Naomba ushauri: Nilipokuwa nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa

Naomba ushauri: Nilipokuwa nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa

Nimekumbwa na changamoto ya kifedha ambapo nilipokua nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa na fitna hiyo ni baada ya mimi kujenga kajumba kangu mpaka hatua ya kupaua..

Wamenifanyia fitna baada ya kuona kahatua hako nlikopiga. mbaya zaidi fitna hii imekuja ndo nimemaliza kupaua tu na hela yote iliishia humo kwenye paa.

Sasa sina hata mia nikafikiria niuze nyumba nianzishe biashara yoyote tu mradi nijenge tena legacy ya kipato.

Naombeni ushauri je nimewaza sawa .. nipo kwenye depression sana wakuu
Hakuna jambo linatokea bila sababu katika ulimwengu wa kiroho,ndo maana maandiko yanasema shukuru kwa Kila jambo.

Mlango Mmoja wa rikizi ukijifunga,milango Saba hufunguka,tulia utaona maajabu
 
Nimekumbwa na changamoto ya kifedha ambapo nilipokua nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa na fitna hiyo ni baada ya mimi kujenga kajumba kangu mpaka hatua ya kupaua..

Wamenifanyia fitna baada ya kuona kahatua hako nilikopiga. Mbaya zaidi fitna hii imekuja ndo nimemaliza kupaua tu na hela yote iliishia humo kwenye paa.

Sasa sina hata mia nikafikiria niuze nyumba nianzishe biashara yoyote tu mradi nijenge tena legacy ya kipato.

Naombeni ushauri je nimewaza sawa?

Nipo kwenye depression sana wakuu.
Walijuaje jamani kama unajenga?
 
Katika miezi hii miwili nimepitia mambo mengi nashindwa kuelezea nimetoka kuongea na mzaz sijamuambia hali nliyonayo alichonambia kikaniumiza zaidi ni kua.. anapasua kichw amdog angu apate kitu chakufanya nikashindwa kumwambia hali nliyonayo na mimi naona kama ntampa presha sasa mimi na mdog angu ni watot wakiume pekee kwake sasa akiona na mimi nipo hali hii hatalala kabsa.. kuna siku niliwaza sana mpaka nikaona hatua ya mwisho niondoke tu huu ulimwengu.. nilishawai mpa dalali auze nyumba kuna jiran yangu alimfukuza dalali akamwambia hii nyumba haiuzwi yule jiran alinipigia tukaongea mda mrefu sanaa lakn ni msabato yeye kauli kubwa anayosema nikaombewe labda nina mapepo kwakel sikumuelewa
Sikiliza bro, wakati wewe unahangaika kutafuta viatu kumbuka wenzio hawana miguu, kuuza si dhambi lakini kwanini? Muite mdogo wako muongee taratibu umueleweshe akuelewe. Lakini pia ushauri wangu wa kininga ni kuwa, hivi eneo lako lina ukubwa Gani? Lakini lipo wapi? Kwa sababu wakati mwingine unaweza kufanya maamuzi ya kukata eneo upate hela flani ya kukusaidia.
Shida sijajua thamani ya location husika inaweza ikakusaidia hii plan. Natamani nikushauri kwa simu bro 0686870530.
 
Aisee,wakakufuatilia!!! Itakuwa Kuna best yako ulimwambia,au alisikia unaongeza na simu,
Vile baadae napitia site kucheka mafundi,blah blah.
Hayo yote nimewaza sana lakini kuna siku boda alikuja ofisini alileta bomba la maji lililobaki baada ya idara kuniwekea maji nahisi walidili nae uyo boda japo sina halika maana alikuja ofisini nikiwa sipo
 
Back
Top Bottom