Naomba ushauri: Nilipokuwa nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa

Naomba ushauri: Nilipokuwa nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa

Usiuze nyumba usiuze nyumba,usiuze nyumba! Hivi nyumba nini mpaka watu mnaogopa kuuza?! Kama unapata hela nzuri uza kaanze maisha mengine.
akiuza nyumba labda awe na mpango mzuri wa biashara lasivo hyo pesa pia itateketea mkuu. Kwasabab
  • ndugu yetu huyu anaonekana nimtoaji sana kusaidia ndugu na wengne.
  • hana uzoefu na biashara. na maisha ya buku naona kama haja yapitia hivi, ndo maana amehaha na kusahau UZIMA ni MTAJI.
  • hii hali ya kuzoea mshahara saiv ana stress mbaya ko akiishka hyo pesa haifk mbali make kwa sasa huenda hajui nin afanya ama wazo la biashara.

tuulize sis tuliokula kiporo cha ugari ahsubh kama chai ndo tunatoka na kujipaka mafuta ya kula mwilin. tunaish fresh hata mishe zikiyumba najua kukaza na kupanga mashambuliz upya ata kama sina pesa.

na mambo yanasonga mbele kikubwa AFYA NJEMA ndo mtaji.
 
Innashangaza sana. Pia sijui alikuwa anaenda nao site hao wafanyakazi wenzie?
hapo ndo aliferi.
Watu hatutakian mema wengne.

Anaweza mtu akaipiga pesa ofisi na kukusingzia kwa evidence kuwa umeiba ukajenga.

Yaan bora watu waje kukutembelea upo kwako, watakusifu tu upo vizuri kuliko wajue unatengeneza pango wataona unaenda kufaid na watajaa kinyongo.

Sijui ni kwanin tu.
Africa Uki-
  • Nunua GARI
  • UKIOLEWA
  • JENGA NYUMBA

watu wanaona ndo umetoboa maisha umefanikiwa.

GARI mtu ananunua kwa ajiri ya usafir binafs na linatesa service na kulihudumia ni kama unamchepuko.

NDOA nayo sana sana mtu akioa/kuolewa vijicho vinakuwa vingi kwel, utadhani wakioana watu ndo wanaenda mbingun wakat ni majukumu mazito kiakir mpaka uchumi.

KUJENGA mtu anajibana apate kwake ila vijicho wanajua katoboa daah.
wakat nyumba ni kitu cha kawaida tu
 
Ndugu yetu EricMan toka katafute ugari ukiwa pale kwako hudaiw kodi.

Kuwa mtulivu wa hakili kajichanganye na watu nje utazame wanaishije huenda utapata wazo la kupata bukubuku hzo.

Huku unatafta kaz taratibu, usipagawe mkeo awe mvumirivu tu, jichunge usimkalipie tu utakosa vyote.

Na ukifanikiwa jifunze kununua chakula cha mwaka mzima au miwili kama mahindi wakat wa mavuno tunza ndan.

Chakula kikiwa ndan hata ukikaa mwez mzima bila kazi, huwaz na unajipanga hakili ikiwa Imetulia na ina energies.
 
Nimekumbwa na changamoto ya kifedha ambapo nilipokua nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa na fitna hiyo ni baada ya mimi kujenga kajumba kangu mpaka hatua ya kupaua..

Wamenifanyia fitna baada ya kuona kahatua hako nilikopiga. Mbaya zaidi fitna hii imekuja ndo nimemaliza kupaua tu na hela yote iliishia humo kwenye paa.

Sasa sina hata mia nikafikiria niuze nyumba nianzishe biashara yoyote tu mradi nijenge tena legacy ya kipato.

Naombeni ushauri je nimewaza sawa?

Nipo kwenye depression sana wakuu.
Hao waliokufanyia fitina walijuaje kama unajenga? Sometimes tunashauriwa kuishi Low Key!

Usiueze nyumba ,chukua hiyo termination letter peleka NSSF uchukua mpunga wako baada ya siku 90 au unaweza kuchukua 33.3% ya mshahara wako mara 6 kwa mkupuo kama una njaa sana hii ni baada ya week 2 hadi 3.

Ya Siku 90 hapo inabidi usubiri sana ndiyo changamoto yake ila ya week 2 hadi 3 ni chap ila ukichukua kama haujapata kazi ndani ya miezi 6 inabidi ukae mwaka mmoja na nusu ndiyo uje kuchukua iliyobaki.
 
Sasa sina hata mia nikafikiria niuze nyumba nianzishe biashara yoyote tu mradi nijenge tena legacy ya kipato.
Usifanye hili kosa mkuu

Pole sana, omba Mungu uvumilivu na utulivu wa akili

Epuka mentality ya kutaka kurudi kama ulivyokuwa awali

Sasa hivi pambania kwanza kupata mahitaji ya lazima maishani kama chakula
 
Aisee,kuuza nyumba? Usiuze,ingekuwa nazo mbili labda,,,,ningekuwa ni mie mkeo,,ningeomba pesa home,ningefanya ki biashara tusilale njaa huku unaendelea kutafuta KAZI.
Hongera kwa kujipakulia minyama, wanakuja

Kwa ground mambo hayapo simple hivyo mdada
 
Hongera kwa kujipakulia minyama, wanakuja

Kwa ground mambo hayapo simple hivyo mdada
Wanakuja wakina nani na wapi???

