Naomba ushauri: Namwambia aache pombe hataki. Nampenda sana siwezi kumuacha, nifanyeje?

Naomba ushauri: Namwambia aache pombe hataki. Nampenda sana siwezi kumuacha, nifanyeje?

Hii ndo namna vitoto vya 2000 vinavyoingia kwenye mapenzi, mada za namna hii kinatuletea sisi sijui kinataka tukishauri nn na huyo mtoto mwezake?!.
Anyway, ukikua utaacha utoto
Mkuu mimi sio mtoto wa 2000..
Niwie radhi mkuu
 
Usimuache,muombee kwa Mungu kila siku bila ya kuchoka atamchomoa,na ataacha kabisa...
Asante mkuu mana ni wewe wa kwnza umeingizia suala la mungu katika hili daah asante sana naendelea kumuomba mungu
 
Wakuu salam

Sasa hii issue imekua very seriously..
Nachoka sana. Najaribu kumwelekeza huyu mwenzangu kuhusu pombe but still ignore me.

Ipo hivi tangu nianze mahusiano na huyu antiel D amekua mtu wa kutaka kuni fanya na mimi niwe addicted na pombe kitu ambacho mi dini yangu inakataza...

Achana na dini hata mimi kutumia hvo vitu nilishasema hapana..
Ila tangu niwe nae nimeanza kutumia japo sio sana.

Sasa kila napomshauri aachane na hivi amekua mkali kwangu na kuniambia sijui lolote kuhusu yeye..

Nimejaribu kumkwepa nisiwe natoka nae kunywa mabia sijui mapombe ila inakua ngumu sana maana anaweza kukutafutia kesi tuu ili mnuniane.

Sasa ndugu zangu hii issue na solve vipi kijana wenu..
Issue ni mimi niingie rasmi katika unywaji wa pombe ili niende nae Sawa..

Nb. Usitoe ushauri wa kumuacha still nampenda
Be you. Ukifanya jambo ambalo si lako ila unalifanya kwa kusudio la kumfurahisha mpenzi,kaka siku ukiachika maumivu yake yatakuwa makali sana. Majuto yake yatakutesa sana. Kama si mtumiaji na hutaki kuwa mtumiaji basi una machaguo mawili;
1. Mkubaliane yeye aendelee kuwa mtumiaji na wewe ukubaliane nalo jambo ilo
2. Uachane nae ikiwa bado mapema.
 
Back
Top Bottom