Japo daah huyu mtu ana kichwa kigumu...

Assume leo hii yupo kiwanja huko aiseee
 
Umeongea point madam...
Japo daah huyu mtu ana kichwa kigumu...

Assume leo hii yupo kiwanja huko aiseee
Angalia kampani zake Anza kukata hizo kwanza bila yeye kujua au zipunguze manage wewe ndio uwe kampani yake kuu wengi wanalewa sababu ya kampani ni wachache wanaojipanga kwenda kulewa wakiwa wenyew pekeyao
 
Asante kwa angalizo! Endelea tu kumvumilia labda ipo siku nae atakupenda kiasi cha kuacha pombe ili asikukwaze.
Asante madam kwa kunielewa namaanisha nini...
Unajua nampenda sana huyu mtu
 
Kwanza kabla ya yote mtafute mbadala wa hiyo starehe kwa kuichunguza hobbies zake nyingine (yaani ikitokea anaacha kuwe kuna kitu kina-cover up ile nafasi ya pombe) hii itasaidia.

Pili kupitia ile mifungo ya kiimani aidha kwaresma au ramadhani unachukualia hiyo advantage mnaweka dhamiri/mnafunga kwa malengo ya kwamba katika mfungo huu Mungu atutendee 123... Ikiwemo ya kuacha pombe... Na ndani yakipindi cha mfungo mnakua hamgusi pombe... Hii itasaidia kuondoa ile hamu ya pombe na kusafisha fikra (ina-clear mind)

Technically/basically mwili wa mwanadamu huwa unaji-restore kuanzia kifikra(behavioural), chemical, biological, physical and physiological changes zilizokua altered na lifestyle ya mtu.

Mazingira yanayorahisisha hili zoezi la mwili kuji-restore ni ile nidhamu(discipline(consistency)) ya kufanya kitu sahihi kwa muda na mahali sahihi, huku ikichagizwa na njaa kali (starving).

Kwanini njaa kali? Ni kwasababu mwili ukiwa na njaa kwanza unajipangilia upya ili kuendanana na mabadiliko, (metabolic processes)

Pili kwenye hayo mabadiliko mwili unahamisha mategemezi ya nishati badala ya kumtegemea chakula unachokula tu! unahamia na kula mwili, ile reserved energy(stored food) katika tishu na ogani mbalimbali za mwili inaanza kutumika, ikianza kutumika tu hapo ndio panamaajabu hata kiwango cha sumu mwilini(chemikali zilizoingia mwilini kupitia vyakula na vinywaji nazo zinaanza kutoweka(excreted out body cells, tissue organ body system and eventually out of human body)

Hata ule uraibu wa madawa ya kulevya unapungua(affinity ya mwili kwa functional group ya compounds mbalimbali inapungua (kama vile alcohol, caffeine, nicotine cocaine etc) Kwahiyo hadri unavyokua mda mrefu katika mfungo ndio mwili unavyozidi kuimarika.

Mfungo ndio mbinu pekee inayoweza kukupatia hali kali ya njaa na pia inakupatia discipline ya mambo, ukifanikiwa kufunga kikamilifu kwa muda mrefu. Utaona mabadiliko na utajifunza by experience mambo mengi na ukiwa wise enough unaweza ku apply ule ustahimilivu uliouonyesha kwenye mfungo katika mambo mengine kama vile utunzaji fedha(akiba), kuacha tabia nyingine za ovyo... Kiufupi unakua na nidhamu(discipline) na self-control nzuri kiasi kwamba kuna vitu ulikua unahisi haviwezekani au huwezi kufanya ila baadae utagundua kumbe inawezekana.
 
Angalia kampani zake Anza kukata hizo kwanza bila yeye kujua au zipunguze manage wewe ndio uwe kampani yake kuu wengi wanalewa sababu ya kampani ni wachache wanaojipanga kwenda kulewa wakiwa wenyew pekeyao
Marafiki wake wa kazini wengi siwajui hao ndo analewa nao sana..
Kuna siku hao hao marafiki zake walinichanganyia vtu nikaanza kujiskia kichwa kuuma..

Bado anafosi nitumie mashisha najaribu kumweka karibu twende sehem ambazo hakuna vilevi ila akikutoka kidogo tuu tayar unakuta kasha washa
 
Usimuache,muombee kwa Mungu kila siku bila ya kuchoka atamchomoa,na ataacha kabisa...
 
Daaah kwanza mkuu naomba nijue wewe ni mtaalamu wa afya sio..?

Maana naona umegusia vitu kitaalamu sana..
Yaani nimesoma kwa makini sana.
Kuna kitu hapa ambacho huwenda mimi nakikosea mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…