Aisee mtu asichangie mada!!,

Mie,Nina wangu kitambo sana,nipo huru kuandika chochote,

Hivi wabongo mnacho waza umalaya tu,

Aisee,hunijui,sikujui.

Usipende kuvamia watu pleas,

Achana na Mimi.
 
Pole sana Mkuu

Kwa sasa calm down, Mshukuru Mungu kwa mitihani unayopitia na Muombe sana akutilie wepesi kwenye maswala ya ridhki

Kikubwa kwa sasa kipato chako kimeshuka sana so usitake kuforce kuishi kama ulivyokuwa unaishi mwanzo ukiwa na kipato cha kutosha kwa kuogopa aibu au kusemwa na ndugu na majirani ni vitu vya kawaida hiviii

Miaka ya nyuma huko kuna issue ilitokea biashara ya Mzee wangu iliyokuwa inamuingizia almost 100k kama faida kila siku ikatetereka mpaka akafilisika kabisa akawa hawezi kuingiza hata 100 hapo ni baada ya kulazwa zaidi ya 6 months hospital..........
 
Wanakuja wakina nani na wapi???

Aisee mtu asichangie mada!!,

Mie,Nina wangu kitambo sana,nipo huru kuandika chochote,

Hivi wabongo mnacho waza umalaya tu,

Aisee,hunijui,sikujui.

Usipende kuvamia watu pleas,

Achana na Mimi.
mbona mapovu?

sikujui... umeambiwa jf ni sehemu ya watu kujuana au kupeana attention?

umechangia nami nimekujibu, hoja yangu ni kuwa maisha ukiona imefikia level hiyo ya ugumu means hata hiyo ya kusema kirahisi tu unaomba pesa kwa wazazi unaanzisha biashara si kirahisi hivyo

hoja yako imejibu umalaya tu, unawaza kuwa malaya tu.

Eti achana na mimi... nakujua wewe? au jf ni ya baba yako mnajibizana na ndugu zako tu 🚮
 
Mkuu, huwezi kuwa kwenye raha wakati wote. Hata matatizo ni sehemu ya maisha. Sasa Mungu alivyo wa ajabu, utaishi na utasimama tena..

Ni changamoto za maisha ambazo kila mtu anakutana nazo. Uzuri ni kwamba yote hayo ambao unaona kama giza nene, yatapita.
 
Kila mshahara uliokuwa unaingia ulikuwa unakula ukidhani hiyo kampuni aliiacha babako ni ya milele,ulikuwa unadhani hutafukuzwa! Unawezaje kujenga wakati ulikuwa unajua ukifukuzwa kazi leo, kesho huwezi kuishi. Biashara hamna,ufugaji hufanyi, kilimo hufanyi kwa mshahara wa chini wa laki nne huku una mke na mtoto? Huna chanzo kingine cha mapato alafu unalazimisha kujenga bwa shee,kisa uheshimike mjini? Watu wanaishi kwenye nyumba za kupanga kwa miaka zaidi ya ishirini ili mradi tu awe na pesa ya kutosha kuendesha family yake pindi anapojenga na hata akifukuzwa kazi haiathiri chochote, kiukweli ndugu ulikurupuka kujenga,au mkeo kwa vile ana degree alikuwa anakwambia hawezi kuishi nyumba ya kupanga? Cha kukushauri, toka hapo mjini tafuta eneo hasa vijiji vya ndanindani nenda kule panga chumba,uza nyumba anza biashara hata ya kuuza nyanya,sabuni nk kodi shamba lima masika ikiingia. Vinginevyo utaliwa kiboga. Acha kutegemea ajira. Pole sana mkuu
 
Acha kuwaza siku zaidi ya uliyopo, itaondoa msongo na utapata ahueni. Toka asubuhi, tafuta vibarua halali vyovyote haswa kwenye ujenzi.

Una yeyote akukope mtaji upitishe biashara nyumba kwa nyumba/bar kwa bar (kama ulipo zimejaa?)
 
Hao waliokufanyia fitina walijuaje kama unajenga? Sometimes tunashauriwa kuishi Low Key!

Usiueze nyumba ,chukua hiyo termination letter peleka NSSF uchukua mpunga wako baada ya siku 90 au unaweza kuchukua 33.3% ya mshahara wako mara 6 kwa mkupuo kama una njaa sana hii ni baada ya week 2 hadi 3.

Ya Siku 90 hapo inabidi usubiri sana ndiyo changamoto yake ila ya week 2 hadi 3 ni chap ila ukichukua kama haujapata kazi ndani ya miezi 6 inabidi ukae mwaka mmoja na nusu ndiyo uje kuchukua iliyobaki.
Samahani Mkuu, hiyo ya baada ya siku 90 Hela yote inatoka?
 
Back
Top Bottom