Naomba ushauri: Nilipokuwa nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa

Naomba ushauri: Nilipokuwa nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa

Una mke, mgeuze asset. Mkeo ana kitu hapa umeomba apewe kazi ya kufundisha. Sasa huyo ni human capital ana akili timamu na elimu yake, mfanye awe mfanyakazi wako wa kwanza. Mko wawili tu anzisha kimradi kidogo mtakachofanya nyinyi peke yenu yaani kwenye matumizi ya mradi neno "mshahara/posho" lisionekane.

Na huwezi pata ushauri wakati location yako haijulikani uko Namtumbo au Kilosa. Hivyo kwanza sema uko wilaya gani.
nipo Arusha mjini mkuu
 
Kimbia nenda hata wilaya nyingine jipange kisha utarudi kivingine, usiuze maana hata ukiuza haina msaada wowote, pesa zitapotea mbele ya macho yako, usikope pia
 
Usikubali maumivu ya leo yakakuondolea mali ya maisha.

Nyumba uliyojenga kwa jasho lako, kuiuza ukiwa kwenye msongo ni uamuzi unaoweza kuja kukugharimu baadaye.

Tuliza akili, tafuta njia nyingine ya kuanza upya, halafu fanya maamuzi ukiwa umetulia.

Kipato kinaweza kujengwa tena, lakini nyumba uliyouza si rahisi kuirudisha.
Hujalew hadi sahii leo?
 
hata hili nimekaa nimeliwaza sana familia ya mke wangu wanajua najiweza na wao niyakimaskini nimekua mikiwadaidia sana. hata juzi tu mke kapigiwa simu kuna msiba sina ela ya kuchanga nimewaza mnoo wanamuona kama kajipata hawajali tena uko kwa mke hali ya kua sio ivo.. kuna siku mama yake kapiga simu kuomba ela ya sabuni nikamsikia mke akijibu mama hatuna hela mama ake akamjibu kweli nyie hamna ela.. nilikua nawaskia japo ye hakuniona kama nawaskiliza kwakwel nilirudi sikugonga mlango niliwaza sanaaa usiku ule nilikuja kuridi sa tano nikasingizia mpira lakin nilikaa tu mahali nikiwaza mnoo
Mkuu ushawah kukutna na phase ya magum kma hii? Mbona hii yak sio ngum kutatua. Dar kariakoo dealz kibao
 
Ukishazungukwa na WaTz wapumbavu masikini hutakiwi kuwajuza mafanikio yako. Kama ni nyumba jenga kimya kimya waje wasikie tu ulihamia kwako, kama ni gari nunua kimya kimya waje waone una park.
Tatizo lenu WaTz mnataka kujionesha mna akili za kufanya mafanikio kuzidi wengine. Walijuaje kama unajenga kama si kiherehere chako na komwe lako
 
hata hili nimekaa nimeliwaza sana familia ya mke wangu wanajua najiweza na wao niyakimaskini nimekua mikiwadaidia sana. hata juzi tu mke kapigiwa simu kuna msiba sina ela ya kuchanga nimewaza mnoo wanamuona kama kajipata hawajali tena uko kwa mke hali ya kua sio ivo.. kuna siku mama yake kapiga simu kuomba ela ya sabuni nikamsikia mke akijibu mama hatuna hela mama ake akamjibu kweli nyie hamna ela.. nilikua nawaskia japo ye hakuniona kama nawaskiliza kwakwel nilirudi sikugonga mlango niliwaza sanaaa usiku ule nilikuja kuridi sa tano nikasingizia mpira lakin nilikaa tu mahali nikiwaza mnoo
Polesana familia nazo ni changamoto
 
Ukishazungukwa na WaTz wapumbavu masikini hutakiwi kuwajuza mafanikio yako. Kama ni nyumba jenga kimya kimya waje wasikie tu ulihamia kwako, kama ni gari nunua kimya kimya waje waone una park.
Tatizo lenu WaTz mnataka kujionesha mna akili za kufanya mafanikio kuzidi wengine. Walijuaje kama unajenga kama si kiherehere chako na komwe lako
Mkuu fuatilia posts zake humo, kaishajibu hilo la walijuaje
 
Nimekumbwa na changamoto ya kifedha ambapo nilipokua nafanyia kazi wamenifanyia fitna nikafukuzwa na fitna hiyo ni baada ya mimi kujenga kajumba kangu mpaka hatua ya kupaua..

Wamenifanyia fitna baada ya kuona kahatua hako nilikopiga. Mbaya zaidi fitna hii imekuja ndo nimemaliza kupaua tu na hela yote iliishia humo kwenye paa.

Sasa sina hata mia nikafikiria niuze nyumba nianzishe biashara yoyote tu mradi nijenge tena legacy ya kipato.

Naombeni ushauri je nimewaza sawa?

Nipo kwenye depression sana wakuu.
Inauma sana kwa kweli.Hivi Braza huwezi KULOGA?
 
