Naomba ushauri: Nilipokuwa nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa

Naomba ushauri: Nilipokuwa nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa

Sio lazima msumi,ni vile TU kujisimamia basi,,,fursa zipo tele, watu tunauza vichori na life linaenda good.
Safi!!!! Mimi kijana wangu akitaka kuoa, lazima anihakikishie mke wake ataingiza Shillingi. Goalkeeper kwenye ukoo wangu hakuna. Tatizo wanaogopa kuwa atakwidwa, kwa sasa hata mke wa huyu jamaa akikwidwa si ni sawa tu ili familia itengamae.
 
Sikiliza bro, wakati wewe unahangaika kutafuta viatu kumbuka wenzio hawana miguu, kuuza si dhambi lakini kwanini? Muite mdogo wako muongee taratibu umueleweshe akuelewe. Lakini pia ushauri wangu wa kininga ni kuwa, hivi eneo lako lina ukubwa Gani? Lakini lipo wapi? Kwa sababu wakati mwingine unaweza kufanya maamuzi ya kukata eneo upate hela flani ya kukusaidia.
Shida sijajua thamani ya location husika inaweza ikakusaidia hii plan. Natamani nikushauri kwa simu bro 0686870530.
eneo lipo Arusha lipo 1km kutoka lami ya East Africa kwakifupi lipo sehemu nzuri sana
 
Safi!!!! Mimi kijana wangu akitaka kuoa, lazima anihakikishie mke wake ataingiza Shillingi. Goalkeeper kwenye ukoo wangu hakuna. Tatizo wanaogopa kuwa atakwidwa, kwa sasa hata mke wa huyu jamaa akikwidwa si ni sawa tu ili familia itengamae.
ni mwalimu hajaajiriwa mkuu sizan kama nilikosea jwakua nilitaraji ataajiriw
 
Safi!!!! Mimi kijana wangu akitaka kuoa, lazima anihakikishie mke wake ataingiza Shillingi. Goalkeeper kwenye ukoo wangu hakuna. Tatizo wanaogopa kuwa atakwidwa, kwa sasa hata mke wa huyu jamaa akikwidwa si ni sawa tu ili familia itengamae.
Kakwambia ni mwalimu,vile yeye hakujishughulisha na mambo ya kutafuta pa kujishikiza,.

Kila kitu kitakuwa sawa.
 
Hela ya kula inapatikana kirahisi sana,

Mwambie mkeo akachukue mahindi mabichi pale sokoni, achukue jiko la mkaa nyumbani, achome mahindi maeneo ya barabarani, hutokosa ata hela ya supu ya samaki.

Aibu yako ndio umasikini wako.​
 
haifai kukodisha maana ndo nimeipau tu hata grill haina
Sahau kuhusu status yako,ongea na wife vizuri kuwa kuna adjustment kwenye lifestyle aliyoizoea kwani umepoteza kazi.
Kama ulipojenga hapakuumizi kwa nauli endapo utapata pa kujiegesha basi bora uhamie huko uepuke gharama za kodi.
Ziba madirisha na milango hata kwa tofali (kwa kuacha space ya kupata hewa) kila uangaliw namna ya kuikimu familia,kiufupi kwa kuanzia usichague kazi.
 
hata hili nimekaa nimeliwaza sana familia ya mke wangu wanajua najiweza na wao niyakimaskini nimekua mikiwadaidia sana. hata juzi tu mke kapigiwa simu kuna msiba sina ela ya kuchanga nimewaza mnoo wanamuona kama kajipata hawajali tena uko kwa mke hali ya kua sio ivo.. kuna siku mama yake kapiga simu kuomba ela ya sabuni nikamsikia mke akijibu mama hatuna hela mama ake akamjibu kweli nyie hamna ela.. nilikua nawaskia japo ye hakuniona kama nawaskiliza kwakwel nilirudi sikugonga mlango niliwaza sanaaa usiku ule nilikuja kuridi sa tano nikasingizia mpira lakin nilikaa tu mahali nikiwaza mnoo
Pole sana mkuu
 
