Naomba ushauri: Nilipokuwa nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa

Naomba ushauri: Nilipokuwa nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa

mkuu mfano nikauza nikajenga nyumba ya wapangaji? hata room 5
Niliona mwanzoni hauko kwenye wakati mzuri wa kufanya maamuzi makubwa kama hayo, na mara nyingi mno ukipata kitu kwa kufanya maamuzi Kwa kushurutishwa, Ni rahisi Sana kupoteza.

Sawa unaweza ukaiuza, ukiwa na discipline na mipango inayoeleweka unaweza ukaisimamia, nje ya hapo, hesabu maumivu hela itapotea huelewi imeenda wapi, ndio mana niliona tuuh usiuze Kwa kuwa uko kwenye mazingira magumu ya kufanya maamuzi. Utakachokipata baada ya kuiuza hiyo nyumba, kinaweza kukufunya usahau kabsa mipango yako, na hii ni kutokana na mazingira uliyopo Kwa SASA.

Usisikilize kelele za nje, tafuta namna nyingine, ya kupunguza ukali wa changamoto ulizo nazo, amini hakuna kitu kigumu Sana kama kujenga
 
Lesson learnt:
Co-workers are not your FRIENDS......Always trust nobody..
 
Usikubali maumivu ya leo yakakuondolea mali ya maisha.

Nyumba uliyojenga kwa jasho lako, kuiuza ukiwa kwenye msongo ni uamuzi unaoweza kuja kukugharimu baadaye.

Tuliza akili, tafuta njia nyingine ya kuanza upya, halafu fanya maamuzi ukiwa umetulia.

Kipato kinaweza kujengwa tena, lakini nyumba uliyouza si rahisi kuirudisha.
Bwashee wakati mwengine unaongea ya maana sana ila ngoja Sasa upige tungi🤔
 
Usikubali maumivu ya leo yakakuondolea mali ya maisha.

Nyumba uliyojenga kwa jasho lako, kuiuza ukiwa kwenye msongo ni uamuzi unaoweza kuja kukugharimu baadaye.

Tuliza akili, tafuta njia nyingine ya kuanza upya, halafu fanya maamuzi ukiwa umetulia.

Kipato kinaweza kujengwa tena, lakini nyumba uliyouza si rahisi kuirudisha.
Mwamba umemaliza. Iko hivyo
 
Nimekumbwa na changamoto ya kifedha ambapo nilipokua nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa na fitna hiyo ni baada ya mimi kujenga kajumba kangu mpaka hatua ya kupaua..

Wamenifanyia fitna baada ya kuona kahatua hako nilikopiga. Mbaya zaidi fitna hii imekuja ndo nimemaliza kupaua tu na hela yote iliishia humo kwenye paa.

Sasa sina hata mia nikafikiria niuze nyumba nianzishe biashara yoyote tu mradi nijenge tena legacy ya kipato.

Naombeni ushauri je nimewaza sawa?

Nipo kwenye depression sana wakuu.
Unapofanya maendeleo Fulani Fanya kimya kimya usiyaweke wazi kwa Kila mtu watu tunahisudiana sio Kila mtu ni mwema!!!
 
Usiuze nyumba usiuze nyumba,usiuze nyumba! Hivi nyumba nini mpaka watu mnaogopa kuuza?! Kama unapata hela nzuri uza kaanze maisha mengine.
Mzee usiseme hivyo mimi niliuza vitu vya sebuleni mwaka huu mwezi wa 3 kwa kuwa nipo single halafu sishindi home nikaona niongeze mzigo wa biashara pesa ikirudi au ikirudi maradufu ninunue vitu vizuri zaidi ya hivi.. Biashara ikawa ngumu pesa inayopatikana inakwenda kwenye matumizi muhimu tu. Hadi leo hii hiyo niliyokuwa naitaka sijaishika..hapa nilipata funzo kubwa!
 
Back
Top Bottom