Naomba Ushauri: Nataka ku-import mizinga ya kisasa ya nyuki toka China

Naomba Ushauri: Nataka ku-import mizinga ya kisasa ya nyuki toka China

Unaweza kufika mkoani Tabora, katika kijiji cha Imalamakoye (wilayani Urambo) na vijiji vya Usinge, Shela na Luganjo (Wilayani Kaliua), ukutane na wateja wetu ambao tumewafanyia kazi hizi.

Karibu mkuu!

Nina safari ya Tabora mwez wa kumi katikati ..so fanya kutoa mawasiliano tunaweza kufanya biashara.
 
Nina safari ya Tabora mwez wa kumi katikati ..so fanya kutoa mawasiliano tunaweza kufanya biashara.

Mawasiliano yetu nimeweka hapo juu mkuu! Katika mkoa wa Tabora tunapatikana wilayani Urambo, mtaa wa Boma Village, barabara ya salama (jirani na Kagezi Lodge)
0784 324 102 /0755 732 981 / 0784 667 480 / 0763 424 714

Karibu.
 
Serikali ya CCM imeharibu sana akili zenu, fikiria tu watu wanaagiza nguzo za umeme afrika ya kusini.

hili ndo shida yetu wabongo ni wepesi sana kulalamika pasipo jua, je wajua kwanini wanatumia nguzo za south????? je unaweza kuwasupply hizo nguzo ukizingatia mashtti yao???? ( sio ila mti unatumika katika katumika kama nguzo ) acha kuwa rofa, ni vibaya saaaana tena mmno kujiweka katika kudi la malofa, twapenda mno short cuti katika maendeleo. ukiambiwa supply nguzo 1000,000 kila mwaka huo uwezo tuko nao???????
 
Mkuu tuwasiliane kwa mahitaji ya mizinga bora kabisa, na yakisasa! Bei zetu ni Tshs 100,000/= tu kwa kila mzinga na utaletewa mzigo POPOTE ULIPO!

Angalia picha zake hizi; View attachment 289372 View attachment 289373 View attachment 289374 View attachment 289375 View attachment 289384

Karibu.
0784 324 102 / 0755 732 981 / 0784 667 480 / 0763 424 714

Nikitaka kununua mizinga mingi mnatoa discount? Mtakuwa mnanitembelea mara kwa mara?

Na gharama ya kujenga bee house kama hiyo hapo juu inaweza kurange kiasi gani?
 
Mizinga China? Halafu tunalalamika watanzania sio wabunifu
 
bwana @John L. Mihambo ingekuwa vyema kama ungetoa abc za ufugaji wa nyuki??? ili hata sie tunaomaliza chuo na vibumu vyetu vya mwisho tuweze jitosa kwenye hilo.
mfano mazingira ya ufugaji, gharama ya ufugaji, mda wa kukomaa kwa zao( asali) toka ulipoweka mizinga kwa mara ya kwanza
 
Mizinga mingi inayouzwa Tanzania inatoka hukohuko China.
Wakija wanatupiga bei ya juu sana.
Mfano nimeona Langstroth beehive Alibaba unauzwa $35 ila hapa bongo mtu anakuambia anakuuzia 220,000.
Let say nataka kufungua bee farm ya mizinga 500-1000. Unadhani nitakuwa nimesave kiasi gani kwa kuagiza mwenyewe?

Ulitaka hakuuzie $ 35 Kwani amesafirisha bure na ulimlipiaa ushuru?
 
Nikitaka kununua mizinga mingi mnatoa discount? Mtakuwa mnanitembelea mara kwa mara?

Na gharama ya kujenga bee house kama hiyo hapo juu inaweza kurange kiasi gani?

Mkuu, mizinga tunatengeneza kwa oda maalum. Ikiwa utahitaji mingi zaidi (kuanzia 50) hapana shaka LAZIMA kuwe na punguzo!

Karibu
 
Nashukuru mkuu kwa kazi nzuri.

Nitakutafuta.

Hiyo mizinga unaweza kuvuna kwa mwaka mara ngapi?

Idadi ya uvunaji kwa mwaka inategemea na namna ambavyo umehifadhi mizinga yako (aina ya ufugaji wako). Ukifugia ndani kwenye banda (bee cage) ama nyumba maalum (bee house), uzalishaji ni wa uhakika, mkubwa na kwa idadi nyingi. Tofauti na ikiwa utafugia nje, kwa kutundika mizinga katika miti tu!

Kwa wastani uvunaji wa asali hufanyika mara mbili kwa mwaka (mwezi juni na novemba), lakini ikiwa utafugia ndani, uvunaji wa asali huwa zaidi ya hizo mara mbili.
 
