Naomba ushauri nimekwama kimapenzi, niufuate moyo wangu au akili?

Naomba ushauri nimekwama kimapenzi, niufuate moyo wangu au akili?

Hanifer Mjanja sasa wewe ni mjanja wa kitu gan?
Mda umetosha sasa wa kupuuza akili yako na kuendekeza hisia zikuongoze. Ruhusu akili zako kufanya kaz sasa.

Wewe dada/kaka usijilazimishe kuwa kwenye mahusiano na mtu ambaye unaona kabisa hana sifa za kuwa mme/ mke bora wala mama/ baba bora maana baada ya yote ayo ni kujenga familia iliyo imara je hio ndio familia unayoitaka siku moja kuiona ukiijenga ya baba mpumbavu?
Maneno kuntu. Asante
 
Pamoja na kufanya kazi na NGO za kimataifa lakini naona akili ni ya kijijini.
Mtu
1. Mzinzi
2. Unamhudumia
3. Unajinunulia zawadi
4. Unajilipia magari.
5. Anakula mitaji ya biashara
Huoni kuwa uko na tapeli? Sio amebakisha tu kukuroga alale na wanawake wengine na ulipe mshahara.
Dada unawaza nini? Amka acha kujifanya uko NGO za kimataifa.

Mungu atakusaidia. Jipe moyo
Asante kwa ushauri wako. Nitaufanyia kazi.
Kwa kweli nasali sana kuomba uongozi wa roho mtakatifu.
 
nipo tayari kukuoa dada nimepata hadi simanzi juu yako
 
Iddi anazidisha sukari sana siku hizi
 
Elimu haihusiani na mapenzi mkaka
Sasa wee sii daktari u ashindwa vipi kutibu moyo wako?
Ebu wee kwa yote hayo unashindwa kung'amua kuwa jamaa hakupendi? Yaani kweli uende zenji mwenzio anaaipelekea moto mbususu ya mwanamke mwengine kwa gharama zako mwenyewe?
Are u that much desparate kupata ndoa?
 
Hello JF, nina miaka 27, sijaolewa bado ila nina mchumba na kashajitambulisha kwetu. Mimi nafanya kazi kwenye NGO ya kimataifa (ni daktari kitaaluma) nina kipato kizuri tu, huyu kaka yeye hana kazi, nimejaribu kumpa mtaji kila mara anakula mpaka sasa hivi nimechoka. Tuko kwenye mahusaino huu ni mwaka wa nne sasa. Mimi ndiyo namhudumia kwa kila kitu tunaishi kwangu lakini Kaka nalazimika kuigiza kuwa naishi kwake ili tu kumlindia heshima yake.

Namfanyia kila kitu ila ni mtu wa wanawake mpaka nachoka, anaweza kuongea na wanawake wengine mbele yangu bila kujali hisia zangu. Najaribu kuigiza kwenye mitandao, mpaka kufikia hatua nimefungua account Instagram kwa jina lake, najipost kwenye ukurasa wake ili watu wajue tu kuwa nina furaha. Ninajinunulia zawadi, nalipia tutoke out naye ili tu watu wajue ananijali lakini hakuna kitu, nimechoka na sijui nifanye nini.

Mwezi uliopita nilimpeleka kwetu, nikajilipia mahari, nikanunua pete na kugharamia kila kitu ili tu anioe kwani nyumbani kila siku wananipigia kelele kuhusu ndoa. Baada ya kuvalishana pete nikamuomba tuende Zanzibar, mimi nikalipia kila kitu lakini akagoma kwenda, kwakua nilishawaambia marafiki zangu nilimbembeleza sana akakubali ila kwa sharti aende na mwanamke wake.Nilikubaliana na sharti lake, nikamlipia hoteli yeye na mwanamke wake, akalala naye mimi nimelala mwenyewe yeye akaja kwangu kupiga picha tu.

Nimerudi niemchoka, najihisi kuchanganyikiwa kwani anataka kunioa ila sioni kama nitakua na furaha. Nilikua naamini kuwa labda atabadilika ila kila nikitafakari, akili inaniambia hakuna kitakachobadilika, ila moyo hautaki. Mama yangu anampenda, ndugu zangu wanampenda, wanajua amesoma kumbe ni darasa la saba, wanajua na kazi nzuri kumbe hata gari anayoendesha na kuzunguka wanawake zake ni yangu, nisaidieni ushauri nifanye nini? Niufuate moyo wangu au akili yangu?
Nitafute inbox nikushauri
 
Asante kwa ushauri wako. Nitaufanyia kazi.
Kwa kweli nasali sana kuomba uongozi wa roho mtakatifu.
Huna haja ya kuomba uongozi, hiyo ndoa ukiingia majuto yake yatakuwa makubwa kuliko uliyoyapitia/unayoyapitia.
I'm done
 
Back
Top Bottom