Hanifer Mjanja
JF-Expert Member
- Dec 10, 2019
- 217
- 329
Hello JF, nina miaka 27, sijaolewa bado ila nina mchumba na kashajitambulisha kwetu. Mimi nafanya kazi kwenye NGO ya kimataifa (ni daktari kitaaluma) nina kipato kizuri tu, huyu kaka yeye hana kazi, nimejaribu kumpa mtaji kila mara anakula mpaka sasa hivi nimechoka. Tuko kwenye mahusaino huu ni mwaka wa nne sasa. Mimi ndiyo namhudumia kwa kila kitu tunaishi kwangu lakini Kaka nalazimika kuigiza kuwa naishi kwake ili tu kumlindia heshima yake.
Namfanyia kila kitu ila ni mtu wa wanawake mpaka nachoka, anaweza kuongea na wanawake wengine mbele yangu bila kujali hisia zangu. Najaribu kuigiza kwenye mitandao, mpaka kufikia hatua nimefungua account Instagram kwa jina lake, najipost kwenye ukurasa wake ili watu wajue tu kuwa nina furaha. Ninajinunulia zawadi, nalipia tutoke out naye ili tu watu wajue ananijali lakini hakuna kitu, nimechoka na sijui nifanye nini.
Mwezi uliopita nilimpeleka kwetu, nikajilipia mahari, nikanunua pete na kugharamia kila kitu ili tu anioe kwani nyumbani kila siku wananipigia kelele kuhusu ndoa. Baada ya kuvalishana pete nikamuomba tuende Zanzibar, mimi nikalipia kila kitu lakini akagoma kwenda, kwakua nilishawaambia marafiki zangu nilimbembeleza sana akakubali ila kwa sharti aende na mwanamke wake.Nilikubaliana na sharti lake, nikamlipia hoteli yeye na mwanamke wake, akalala naye mimi nimelala mwenyewe yeye akaja kwangu kupiga picha tu.
Nimerudi niemchoka, najihisi kuchanganyikiwa kwani anataka kunioa ila sioni kama nitakua na furaha. Nilikua naamini kuwa labda atabadilika ila kila nikitafakari, akili inaniambia hakuna kitakachobadilika, ila moyo hautaki. Mama yangu anampenda, ndugu zangu wanampenda, wanajua amesoma kumbe ni darasa la saba, wanajua na kazi nzuri kumbe hata gari anayoendesha na kuzunguka wanawake zake ni yangu, nisaidieni ushauri nifanye nini? Niufuate moyo wangu au akili yangu?