Naomba ushauri: Nilipokuwa nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa

Kimbilio la haraka haraka kama umeyumba kiuchumi mpaka unakosa pesa ya kula ni kufanya kazi ya bodaboda ili upate pesa ya kula huku ukijipanga. Piga boda boda mana dhamana ya maisha yako ipo mikononi mwako!
ntafanyaje mkuu familia inalala njaa
 
Ya Siku 90 hapo inabidi usubiri sana ndiyo changamoto yake ila ya week 2 hadi 3 ni chap ila ukichukua kama haujapata kazi ndani ya miezi 6 inabidi ukae mwaka mmoja na nusu ndiyo uje kuchukua iliyobaki
Ni kweli baada ya siku 90 wanakupa mpunga wako wote au ndio vile tena danadana?
 
Nimekumbwa na changamoto ya kifedha ambapo nilipokua nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa na fitna hiyo ni baada ya mimi kujenga kajumba kangu mpaka hatua ya kupaua..

Wamenifanyia fitna baada ya kuona kahatua hako nilikopiga. Mbaya zaidi fitna hii imekuja ndo nimemaliza kupaua tu na hela yote iliishia humo kwenye paa.

Sasa sina hata mia nikafikiria niuze nyumba nianzishe biashara yoyote tu mradi nijenge tena legacy ya kipato.

Naombeni ushauri je nimewaza sawa?

Nipo kwenye depression sana wakuu.
Ombea Mkopo hiyo Nyumba ifanyie Finishing weka mpangaji fedha inayobaki anzisha biashara. Hapo utakuwa na fedha ya Kodi, na Fedha ya Biashara. Ukiona Biashara imekaa sawa muachie Wife wako, wewe anza kujichanganya Mbeya, Kahama
 
wakuu nimeamua niiuze tu, Aiseee ukiwa Huna kipato Hakuna Rangi utaacha ona na Utawajua watu vizuri. Kwa kipindi hiki cha miez mi3 nimejua tabia za watu wote wanaonizunguka
 
Pole kwa kuchelewa kulijua hilo mkuu
 
wakuu nimeamua niiuze tu, Aiseee ukiwa Huna kipato Hakuna Rangi utaacha ona na Utawajua watu vizuri. Kwa kipindi hiki cha miez mi3 nimejua tabia za watu wote wanaonizunguka
Aiseh! Pole Sana Mimi naona usiuze, tafuta namna nyingine. Naimani utakuja kujutia kwa kufanya maamuzi Kwa nyakati kama hizo
 
mkuuu nimejitahidi kujizuia nisiuze ila nimefeli kabsaaa... Masimango yamekua mengi kiasi kwamba sina namna tena kila siku unasimangwa na jambo jipya,
 
Hapana kiongozi, amini yote yatapita tafuta namna ya kujikwamua, ila hiyo nyumba usiuze huo ni uwekazi wa muda mrefu, ni jasho lako Hilo, la kujinyima sana, usiruhusu liondoke kwa shida za kupita.
 
Mkuu ipo hatua ya kuanza finish yaan nimepaua sio kwamba imeisha kabsaa yaan ndo inaanza kingereza naona sitatoboa bora niisukume nijipange upya kimaisha..
 
Sawa kiongozi, kila la kheri. Kaa utulie uone kama hayo maamuzi yako sahihi, unaweza ukaiuza ndio ikawa chanzo cha kupotea kabsa
 
mkuu mfano nikauza nikajenga nyumba ya wapangaji? hata room 5
 
Back
Top Bottom