Katika miezi hii miwili nimepitia mambo mengi nashindwa kuelezea nimetoka kuongea na mzaz sijamuambia hali nliyonayo alichonambia kikaniumiza zaidi ni kua.. anapasua kichw amdog angu apate kitu chakufanya nikashindwa kumwambia hali nliyonayo na mimi naona kama ntampa presha sasa mimi na mdog angu ni watot wakiume pekee kwake sasa akiona na mimi nipo hali hii hatalala kabsa.. kuna siku niliwaza sana mpaka nikaona hatua ya mwisho niondoke tu huu ulimwengu.. nilishawai mpa dalali auze nyumba kuna jiran yangu alimfukuza dalali akamwambia hii nyumba haiuzwi yule jiran alinipigia tukaongea mda mrefu sanaa lakn ni msabato yeye kauli kubwa anayosema nikaombewe labda nina mapepo kwakel sikumuelewa
Hamna mapepo mkuu
Ni mapito tuu, ukianza kuingia kwenye izo imani za mapepo na makanisa ndio utapotea kabisa
 
Nimekumbwa na changamoto ya kifedha ambapo nilipokua nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa na fitna hiyo ni baada ya mimi kujenga kajumba kangu mpaka hatua ya kupaua..

Wamenifanyia fitna baada ya kuona kahatua hako nilikopiga. Mbaya zaidi fitna hii imekuja ndo nimemaliza kupaua tu na hela yote iliishia humo kwenye paa.

Sasa sina hata mia nikafikiria niuze nyumba nianzishe biashara yoyote tu mradi nijenge tena legacy ya kipato.

Naombeni ushauri je nimewaza sawa?

Nipo kwenye depression sana wakuu.
Pole sana, walikuaje unajenga? Uliwahadithia?
Anyway, njoo PM nikupe namba ya Mzee mmoja wa kule Msisi Tanga akawaroge kwa kuhamishia nyuchi zao usoni
 
Mafunzo matatu kwa vijana tunayopata hapa:
1. Usioe golikipa, hata kama kakosa kazi baada ya masomo hakikisha unamuwezesha ili mambo yako yakiyumba uwe na pa kuanzia walau hamkosi uji ndani.

2. Usioe mwanamke ambaye kwao ni maskini. Wameishi miaka 50+, maisha yanewapiga ila ghafla wanamgeuza mtaji wakati yeye yuko under 30 na hana kazi wala hawajampa biashara. Muoe kama unajiweza, unaweza kuta wewe ni rescue mission kwa familia yake.

3. Usijenge nyumba bila kipato cha uhakika. Mleta mada katumia miaka minne kujenga ila mpaka sasa ndio kapaua. Hiyo hela aliyozika ardhini mpaka sasa hawezi kuitumia, na bado kodi anakoishi analipa. Wakati angewekeza kukuza kipato kwanza hapa angekuwa amekosa kazi ila ana sehemu ya kutafutia kodi.

4. Kuajiriwa sekta binafsi ni kukaa gwaride. Mguu sawa asubuhi ila mguu pande jioni. Kama hauko special kwenye kipaji, elimu nadra kupatikana, uzoefu mkubwa, nafasi kubwa ambayo unagombaniwa basi usiharakishe kuwekeza kwenye assets zinazotumia miaka kukamilika. Wekeza kwenye chanzo cha kipato ambacho kitakuwa fall back plan endapo majungu yatakutoa kwenye kibarua.

Nimeandika sio kumdhihaki aliyeleta mada. Ni kusudi tujifunze kutokana na makosa. Hilo suala la nyumba ningekuwa mimi ningeuza, ila sasa sijui kama una mipango kama niliyonayo kichwani.
 
Back
Top Bottom