John L. Mihambo .. hujajibu swali la gharama za bee house na je bee house moja inaweza kubeba mizinga mingapi??
 
hili ndo shida yetu wabongo ni wepesi sana kulalamika pasipo jua, je wajua kwanini wanatumia nguzo za south????? je unaweza kuwasupply hizo nguzo ukizingatia mashtti yao???? ( sio ila mti unatumika katika katumika kama nguzo ) acha kuwa rofa, ni vibaya saaaana tena mmno kujiweka katika kudi la malofa, twapenda mno short cuti katika maendeleo. ukiambiwa supply nguzo 1000,000 kila mwaka huo uwezo tuko nao???????
Chief una zabuni ya kuleta nguzo za umeme TANESCO toka SOUTH AFRICA, eti?
 
Mi mihambo,ebu elewa anacho hitaji mleta Uzi.labda nikufafanulie kuna mizinga ya kisasa ya aina kuu mbili ambayo ni top bar na commercial bee hive.hii aina ya commercial ndo inayotakiwa tuwe nayo ili tuzalishe kifaida.
Huyu kahitaji mizinga aina ya langstroths hii ni commercial hive nyuki wakiingia kama ni msimu WA maua baadavya siku, tisini mzinga umejaa na utakuwa unavuna kila baada ya wiki tatu.
Sasa wewe mihambo picha ya mizinga yako ni aina ya top bar,hii sana utavuna Mara moja kwa mwaka.hiyo bei ya laki moja unayouza ni kubwa ukilinganisha na mzinga wenyewe.
Langstroths bee hive ni aina ya mzinga bora WA kisasa ambao kwa hapa bongo bei ni kubwa bora uagize China itafika hapa kwa gharama nafuu kuliko utengeneze hapa.
Mfano langstroth hive two layer kwa suchuo cha sua ni 180000 na Tawiri ni zaidi ya hapo.wakati China mzinga huo huo kwa China unaununua 50000 za Tanzania tena umetengenezwa kwa ubora zaidi.
Kuhusu saizi ya nyuki ni tofauti na wahuku kwetu.kuna jamaa yangu aliagiza tukichofanya tuliwapa vipimo vya kihunzi cha nyuki wetu ambacho ni 32mm na bee spance ni 8mmm.wakatutengenezea kwa vipimo hivyo.
Mi ni mdau WA ufugaji nyuki tuache lobgolongo nakushauri kabisa agiza mizinga China wape vipimo vya nyuki WA kwetu huku watakutengenezea.utanunua utasafirisha ,utaitoa bandarini mpaka shambani bado utaokoa pesa nyingi kuliko kununua bongo.
Nakushauri top bar achana Nayo nunua .commercial hive
 
Isitoshe tofauti ya utengenezaji,ubora na mvuto ya China iko bomba yakwetu hapa nikuvurunda runda tu mbao hazirandwi vizuri Mara kwenye kona kuna tundu pamejazwa gundi,bado hatujafikia ufundi WA wachina
 
Mi mihambo,ebu elewa anacho hitaji mleta Uzi.labda nikufafanulie kuna mizinga ya kisasa ya aina kuu mbili ambayo ni top bar na commercial bee hive.hii aina ya commercial ndo inayotakiwa tuwe nayo ili tuzalishe kifaida.

Huyu kahitaji mizinga aina ya langstroths hii ni commercial hive nyuki wakiingia kama ni msimu WA maua baadavya siku, tisini mzinga umejaa na utakuwa unavuna kila baada ya wiki tatu.

Sasa wewe mihambo picha ya mizinga yako ni aina ya top bar,hii sana utavuna Mara moja kwa mwaka.hiyo bei ya laki moja unayouza ni kubwa ukilinganisha na mzinga wenyewe.

Langstroths bee hive ni aina ya mzinga bora WA kisasa ambao kwa hapa bongo bei ni kubwa bora uagize China itafika hapa kwa gharama nafuu kuliko utengeneze hapa.

Mfano langstroth hive two layer kwa suchuo cha sua ni 180000 na Tawiri ni zaidi ya hapo.wakati China mzinga huo huo kwa China unaununua 50000 za Tanzania tena umetengenezwa kwa ubora zaidi.

Kuhusu saizi ya nyuki ni tofauti na wahuku kwetu.kuna jamaa yangu aliagiza tukichofanya tuliwapa vipimo vya kihunzi cha nyuki wetu ambacho ni 32mm na bee spance ni 8mmm.wakatutengenezea kwa vipimo hivyo.

Mi ni mdau WA ufugaji nyuki tuache lobgolongo nakushauri kabisa agiza mizinga China wape vipimo vya nyuki WA kwetu huku watakutengenezea.utanunua utasafirisha ,utaitoa bandarini mpaka shambani bado utaokoa pesa nyingi kuliko kununua bongo.

Nakushauri top bar achana Nayo nunua .commercial hive

Shukrani kaka.
Nimeona ulichoongelea ni exactly na kile nilichofikiria.
Kuagiza nje ni bei rahisi zaidi kuliko kununua hapa bongo.
 
Back
Top Bottom