RUDI HUKO ULIKOKUWA UNAFANYA KAZI INGIA OFISINI UKAE HUDUMIA WATU AFU MENEJA AU BOSS ALIYEKUFUTA KAZI AITWE KUWA UPO KAZINI NA ALIKUFUTA, AKIANZA KUKUONGELESHA NYAMAZA ILA AKIFIKA PALE PA nimekufuta kazi MWAMBIE TU KIROHO SAFI KUWA "HUNA UWEZO WA KUNIFUTA KAZI WEWE BALI KUANZIA LEO NIMESIMAMA KAZI" AFU UONDOKE UENDE HOME ULALE KESHO YAKE WATAKUITA WENYEWE. Aza j3 asubuhi. Nyumba usiuze chakarika kwanza na ukubali matokeo
 
Katika miezi hii miwili nimepitia mambo mengi nashindwa kuelezea nimetoka kuongea na mzaz sijamuambia hali nliyonayo alichonambia kikaniumiza zaidi ni kua.. anapasua kichw amdog angu apate kitu chakufanya nikashindwa kumwambia hali nliyonayo na mimi naona kama ntampa presha sasa mimi na mdog angu ni watot wakiume pekee kwake sasa akiona na mimi nipo hali hii hatalala kabsa.. kuna siku niliwaza sana mpaka nikaona hatua ya mwisho niondoke tu huu ulimwengu.. nilishawai mpa dalali auze nyumba kuna jiran yangu alimfukuza dalali akamwambia hii nyumba haiuzwi yule jiran alinipigia tukaongea mda mrefu sanaa lakn ni msabato yeye kauli kubwa anayosema nikaombewe labda nina mapepo kwakel sikumuelewa
wew ni mwanaume, utaishi kivovote.

Mwanaume haitakiw kukata tamaa kwa kitu kidogo kama hiki.

Watu wanafiriska na wanaanza kujitafuta upya tena, bila kuogopa watu watanionaje.
Na wanarud njian.

Pga kaz yoyote ile ila nyumba usiuze
 
Najua hutakosa subwoofer ndani, tv na baadhi ya takataka ambazo kwa sasa huna kazi nazo. Mfano fridge, ac and many more.
Chukua bati lililobaki utengenezee mlango mkuu mmoja tu huo mwingne pamoja na madirisha ziba na vipisi vya tofali hamia ndani ya hiyo nyumba yenu, after kulala cku mbili 3 uza hayo makolokolo niliyoyataja hapo juu mixer na hiyo cmu yako upate hela ya mtaji ujitafute upya mda huo. Kipindi ulikuwa na kazi hukufanya marafiki ndio maana unateseka. Kama huna mgonjwa chonde chonde usiuze nyumba ila fundisha familia kula majani mda huu. Waambie mambo na chips, bugger cjui kuku sahau kwa mda huu anza kula chakula cha wanyama na ndege ambao ulikuwa unakula nyama zao. Mfano kuku inabidi usahau nyama yake iwe mwendo wa kande bila mafuta, mbuz anza kula mboga za majani ambazo ulikuwa huli and etc. Arusha na umekaa huko mda mrefu huwezi kukosa hata vibarua ukafanya maisha yasonge ndugu hakuna kitu kitamu utoke mjengo na f 5 yako unafikia kwako nyumba yako. Lakini rudi nyumban na f10 afu umepanga...
 
Pole sana Mkuu, kaa chini ufanye financial analysis. Jiulize ukiuza hiyo nyumba, mtaji utakaoupata utafanya biashara gani? Na je hiyo biashara una uhakika itaweza kukurudishia uwezo wa kujenga nyumba nyingine?

Bila plan, unaweza kupoteza vyote, kubwa mtulivu sana kwenye hili.
 
Pole sana na hongera kwa hatua uliyofikia ya kujenga nyumba uamuzi ulionao wa kuuza nyumba upo sahihi lakini je unapouza nyumba ile pesa ukawa umepoteza utachukua hatua gan nyingine? Waliokuachisha kazi wana lengo la kukufanya uwe na maisha magumu ili uuze hiyo nyumba yako unapouza unawapa ushindi leo utauza nyumba kwasababu umekoswa hela ya kula kesho utauza kitanda mwisho utauza hadi figo USIKATE TAMAA cha kwanza shukuru kwa hali ulionayo pili angalia unaujuzi au kipaji gan? Utumie kuigiza kipato biashara inahitaji agalau miezi 3 ndo ikupatie faida kumbuka UNAPOTATUA TATIZO MOJA UNAZALISHA MATATIZO MENGI ZAID agalia vitu ambavyo unavyo lakin havizalishi uza hivyo anza biashara
 
Naombe mnisaidie hata mke akafundishe akilipwa chochote ntashukuru ni mwalimu
hongera kwa kupata mke mwalimu mshauri kwa hali iliyopo umtafutie au umfugulie tuition center awe anafundisha analipwa kwa topic kama inawezekana tafta hata shule binafsi aobe kufundisha awe analipwa ili na wew ujipange
 
Back
Top Bottom